Wanawake wanaweza hatimaye tumevunja mwiko wa tangu uhuru NMB Jamii Bond yaanza kuuzwa London stock Exchange-UK

Wanawake wanaweza hatimaye tumevunja mwiko wa tangu uhuru NMB Jamii Bond yaanza kuuzwa London stock Exchange-UK

Unajua haya mambo tunayaona ni madogo kwa sababu wengi wetu jatuijui LSE,

Tanzania kuanza kuuza share zake pale tayari Wazungu wameanza kuiamini Tanzania,

Hongera sana NMB hata kama Sina mia ila mmetisha
Huyu Zaipuna Yuko smart mno, tunampongeza sana
 
Niliwahi kusema hapa huyu dada anakitu Cha ziada, Hii NMB tangu aingie huyu Mama mambo ni mengi mapya na faida ni kubwa sana

Rais Samia angeweza kumwingiza Serikalini kama Waziri angeisaidia sana Serikali.
Wakichangia huko kwenye mbogamboga, akili zinakuwa mgando ndugu, anakuwa chawa pro. Hutaamini kama ni yeye
 
Niliwahi kusema hapa huyu dada anakitu Cha ziada, Hii NMB tangu aingie huyu Mama mambo ni mengi mapya na faida ni kubwa sana

Rais Samia angeweza kumwingiza Serikalini kama Waziri angeisaidia sana Serikali.
Hawezi kuwa bora,,sbb serikalini kunasiasa zake zaidi,,unaona hata kimei amechemsha
 
Cha kusikitisha ni umaskini wa Tanzania kushindwa kununua hizo bonds za miaka mitatu kwa fixed rate ya 9.5%.

Otherwise MNB kwa unyonyaji wanaowafanyia watanzania wana faida kubwa sana na debt to equity ratio ni ndogo sana.

MNB kama taasisi kwa capital reserves walizonazo hata wakikaguliwa na rating agency yeyote wapo A+, mtaji wanaoomba na capital reserve waliyonayo ni hela ndogo sana.

Sasa kwanini wazungu wakatae hii bonanza ya 9.5% wakati bonds nyingi huko kwako ni 5%. Kwanini MNB wanaweza lipa fixed rate ya juu ivyo, kwa sababu hizo hela wanakuja kuwakopesha watanzania kwa riba za ja ajabu.

Hakuna cha akili yoyote
Wanazikusanya kisha wanakopesha watumishi wa umma kwa riba kubwa kisha wanakata kwenye mishahara wanawakamua kweli kweli watumishi wa umma 🤣🤣🤣. Yaani Asilimia kubwa mikopo ya nmb wanakopesha watumishi wa umma, ambao wengi sio wazalishaji. Baada ya hapo wanajiona wajaaaaaanjaaa 🤣🤣
 
Niliwahi kusema hapa huyu dada anakitu Cha ziada, Hii NMB tangu aingie huyu Mama mambo ni mengi mapya na faida ni kubwa sana

Rais Samia angeweza kumwingiza Serikalini kama Waziri angeisaidia sana Serikali.
huko akienda ataenda kulainishwa aachwe kwenye karia yake tu!
 
Niliwahi kusema hapa huyu dada anakitu Cha ziada, Hii NMB tangu aingie huyu Mama mambo ni mengi mapya na faida ni kubwa sana

Rais Samia angeweza kumwingiza Serikalini kama Waziri angeisaidia sana Serikali.
Siku akiingia tu kwenye siasa anakuwa fisadi. Siasa ni laana.
 
Sasa wakishakuwa na pesa kwanini wasijione wajanjaaa😂
🤣🤣
Kazi ya benki ni kuzipa fedha sekta zinazozalisha mali na huduma. Ili kukuza uchumi wa nchi. Sasa taarifa za fedha za nmb za mikopo zinaonesha zaidi ya 60% ya hela wanakopesha watumishi wa umma nyingine wanatumbukiza serikalini na asilimia ndogo mno ndio inaenda kwenye uzalishaji, huo ni ujanjaujanja tu 🤣🤣🤣

Watumishi wa umma wenyewe wakipewa hiyo mikopo wazalishi ni kununua magari, kuweka heshima bar, na kutafuta michepuko wenye matako makubwa 🤣🤣🤣🤣

NmB sio tena microfinance bank ni kama savings bank tu. Ni kama kibubu cha kutunza hela
 
Wanazikusanya kisha wanakopesha watumishi wa umma kwa riba kubwa kisha wanakata kwenye mishahara wanawakamua kweli kweli watumishi wa umma 🤣🤣🤣. Yaani Asilimia kubwa mikopo ya nmb wanakopesha watumishi wa umma, ambao wengi sio wazalishaji. Baada ya hapo wanajiona wajaaaaaanjaaa 🤣🤣
Si ndio maana wazungu wameona na wao wafaidike na hii biashara ya unyonyaji wanayofanyia watanzania.

Unadhani hizo bonds za MNB zingekuwa zinalipa fixed interest ya 5%, kama ilivyo rate za juu EU kwa sasa on low risk investments kama gov bonds and corporate bonds za mashirika imara kuna mtu angeangaika nao.

Wazungu washaona kupitia financial statement za MNB na kuona wana liquidity ratio nzuri kushinda industry average. MNB ni stable kwenda kuchukua 9.5% fixed interest yao is better kushinda 5% wanayopewa huko kwao. Sasa kwanini uache hii fursa ya unyonyaji.

IMG_7401.jpeg

Trend ya fixed rates za corporate bonds zenye triple A’s kwa mujibu wa Moody’s between 5%-6% na hii ni highest in since 2010. Influence kubwa ya fixed rate kufikia kiwango icho ni high central banks interest rates. Inflation ikishuka, CB wakishusha riba na hizo corporates bonds rates 5% zinashuka.

Sasa atokee mtu wa kuwapa riba ya 9.5% waachie vipi wazungu.

Hiyo hela wakipata hakuna cha uwekezaji wa jamii wala nini, wanaipeleka kwa wafanyakazi tu; mradi gani wa jamii unaweza lipa riba ya 16%+ ili hao MNB waweze mudu kulipa interest ya 9.5%.

Hizi bank ni kikwazo kwenye kuchochea uchumi, hiyo ni story nyingine na mada nyingine.

Hakuna cha ubunifu wowote na wanafanya huu unyonyaji with government blessing and little pressure shughuli za bank zijikite kwenye kuchochea macro economy.

Anyway kwa wachumi wa serikali sioni wa kuzipa pressure hizi bank kubadili tabia.

Eti huyu mama ana akili sana, akili my foot wakati anaendesha biashara ya kinyonyaji.
 
Riba za Tanzania ni za kinyonyaji sana
Na pia benki za Tz zinaendeshwa kiujanjaujanja sana! Hapo atakuja kukopesha watumidhi Kwa 14% - 17%.
CRDB zama za Kimei miaka ya 2014/25 hivi imewahi kuchukua billions IMF kwa 7% kwa miaka 5 ikaja kukopesha watumidhi kwa 18%.
Michezo ni uleule ila tu chenga zimeboreshwa.
Nyongeza: Wazungu wanatafuta njia ya kurudi Afrika kwa kasi ya ajabu. Tunashuhudia wasamii wetu wakitajwa huko majuu, muda mfupi Mh. Tuto alipata MSM's coverage pale WH akiwa3na MH. Boden n.k n.k
 
Back
Top Bottom