Wanawake wengi huondoka na watoto wakidhani wanaume watawafuata. sijui nani aliwadanganya kuwa mwanaume mtego wake ni mtoto

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Watoto uliowazaa wanaumuhimu Kwa Mwanaume pale unapoishi naye. Weka akilini hiyo.

Weka na hii Hapa, Mwanamke anaumuhimu Kwa Mwanaume pale wanapoishi Pàmoja.

Zingatia, Wanaume wengi hujiona wanawajibu Kwa wale anaowaona. Yaani waliokaribu Yake ndîo Huona umuhimu waô kuliko waliombali, asiowaona. Kisaikokojia Mwanaume huchukua hatua na kufanya reactions Kwa Kuona. Yaani macho yanaathari kûbwa Kwa Mwanaume.

Ni Kosa la kiufundi Kwa Mwanamke kutokujua Saikolojia hii.

Hata ukiwa Mke WA Ndoa, kadiri unavyokuwa Karibu na Mumeo ndivyo wajibu wa Mwanaume huyo kwako unaongezeka.

Wanawake wengi hufanya Makosa ya kiufundi ndàni ya Ndoa. Mfano, wamegombana kidôgo na Mumewe anafungasha virago anaondoka.

Hilo ni Kosa la kiufundi.

Mwanaume hanaga Muda wa kukufikiri ukiwa Mbali naye. Weka akilini hiyo.

Mwanaume anakuwa na stress pale anapokuona hauna Raha, umenuna, au haujala kisa yeye hajatafuta Hana Pesa. Na wengi hufa mapema Kwa sababu hiyo.

Unapogombana na Mwanaume ukabaki hapohapo Usiku hawezi Kulala vizuri. Lakini ûkienda kwèñu au ukiondoka nakuhakikishia atalala usingizi mtamu na haitachukua Muda atakusahau.

Mwanaume anapokufukuza nyumbani kwàke lengo lake kuu ni awe na Amani na utulivu Kwa sababu ukiendelea kukaa pale Wakati mmegombana Moyo wake hautakuwa na furaha, kula hatakula Vizuri, Kulala hatalala, akienda Bar anakuwaza tuu wewe. Anawaza atarudije nyumbani.

Uchunguzi wangu unaonyesha Wanawake wengi yàani ya zaidi ya Asilimia 90% waliojaribu kukimbia Nyumba hawakupigiwa Simu na waume zào ili warudi.

Wanawake Baadhi Yao walirudi wènyewe Kwa aibu na Hasira kuwa hata wakiondoka Mwanaume Hana uhitaji kihivyo.

Wanaume hufuatilia Wake Zao wakiwa chini ya Mmiliki Yao yàani nyumbani Kwa Mume lakini Mke akishaondoka Mume anasahau kama yeye ni Mume na Uhuru wake huongezeka.

Kûna Wanawake hufikiri akiondoka na Watoto ndîo Mume atamfuata.
 
Pia wanawake huwa wanaondoka na watoto Kama ngao au kiunganishi Cha mawasiliano na matumizi fulani maana wengi wao huwa wanakua hawana uhakika na wanakoenda akiwa na mtoto anajua hata akisema anaumwa lazima utatuma tu pesa za kuhudumia hata Kama haumwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…