Wangapi mko tayari kuchangia gharama ya kesi ya kuomba kurekebishwa Sheria ya Mikopo?

Wangapi mko tayari kuchangia gharama ya kesi ya kuomba kurekebishwa Sheria ya Mikopo?

Mwanafalsafa

Platinum Member
Joined
Jun 24, 2007
Posts
673
Reaction score
865
Wadau,

Naitwa Fredrick Mboma. Ni Mjasiriamali.

Kuna sheria ndogo mpya inayoitwa Microfinance (Non-Deposit Taking Microfinance Service Providers) GOVERNMENT NOTICE NO. 679 Published On 13/9/2019 (nimeiambatanisha)

Ni miongoni mwa sheria mbovu kabisa ambazo zimetungwa kusimamia sekta husika. Na nina uhakika kwa kiasi kikubwa sheria hii imetungwa bila ya kuwashirikisha wadau, maana sikuona tangazo lolote la kuwaita wadau wajitokeze kuchangia mawazo.

Yaani hii sheria imetungwa ili kusimamia wakopeshaji ambao ni watu binafsi lakini inasema eti mtaji wa kuanzia ni Tshs. milioni 20.

Pia ada kwa mtu binafsi (sole proprietor) ya kuomba leseni ya kukopesha ni Tshs. 300,000/-, wakati kusajili Sole Proprietor BRELA ni Tshs. 15,000/- tu.

Kwa lugha nyingine BRELA wanaelewa Sole Proprietor ni mtu wa aina gani kifedha, lakini waliotunga sheria hii ya mikopo hawaelewi.

Wakopeshaji binafsi kwa ufupi ndo Wamachinga wa sekta ya mikopo. Ni biashara ambayo mtu anaweza akaanza hata na Tshs. 100,000/- tu. Lakini hawa waliotunga hii sheria wameitunga kana kwamba wakopeshaji wadogo ambao ni watu binafsi nao ni mabenki au ni mataasisi kama PRIDE, FINCA au UTT.

Ukiondoa hiyo minimum capital ya Tshs. milioni 20, bado kuna utitiri mreeeefu wa masharti kama vile kuandaa audited financial statements, kubadili auditor kila baada ya miaka mitatu, kuajiri internal auditor, n.k.

Haya ni mambo ambayo yana mashiko kwa Kampuni kwa sababu zina wadau wengi, na pia yana mashiko kwa Wakopeshaji ambao wanaruhusiwa kuchukua deposits kwa kuwa watakuwa wanakaa na hela za watu.

Lakini wakopeshaji ambao ni watu binafsi hawachukui deposits za wateja, na wanatumia hela zao wenyewe za kutoka mifukoni, sasa hata akipata shoti akafilisika hamuumizi mtu maana ni hela zake mwenyewe.

Sheria hii ni sawa na kuwataka wamachinga wafanye biashara kwa kufuata Sheria ya Makampuni (Companies Act).

Na kwamba usipoifuata sheria hii unakuwa umefanya kosa. Yaani sasa hivi wewe ukiwa na vijihela vyako ukamkopesha mtu kishkaji anaweza akakuruka asikulipe na ukienda Mahakamani akakushinda kwamba huna leseni ya kukopesha. Wakati leseni yenyewe ndo inatwakiwa uipate kwa masharti ambayo hayaendani na hali zetu halisi.

Nani yuko tayari kuchangia gharama za kufungua kesi Mahakama Kuu kupinga hii sheria mpya?

Tuwasiliane INBOX
 
Attachments

Ngoja nikukumbushe hili sakata lilipoanza nakuleta huu ujinga naimani mh rais ajui kilichopo nyuma ya pazia kuna hili sakata

Baada ya hili sakata wakopeshaji wa kadi inchi nzima waliogopa serikali iliwakalia kooni kwa sababu walikuwa wanafanya biashara kinyume na sheria

Baada ya hapo hawa maboss inchi nzima wakaitana Dodoma, wakatafuta hotel nzuri wakachanga pesa nzuri kila tajiri wakawaita viongozi wa serikalini wakiomba sheria hii itungwe viongozi wenye dhamana wakaona hapana haiwezekani

Basi hawa matajiri wakaitana tena wakachangishana pesa nyingi sana wakatumia watu kwenda serikalini wanaanza kucheza na wizara ya feza kuwahonga ili waweze kutungiwa hii sheria wamehonga pesa nyingi sana yani wamehonga kupita maelezo lengo sheri a iwepo iwape Uhuru wakuendesha biashara zao ambazo zipo kinyumbe na utaratibu za inchi na ni zakihujumu uchumi

