Wangapi tuliwahi kucheza mchezo hatari wa 'kula mbakishie baba' utotoni?

Kombolela, kidali po, mdako, kibaba na mama, makida makida, ya nchi, gololi mpunano, kuendesha maringi na magari, mpira wa visoda, matobo, kuruka kamba, kula mbakishie baba, kujipikilisha, kuchezesha vichupa, kushindana danadana, daaaah... Hii michezo ilitakiwa angalau iwekwe kwenye documentary kama kumbukumbu... Imeshapotea na mitoto ya siku izi ndomana inakua kama mazezeta vileee....
 
Hahahhaha..jamani si mlikua kama vikobo loh!
 
Hahahahahaa na ukikimbia unaitwa mtoto wa mama.
Sasa raha ya kula mbakishie baba ule mchanga ukibaki kidooogo kijiti kinakaribia kuanguka, watu wanakuwa wanategea kula basi inaanza zamu ya kupiga tonge moja moja mnaenda kwa zamu sasa hapo mtu anadokoa wengine wako standby kumkimbiza au kumuwahi kwenye nguzo!

Ila mimi nilikuwa nawaweza kwenye kombolela, wakienda kujificha na mimi naenda zangu kujificha home!
 
[emoji23] Kula mbakishie baba huo mchezo sitausahau enzi hizo nipo boma ng'ombe, mtaani ndiyo tunahamia na Sanya juu nilipotoka ilikuwa ni kutocheza sana michezo hiyo. Mzee anabana.

Mungu wangu si nikakuta watu wanacheza kwenye uwanja, kushika ni bomba lipo kando ya uwanja. Sijui kama kuna mchezo huo, ndiyo kwanza naona na sina habari kuna mabanzi. Mtoto wa kufugwa mimi nikaangusha kijiti, nilichezea mabanzi hadi nikaangua kilio.

[emoji2] mtifu uliyofuatia hapo vilio vilifuata kwao waliyonipiga, bro wangu hakuwa mbali alivamia alitembeza kibano kwa wote waliyonipiga.
 

Hahahahahahahahhahhaaa I can see the way you were.....

Those were the days.

Hivi muhimbili shuleni walikuwa wanacheza komborela? Au ilikuwa mpira wa miguu tuu pale uwanjani?

Ila yale yalikuwa maajabu.... Yaani madarasa tofauti tofauti kila darasa na mpira wake wote wanacheza kwenye uwanja mmoja na hawachanganyani hata....
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 


hohohoho nacheka kijapani
kidari poo ni nomah
 
Ulikua mayaimayai
 
Nakumbuka mchezo wa vipande..rede ya kuhesabu vyumba..dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…