Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 673
- 865
Wadau,
Naitwa Fredrick Mboma. Ni Mjasiriamali.
Kuna sheria ndogo mpya inayoitwa Microfinance (Non-Deposit Taking Microfinance Service Providers) GOVERNMENT NOTICE NO. 679 Published On 13/9/2019 (nimeiambatanisha)
Ni miongoni mwa sheria mbovu kabisa ambazo zimetungwa kusimamia sekta husika. Na nina uhakika kwa kiasi kikubwa sheria hii imetungwa bila ya kuwashirikisha wadau, maana sikuona tangazo lolote la kuwaita wadau wajitokeze kuchangia mawazo.
Yaani hii sheria imetungwa ili kusimamia wakopeshaji ambao ni watu binafsi lakini inasema eti mtaji wa kuanzia ni Tshs. milioni 20.
Pia ada kwa mtu binafsi (sole proprietor) ya kuomba leseni ya kukopesha ni Tshs. 300,000/-, wakati kusajili Sole Proprietor BRELA ni Tshs. 15,000/- tu.
Kwa lugha nyingine BRELA wanaelewa Sole Proprietor ni mtu wa aina gani kifedha, lakini waliotunga sheria hii ya mikopo hawaelewi.
Wakopeshaji binafsi kwa ufupi ndo Wamachinga wa sekta ya mikopo. Ni biashara ambayo mtu anaweza akaanza hata na Tshs. 100,000/- tu. Lakini hawa waliotunga hii sheria wameitunga kana kwamba wakopeshaji wadogo ambao ni watu binafsi nao ni mabenki au ni mataasisi kama PRIDE, FINCA au UTT.
Ukiondoa hiyo minimum capital ya Tshs. milioni 20, bado kuna utitiri mreeeefu wa masharti kama vile kuandaa audited financial statements, kubadili auditor kila baada ya miaka mitatu, kuajiri internal auditor, n.k.
Haya ni mambo ambayo yana mashiko kwa Kampuni kwa sababu zina wadau wengi, na pia yana mashiko kwa Wakopeshaji ambao wanaruhusiwa kuchukua deposits kwa kuwa watakuwa wanakaa na hela za watu.
Lakini wakopeshaji ambao ni watu binafsi hawachukui deposits za wateja, na wanatumia hela zao wenyewe za kutoka mifukoni, sasa hata akipata shoti akafilisika hamuumizi mtu maana ni hela zake mwenyewe.
Sheria hii ni sawa na kuwataka wamachinga wafanye biashara kwa kufuata Sheria ya Makampuni (Companies Act).
Na kwamba usipoifuata sheria hii unakuwa umefanya kosa. Yaani sasa hivi wewe ukiwa na vijihela vyako ukamkopesha mtu kishkaji anaweza akakuruka asikulipe na ukienda Mahakamani akakushinda kwamba huna leseni ya kukopesha. Wakati leseni yenyewe ndo inatwakiwa uipate kwa masharti ambayo hayaendani na hali zetu halisi.
Nani yuko tayari kuchangia gharama za kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga hii sheria mpya?
Tuwasiliane INBOX