Kwaiyo hiyo sheria imetungwa baada ya kundi furani kuhonga pesa ili wakafanye mambo yao uko mitaani

Ajabu vyombo vya usalama vipo unajiuliza hawajui haya mambo yani kiufupi viongozi wa serikali wamekuwa corrupted na hili genge la wakopeshaji wa mitaani maana jamaa ni wizi wanawanyonya sana watu

Ngoja ipo siku takuja na Uzi mzima wamehonga bei gani mpaka wametunguiwa sheria hii ya hivyo na inayoenda angamiza taifa
 
Na wadhibitiwe kukaa na ATM za watumishi
Hilo genge la kukaa na ATM card ndio limekomaa hii sheria itungwe ili wawe huru kuendesha mambo yao hii sheria ya kihuni sana mh rais akiona hii I swear anaifutilia mbali sheria ya kipumbafu sana unaenda haribu uchumi
 
Unataka kumaanisha kwamba Bunge letu liko cheap and corrupt kwa kiasi hicho, genge lawatu linaweza kununua Bunge zima, kama ni kweli hi sio nchi tena
 
Unataka kumaanisha kwamba Bunge letu liko cheap and corrupt kwa kiasi hicho, genge lawatu linaweza kununua Bunge zima, kama ni kweli hi sio nchi tena
Amini nachokwambia na ndio maana mdau hapo juu unaona analalamika kuwa mbona huo muswada haujaletwa wadau watoe mawazo yao kuna uhuni umefanyika wakiamini hili suala lina wadau wachache so halitaweza ibua hisia za watu
 
Sasa mtu anakopesha hela yake audited financial statements za nini? Kwa sababu kazi ya financial statements ni kuwapa 'users' kama investors, creditors,etc picha ya mwenendo wa biashara. Internal auditor wa nini? Rotation of external auditors wa nini?

Nadhani hapa Serikali inataka hawa walipe kodi, yoote hiyo lengo ni makusanyo ya kodi tu.

Hii inawaongezea running costs wakopeshaji wenyewe wataacha mbona.
 
Hapana,walipe kodi kwani wanatoza riba kubwa mno hivyo wacha walipe tu.

Binafsi niliwahi shauri walipe kodi kupitia JF:

Watu binafsi wanaofanya biashara ya kukopesha kwa riba, wana riba kubwa,hawalipi kodi na hakuna sheria inayowabana.
 
Hatupo tayari kuchangia gharama zozote.

Kwani wabunge kazi yao nini? Si kutunga na kurekebisha sheria? Nenda kawakinaishe wabadili sheria kama unaona una hoja ya maana.

Usituletee mambo ya michango hapa. Tuliyonayo tumboni inatutosha.
 
Akiona vipi? Kwani ili iwe sheria anaye sign ni nani?
Hilo genge la kukaa na ATM card ndio limekomaa hii sheria itungwe ili wawe huru kuendesha mambo yao hii sheria ya kihuni sana mh rais akiona hii I swear anaifutilia mbali sheria ya kipumbafu sana unaenda haribu uchumi
 
Unataka kumaanisha kwamba Bunge letu liko cheap and corrupt kwa kiasi hicho, genge lawatu linaweza kununua Bunge zima, kama ni kweli hi sio nchi tena
Ukweli bunge letu limepoteza uhalali wa kuitwa bunge. Kuna mambo mengi sana yameenda sivyo ndivyo chini ya Spika huyu. Kwahiyo, hata bila kuhongwa, bunge la wabunge wengi wa ccm wasio fikiri wanaweza kupitisha upuuzi wowote kwasababu tu kufanya hivyo hakumnyimi posho na mshahara wake kama mbunge.
 
Mkuu mletamada, mbona hiyo no Rasimu tu ya Kanuni husika? Dada FaizaFoxy , hizo ni sheria ndogondogo ambazo hazitungwi na Bunge na hivyo Wabunge hawahusiki katika hilo. Mara nyingi sheria ndogo hutungwa na Waziri au Rais.
 
Hiyo ni sheria ndogo au ni hizo ni kanunuzi zitazotumika sambamba na sheria ya Microfinance ya mwaka 2018?
 
Hatupo tayari kuchangia gharama zozote.

Kwani wabunge kazi yao nini? Si kutunga na kurekebisha sheria? Nenda kawakinaishe wabadili sheria kama unaona una hoja ya maana.

Usituletee mambo ya michango hapa. Tuliyonayo tumboni inatutosha.
Mmmh inaonekana wewe mdau wa huu mswaada
 
Back
Top Bottom