Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 2,603
- 7,501
Ndugu zangu
Japo wapo wanawake wanao danga kwa tamaa zao binafsi ila wimbi kubwa la wanawake na mabinti wadogo wadangaji linalojitokeza ni kwasababu ya kukosa hela ya kununua Taulo za kike (ped) na nguo za ndani kutoka kwa waume zao, wazazi au walezi wao ili kujisitiri pindi anapoingia kwenye hedhi
Katika familia zetu wazazi wamekua wakihangaika kutafuta chakula na huduma zingine huku wakisahau kwamba wana watoto wakike waliovunja ungo ambao kila mwezi wanatakiwa wapatiwe hela za kununua taulo zao za kike na nguo za ndani kiujumla ili waweze kujisitiri kwa usahihi pindi wawapo hedhini
Pia miongoni mwa sisi wanaume wapo wanaume wenzetu ambao wao kazi yao ni kulipa kodi na kuacha hela ya chakula tuu na matumizi madogo madogo ila linapokuja swala la kununua ped na nguo za ndani za mke wake anaingia mitini kiasi cha kumfanya mwanamke kushindwa kujua ataegemea wapi pindi awapi hedhini .
Pia kuna wanaume wenzetu wenye wapenzi wao ambao kwa makusudi kabisa wanawake waliona kuliko kudhalilika wawapo hedhini ,wao wakaona wawakubali wanaume kuingia nao kwenye mahusiano ili linapotokea swala la hedhi amwombe angalau hata hela ya ped ila hao wanaume wamewajumuisha wanawake zao kwenye kundi la wapenda pesa.
Maswala yote hayo yamepelekea wanawake na mabinti wengi wadogo pindi wanapo karibia kuona siku zao (hedhi) kujirahisisha kwa wanaume wowote ili mradi tuu wapate angalau hela ya kununua ped ( Taulo za kike) kutokana na kukosa huduma hizo kwa waume , wazazi na walezi wao na kuchagua kudanga ili wajipatie kwa wanaume hela kwaajili ya kununua taulo za kike kwa lengo la kujisitiri pindi waingiapo katika hedhi
Ndugu zangu jambo hili linaleta ukakasi sana hasa kwa sisi wanaume pindi ukutanapo na mwanamke mtu mzima akidanga au binti mdogo akidanga na kukuambia nafanya hivi kipindi hichi kutokana na kukosa hela ya kununua ped( taulo za kike) na nguo za ndani kwa lengo la kunisitiri maumbo yake pindi anapoingia kwenye hedhi
###NINI KIFANYIKE KUMSITIRI MWANAMKE ASIDANGE KUPATA HELA ZA KUNUNUA PED PINDIA ANAPO KARIBIA HEDHI YAKE
1: Niwaombe wazazi , walezi na wanaume wenzetu mlio oa au wenye wapenzi angalau muwakumbuke hawa wanawake na mabinti zenu kwenye kuwanunulia ped (taulo za kike) kila mwezi, pia uwapo na mwanamke wa permanet au binti yako mbali na kuwaza kusuka au kumpa chakula muwaingize kwenye bajeti zenu ili swala la ped na nguo za ndani ili wawapo hedhini na wao waweze kujisitiri wasiaibike ili atakapo danga wakati anahukumiwa ahukumiwe kwa usahihi.
2: Niiombe serikali;
a) Kupitia wizara ya afya na ile wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wazee, wanawake na watoto kwamba wanawake wote walio vunja uongo wasajiliwe na wapewe kadi maalumu ambayo itamuwezesha kila mwezi kupata mgao wa bure wa taulo za kike mara moja bila kurudia rudia zaidi ya mara moja kwa mwezi, huko kwenye mahospitali, shuleni, vyuoni na kwenye ofisi za umma kama vile wanavyogawa condom bure kwenye vituo vya afya na sehemu zinazo fanana na hizo ( kadi hiyo iwe na mwezi january mpaka december ambako kutakua na sehemu ya kutiki idadi ya pedi alizo pewa na kusaini pembeni amfisa mgawaji na mkereketwa anae pokea
b) Serikali iongeze kodi kwenye urembo mwingine wa wanawake kama mawigi, rasta, kucha bandia, nguo zisizo na staha ,makeup na hereni ili kujikusanyia mapato yatakayoelekezwa moja kwa moja kwenye swala la taulo za kike na serikali ishushe gharama ya pedi na ifikie shilingi 200 kiwango cha chini na shilingi 500 kiwango cha juu, kwa kila pakiti kulingana na aina ya ped ( taulo za kike)
c) Serikali ijenge viwanda vyake vya umma kwaajili ya kutengeneza taulo za kike za kisasa na kuzigawa bure kwa wanawake wote waliovunja uongo kupitia utaratibu nilioelekeza kwenye kifungu (a)
d) Serikali ione kama vile kwenye ofisi kulivyojengewa visanduku vya kugawa condom za bure kwa kuzipangilia na kila mwenye uhitaji anachukua bure basi ishinikize kila taasisi iweke visanduku malum pia kwaajili ya kugawa taulo za kike za bure na kila mwanamke mwenye uhitaji na yeye awe anachukua bure.
e) Ili pia wanaume tuweze kuchangia upatikanaji wa ped ( taulo za kike) kwa bei rahisi ya kati ya shilingi 200 kiwango cha chini na shilingi 500 kwa kiwango cha juu, serikali iongeze kodi kwenye luxury commodites zote ziwausuzo wanaume wenye umri wa kwanzia miaka 18+
f) Taasisi za kidini nao waone hili na kuweka utaratibu wa kugawa taulo za kike kila mwezi wa waumini wao wa jinsia ya kike kwa wale tuu waliovunja uongo.
Naomba kuwasilisha