Wanazi wa Mabasi: Huu Ndiyo Uwekezaji Sasa!

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,266
Reaction score
25,555
Mugonile/Mlivyedi
Привет hii ni kutoka hapa chuo kikuu cha RUDN.

Moja kwa moja kwenye hoja.
Nawapongeza wawekezaji kama huyu jamaa ambaye nasikia ni kutoka nyanda za juu kusini huku mbeya.



Hizi ndiyo mashine za kazi sasa na hapa kachukua nne kwa mpigo, hii nampa 👊🏾 sababu angeweza kushuka hapo Shenzhen au Guangzhou akabeba zile taka ubishi kama bus 8 na kifungashio moja 😆!

Na nilipochungulia whatsap nikaona jamaa anasema Mkurugenzi kachukua madereva wa iliyokuwa kampuni ya Sauli wanne.

Haya wanazi na wadau wa usafirishaji, mgeni huyooo anatroti.

Sina neno ila namsifu sana huyu jamaa kwa ujasiri huu.

Watu wa mbeya mnogile!.

Nawasilisha.
Kutoka Kremlin.
 
Привет hii ni kutoka hapa chuo kikuu cha RUDN
Vipi huko rasha CHura wetu Kiziwi hajambo?
 
Shida ya biashara ya basi zinataka mtaji mkubwa faida kidogo, sifa nyingi. 😊
Mkuu hii biashara inalipa sana, asikwambie mtu, kama ingekuwa na faida kidogo kuna malegend wa usafirishaji kww mabus hadi leo wapo, unadhani kuna return mbaya?.

Kingine, faida kidogo ila wanaopiga pesa ni agents, yaani agent anagawana faida na mmiliki.
 

Nitajie legends watano ambao mpaka leo wapo kwenye biashara hii! Hii biashara ina watu wapya kila uchao, watu wanaishia kufilisika, na madeni na hii biashara.
 
Nitajie legends watano ambao mpaka leo wapo kwenye biashara hii! Hii biashara ina watu wapya kila uchao, watu wanaishia kufilisika na hii biashara.
buti la zungu ananunua magari kila mwaka inamaana pesa anaitoa wapi? King yasin alianza na 3 ila saivi zipo nyingi kwahiyo huwa wanaitoa wapi pesa ya kuongeza magari mapya?
 
buti la zungu ananunua magari kila mwaka inamaana pesa anaitoa wapi? King yasin alianza na 3 ila saivi zipo nyingi kwahiyo huwa wanaitoa wapi pesa ya kuongeza magari mapya?

Wanakopa;
Hoja yangu ni kwamba; biashara basi za abiria, haina faida ulilinganisha na mtaji wake, mtaji mkubwa return kidogo. Ndio hoja yangu, elewa hoja yangu.
 
Sasa nitajie biashara ambayo mtaji unakuwa mdogo ila faida inakuwa kubwa sana

Mkuu, umeziona hizo gari mtoa mada ameposti hapo?
Mimi sipingi biashara za watu; hoja yangu ni ndogo tuu, biashara ya basi inahitaji mtaji mkubwa kwa return ndogo au ya kusua sua. Ndio maana utaona option kubwa ya watu wa basi ni au kukopa gari au kuchukua gari za bei rahisi. Hata hivyo hatubishani.
 
Sijasema tunabishana kiongozi ila kauli zenu Kuna wajinga wengi mno humu wanaziamini....nina ndugu yangu yupo humu jamii forum kamaliza chuo ndio anakutana na wapuuzi wa humu wanadai kilimo cha kutegemea mvua ni kamari mbaya sana chakushangaza dogo nae akaamini...
 
buti la zungu ananunua magari kila mwaka inamaana pesa anaitoa wapi? King yasin alianza na 3 ila saivi zipo nyingi kwahiyo huwa wanaitoa wapi pesa ya kuongeza magari mapya?

Ukitaka kujua biashara ya mabasi ina ugumu kiasi gani, basi sikiliza simulizi za Summry...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…