Wanawake wanaweza hatimaye tumevunja mwiko wa tangu uhuru NMB Jamii Bond yaanza kuuzwa London stock Exchange-UK

Tumpe hongera Mwanaume mwenzetu Kwa kumpa Utulivu Bi Ruthi Zaipuna hadi kuweza kufanya shughuli zake Kwa mafanikio makubwa namna hii

Wanaume tukiwawezesha Wanawake hakika wanaweza

Hongera NMB, hongera bi Ruth Zaipuna
Huu ni unyanyapaa.
Wanawake wanaweza hata bila kuwezeshwa.
 
Huku riba ikiwa kubwa, yaani mtu anafurahia NMB kuwa listed LSE ila anaona riba ya 16% ni kamawaida.
 
Wanaume wengi zaidi ya kuwaza umalaya na wizi Kuna kipi wanaweza?

Samia amewaonesha mfano kwamba wanawake wanaweza bila majigambo the same to huyo madam Zaipuna wa NMB.
 
Habari njema sana hii kwa Taifa
 
Unajua haya mambo tunayaona ni madogo kwa sababu wengi wetu jatuijui LSE,

Tanzania kuanza kuuza share zake pale tayari Wazungu wameanza kuiamini Tanzania,

Hongera sana NMB hata kama Sina mia ila mmetisha
Sawa sawa
 
Niliwahi kusema hapa huyu dada anakitu Cha ziada, Hii NMB tangu aingie huyu Mama mambo ni mengi mapya na faida ni kubwa sana

Rais Samia angeweza kumwingiza Serikalini kama Waziri angeisaidia sana Serikali.
Mkuu, tuwaache hawa wasomi. Tukiwaingiza kwenye siasa tena hizi za kibongo tutamuharibia CV tu mama wa watu, keshokutwa umsikie anatukanwa na RC ubaki kushangaa.
 
Mkuu, tuwaache hawa wasomi. Tukiwaingiza kwenye siasa tena hizi za kibongo tutamuharibia CV tu mama wa watu, keshokutwa umsikie anatukanwa na RC ubaki kushangaa.
Nimefuatilia mjadala vizuri watu wengi wanatamani mama abaki kwenye nafasi yake ile ile ya U-CEO
 
Niliwahi kusema hapa huyu dada anakitu Cha ziada, Hii NMB tangu aingie huyu Mama mambo ni mengi mapya na faida ni kubwa sana

Rais Samia angeweza kumwingiza Serikalini kama Waziri angeisaidia sana Serikali.
duh waziri tena...ila watz tunapenda kuwapa watu vyeo kirahisi tu,,,ni mtendaji mzuri lkn si kila mtendaji mzuri anaweza kuwa waziri,
 
Natoa pongezi kwa wakina mama wote wanaopambana kuleta matokeo.
 
Hongera sana Madame Zaipuna
 
Cha kusikitisha ni umaskini wa Tanzania kushindwa kununua hizo bonds za miaka mitatu kwa fixed rate ya 9.5%.

Otherwise MNB kwa unyonyaji wanaowafanyia watanzania wana faida kubwa sana na debt to equity ratio ni ndogo sana.

MNB kama taasisi kwa capital reserves walizonazo hata wakikaguliwa na rating agency yeyote wapo A+, mtaji wanaoomba na capital reserve waliyonayo ni hela ndogo sana.

Sasa kwanini wazungu wakatae hii bonanza ya 9.5% wakati bonds nyingi huko kwako ni 5%. Kwanini MNB wanaweza lipa fixed rate ya juu ivyo, kwa sababu hizo hela wanakuja kuwakopesha watanzania kwa riba za ja ajabu.

Hakuna cha akili yoyote
 
Kama kweli NMB ni shujaa kwanini haiko tayari kushindana na benki zingine katika soko huria? Serikali na mashirika yake ziache kulazimisha NMB katika malipo ya mishahara na pensheni. Acheni waajiri wajichagulie benki wazipendazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…