tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia Chama Cha Kijamii (CCK), David Mwaijojele, ametaja moja ya changamoto kubwa kwa watumishi wa umma kuwa ni hofu ya kustaafu, akisema wengi wao hukosa ujasiri wa kuacha kazi hata wanapofikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza leo Jumanne, Agosti 12, 2025, baada ya kukabidhiwa rasmi fomu za kugombea urais, Mwaijojele amesema sababu kuu inayowafanya baadhi ya watumishi wa umma kusita kustaafu ni kutokujua watakwenda wapi au kufanya nini baada ya maisha ya ajira.
Soma pia:
“Watu wengi wanaogopa kustaafu kwa sababu hawajajiandaa kisaikolojia wala kiuchumi. Hawajui wataishije au watakaa wapi baada ya kazi. Lakini suluhisho lipo,” amesema Mwaijojele, bila kufafanua kwa undani mapendekezo ya chama chake katika kushughulikia changamoto hiyo.
Mwaijojele ameahidi kuweka wazi mikakati ya CCK kuhusu masuala ya wastaafu katika kampeni zake za urais.
Hata hivyo, Mwaijojele amesema moja ya mikakati ya kuwawezesha watumishi wa umma kunufaika baada ya kustaafu ni kuanzishwa kwa mpango maalumu wa makato ya kodi, ambapo sehemu ya mapato yao itahifadhiwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi.