Wanazi wa Mabasi: Huu Ndiyo Uwekezaji Sasa!


Kauli yangu mimi ni ndogo tuu; sijasema biashara ya basi haina faida, wala sijalenga kumpotosha mtu.
Mtoa mada ameposti gari hizo. Hizo gari kwa taarifa zangu za vijiweni, sio pesa kidogo, unazumgumzia billions of money hapobka basi hizo nne tuu.
Hiyo pesa kurudi kwake kitakuwa mwendo wa kinyonga bila kujali route zitakazokuwepo.
 
Tambua ipo hivi huyo ni tajiri mkubwa sana kama kaweza kumiliki hizo basi...nawatu wa aina hiyo hawakurupuki
 
Kujadili habari za mabasi mwisho miaka mingapi?
 
Hata kilimo nacho unadhani kina uhakika kwa asilimia zote? Mbona wengi sana kilimo kimewafilisi je napo tuseme kilimo hakina maana?

Huyo bwana bila kujali route; kuanza kula faida ya hiyo gari sio chini ya miaka mitatu au minne. Hapo tunachukulia risks zingine hamna. Sio gari ya pesa kidogo hiyo.
 
Mimi sijazungumzia utajiri wake; nimezungumzia biashara hiyo kwa uhalisia. Kama hutajali tupige hapa hesabu za uhalisia.
Tuchukulie gari hizo ataziweka route gani?
Unaona sasa ujue nilidhani tangu mwanzo unajua route atakayoenda kumbe haujui sasa tutapiga hesabu gani ?
 
Biashara ya usafirishaji wa abiria ni biashara kama zilivyo biashara nyingine.
Biashara hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, kama huna nidhamu kwenye biashara hiyo miaka miwili tu utaenda kuuza magari yako kwenye chuma chakavu.
 
Biashara ya usafirishaji wa abiria ni biashara kama zilivyo biashara nyingine.
Biashara hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, kama huna nidhamu kwenye biashara hiyo miaka miwili tu utaenda kuuza magari yako kwenye chuma chakavu.
Umeongea jambo la msingi sana nidhamu ni kila kitu nina brother wangu yupo nannyanga kupata milion 15 za korosho ni jambo la kawaida ila chakushangaza mwezi wa 7 anakuambia sina hata mia nipe kula Maua kwa bei ya sh 1000 kwa kilo
 
Namimi nikakuomba unitajie biashara ambayo mtaji ni mdogo ila faida ni kubwa sana na haina sifa

Naweza kukutajia biashara kubwa yenye mtaji mkubwa na faida kubwa. Biashara ya basi, inamtaji mkubwa faida kidogo na ya kusua sua.
Ndio hoja yangu toka mwanzo.
 
Kama biashara ya usafirishaji haina faida mbona kila siku watu wanasafiri na malori tunayaona barabarani kila uchwao.
 
Wewe utakuwa na shida binafsi na Sumry, huko juu umesema Sumry hakustui. Sasa unakataza tusifanye rejea kwa mtu ambaye kafanya biashara tunayoiongelea kwa miaka 30!
Mimi simjui hata sura yake ila taarifa zake nilizipata humu mtandaoni kwahiyo siwezi kuwa na shida binafsi na mtu nisiejuana nae kiongozi...mzee kikwete alisema akili za kuambiwa changanya na zako...summry anadai kilimo cha mahindi kinamlipa sana kiasi kwamba mtu mwingine anajiuliza mahindi hayahaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…