Wanazuoni naomba kuuliza tofauti ya fake news na propaganda : case study of Russia ukraine war

Wanazuoni naomba kuuliza tofauti ya fake news na propaganda : case study of Russia ukraine war

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,026
Propaganda ni kitu kinachotajwa sana kwenye ulingo wa siasa na vita hasa pale panakuwa na pande mbili zinazochuana kupata ushawishi wa jambo flani.

Hali kadhalika wakati wa vita ''propaganda" huchukua mkondo wake kama njia ya kuongeza au kupunguza hamasa ya mapigano kwenye uwanja wa medani.

Bila kupoteza muda naomba niende kwenye mada, baada ya uvamizi wa Russia ndani ya ardhi ya ukraine kumeonekana kuna discrepancy kubwa ya uelewa kati ya " fake news na propaganda'' hali hii imetokana na watu wengi kuwa na mahaba na upande flani.

Kwa faidi ya msomaji naomba kuwakaribisha nguli wa vita na siasa na vita kutoa ufafanuzi juu ya '' fake news na propaganda"

asanteni sana
 
Fake News Kama jina lake ni habari ya uongo

Propaganda ni hoja inayokulazimisha wewe (bila kujua) kufikia hitimisho analotaka mtoa hoja (agenda yake)

Chukua Vita ya Tanzania na Uganda

Hizi zote mbili ni Propaganda zenye agenda mbili tofauti.

"Majeshi vamizi ya Tanzania yamemuondoa kiongozi thabiti wa Uganda"

"Majeshi ya ukombozi ya Tanzania yameikomboa Uganda kutoka kwa dikteta mla nyama za watu"

Kiufupi, Fake News ina deal na tukio au matukio ya kubuni ambayo hayajawahi tokea

Mfano
"Rais Samia alikutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, ikulu ya magogoni, Aug 24, 2021"

Propaganda ina deal na matukio yaliyotokea kweli, ila inachofanya ni ku change perception kulingana na agenda ya propagandist

Kwa case ya Russia na Ukraine

Hizi ni Propaganda

1.Majeshi vamizi ya Urusi yamelipua hospital na kusababisha vifo vya watu 10, wakiwemo watoto wachanga wawili

2.Urusi imeapa kuondoa itikati za kinazi katika jeshi la Ukraine.

Ni kweli Hospital imelipuliwa, na kuua watu 10.
Lakini haikukusudiwa, lakini sisi tunachukua hili tukio na kulisimulia kwako katika namna inayofikisha agenda yetu (Urusi ni ovu)

Ni kweli, kuna wa Nazi kwenye jeshi la Ukraine, lakini lengo letu la kuivamia Ukraine ni kuizuia isiwe mwanachama wa Nato kwa usalama wa Nchi yetu, so tunatumia kisingizio cha kupambana na u Nazi kutimiza Agenda yetu (Kuivamia Ukraine)

Fake News ni
"Sadam Hussein ana silaha za Nyuklia au China wamevunja sanamu la Buddha"
View attachment 2337107
 
Fake News Kama jina lake ni habari ya uongo

Propaganda ni hoja inayokulazimisha wewe (bila kujua) kufikia hitimisho analotaka mtoa hoja (agenda yake)

Chukua Vita ya Tanzania na Uganda

Hizi zote mbili ni Propaganda zenye agenda mbili tofauti.

"Majeshi vamizi ya Tanzania yamemuondoa kiongozi thabiti wa Uganda"

"Majeshi ya ukombozi ya Tanzania yameikomboa Uganda kutoka kwa dikteta mla nyama za watu"

Kiufupi, Fake News ina deal na tukio au matukio ya kubuni ambayo hayajawahi tokea

Mfano
"Rais Samia alikutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, ikulu ya magogoni, Aug 24, 2021"

Propaganda ina deal na matukio yaliyotokea kweli, ila inachofanya ni ku change perception kulingana na agenda ya propagandist

View attachment 2337107
Fake news pia inaweza kuletwa kwa lengo la propaganda. Unakumbuka ile habari iliyoenezwa na Chombo cha habari cha serikali kuhusu Donald Trump kumpongeza Rais Fulani wa Tanzania? Ile si tu ilikuwa fake, Bali pia ilitaka kuonyesha "even the Giant" wanamkubali Mteule wa Mungu.
 
Yah, wanasiasa haswa wasio na uzoefu sometimes wanatumia "Fake News" wakidhani ni Propaganda.
Professionals wanakuletea ukweli huo huo kwa maneno mengine
 
Yah, wanasiasa haswa wasio na uzoefu sometimes wanatumia "Fake News" wakidhani ni Propaganda.
Professionals wanakuletea ukweli huo huo kwa maneno mengine
Ni ukweli kabisa wanasiasa wengi huja na fake news wakidhani ni " propaganda ''
 
Back
Top Bottom