Wangapi wanamuunga mkono mbunge Msambatavangu?

Wangapi wanamuunga mkono mbunge Msambatavangu?

passion_amo1

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
1,828
Reaction score
3,922
Wakuu Heshima mbele!

Jana nilipokuwa natazama vikao vya bunge vinavyoendelea Dodoma.

Mbunge msambantavangu alikuwa akizungumza kuhusu ukatili wa kijinsia, anasema imekuwa ni kawaida kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wakike na wamama, lakini Kwanini si kwa watoto wakiume? Kwani watoto wakiume hawafanyiwi ukatili wa kijinsia?

Kwanini bajeti ni kwa ajili ya kumuwezesha mtoto wakike tu na si wakiume pia kama ni usawa wa kijinsia?

Msikilize hapa chini👇

View: https://www.youtube.com/watch?v=xtinj83xrDo

Wangapi wanamuunga mkono Mbunge msambatavangu?
 
Naunga mkono hoja, tunakoelekea kutakuwa na gap kubwa sana kati ya ke na me kwa namna upande mmoja unavyopewa thamani na kipaumbele kuzidi mwingine.
 
Kaongea ya maana sanaa sanaa sifuatilii bunge ile nmeona klip kwa milad na huwa siangaliagi ila hii mwanzo amenishawishi kusikiliza hadi mwisho.
Congrats mama.
 
Namuunga mkono,tustuke jamani maana kasi ya kumuangusha mwanaume imekuwa kubwa mno na sisi wenyewe tunaisapoti bila kujua
Kabisa kuna mtu aliwahi kuniambia kwa namna sapoti kubwa inavyoelekezwa kwa wanawake kwenye mambo mengi kwenye jamii ni ishara ya wazi baada ya miaka michache watatuacha mbali sana kwenye mambo mengi. Naanza kulishuhudia hilo.
 
Watoto wa kiume wanaofanyiwa ukatili wazazi wengu wanaficha wakiogopa mtoto atacheka na jamii

Wanaona ukakasi kusema "kijana wangu kalawitiwa"
 
Huyu mama Ana akili Sana anaongeaga mambo ya msingi bungeni 2025 arudi tu bungeni hata kwa kupitia viti maalumu.
 
Kabisa kuna mtu aliwahi kuniambia kwa namna sapoti kubwa inavyoelekezwa kwa wanawake kwenye mambo mengi kwenye jamii ni ishara ya wazi baada ya miaka michache watatuacha mbali sana kwenye mambo mengi. Naanza kulishuhudia hilo.
Silipendi sana hili suala,tukomaeni kulipunguza,na tuanzishe ajenda kubwa kuwasimamisha wanaume imara.
 
Namuunga mkono,tustuke jamani maana kasi ya kumuangusha mwanaume imekuwa kubwa mno na sisi wenyewe tunaisapoti bila kujua
Wanaume tumekubali kuingia kwenye mfumo wakuharibu familia.Hizo porojo za 50/50 lengo lake liko mbali sana nawala sio upendo kwa wanawake kama tunavyojifariji.Tumekubali kupoteza heshima yetu kama kichwa.Tupo tupo tu kama mazezeta.Miaka ijayo tutegemee kizazi cha ovyo kupindukia.Kwasababu mwisho wake ni wanawake watapoteza na wanaume watapoteza na jamii itakua mfu.
 
Namuunga mkono,tustuke jamani maana kasi ya kumuangusha mwanaume imekuwa kubwa mno na sisi wenyewe tunaisapoti bila kujua
Watoto wa kiume kutwa kukatikakatika mauno
Wanacheza singeli sjui amapiano
Watoto wa kiume wanavaa vipuli
Puani mguuni vikuku 😄
Lazima waliweee sana

Ova
 
Wanaume tumekubali kuingia kwenye mfumo wakuharibu familia.Hizo porojo za 50/50 lengo lake liko mbali sana nawala sio upendo kwa wanawake kama tunavyojifariji.Tumekubali kupoteza heshima yetu kama kichwa.Tupo tupo tu kama mazezeta.Miaka ijayo tutegemee kizazi cha ovyo kupindukia.Kwasababu mwisho wake ni wanawake watapoteza na wanaume watapoteza na jamii itakua mfu.
Hii harakati tuianzishe na kuisimamia,wanaume tusiwe mabolizozo
 
Watoto wa kiume kutwa kukatikakatika mauno
Wanacheza singeli sjui amapiano
Watoto wa kiume wanavaa vipuli
Puani mguuni vikuku 😄
Lazima waliweee sana

Ova
Ndio tuamke mzee,mtoto wa kiume awe na heshma yake
 
tulichochelewa kujua ni kwamba kwenye haya mambo ya haki sawa lengo ni ndoa za jinsia moja tu hakuna lingine....... na wanajua afrika tukipokea jambo lazima tuharibikiwe ndio haya ya sasa kusagana ushoga na mengineyo...

jamii ikishaharibika kuanzia ngazi ya familia wazungu wanajichotea mali kwakua hakuna mwenye utashi wa kuongoza
 
Mkuu 92,

Kwa mujibu wa takwimu za “Tanzania in figures” un- natural offense Tatizo la ushoga si Tatizo la taifa wala tatizo la ngazi ya mkoa au wilaya.

“Jamii ikishaharibika kuanzia ngazi ya familia wazungu wanajichotea mali kwakua hakuna mwenye utashi wa kuongoza”

Mkuu 92,

Suala la wazungu kuja kuchota mali hatuwezi lihusisha na matendo ya ushoga au ulawiti au usagaji. sababu ya takwimu hizo hapo.

Sasa wakati kama huu yapo mambo ya viongozi wabadhilifu na wasio timiza wajibu, je nao ni sababu ya ushoga?

Kuna wakati kama taifa tunabidi kukubali kwamba tuna viongozi ambao wapo kwa ajili ya kutanguliza masilahi yao mbele kwa asilimia kubwa kabla ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.

mbunge msambatavangu hakusema kwamba pasiwe na usawa, ila katika kasi hii ya kumnyanyua mtoto wakike tusisahau nafasi ya mwanaume kama kiongozi na mwanamke kama msaidizi bila ya kuwapa athari kwa upande wowote.
 
Attachments

  • 5E61330B-6E49-46EE-B459-6F0462191DDB.jpeg
    5E61330B-6E49-46EE-B459-6F0462191DDB.jpeg
    54.3 KB · Views: 3
Wote wenye watoto wa kiume, wote wanaotarajia watoto, wote wenye ndugu, jamaa na marafiki wa kiume. Kwahiyo ni sote.

Jamii inafaa nini katika kumkandamiza mmoja?
 
Back
Top Bottom