Wangapi watamuunga mkono Joseph Selasini kujitoa bunge la Katiba?

Wangapi watamuunga mkono Joseph Selasini kujitoa bunge la Katiba?

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Baada ya kutangaza kujitoa endapo leo jioni Ccm watapitisha kura ya wazi, tunatarajia wabunge wenzake wa upinzani kumuunga mkono. Swali ni je CUF, NCCR na wabunge wakuteuliwa hasa wake 201 watafuata? wataziacha zile laki 3 kwa siku?

Yeye msimamo wake uko wazi kwamba ukishaona kura ya wazi imepita hakuna tena katiba ya wananachi bali katiba ya CCM. Tunatarajia wabunge wengi ukiondoa akina Kingunge na Makonda watamuunga mkono.
 
Uwepo wa James Mapalala kwenye hili bunge unampatia heshima kubwa tofauti na kama angeliogopa kwenda gerezani nyakati zile kwa kupigania (sio CUF tu bali) mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Mimi naungana na Mh. Selasini kwa maana endapo hilo litapita basi huenda tukawa na mchakato mwingine wa kutengeneza katiba katika kipindi kisichofikia hata miaka saba kutoka sasa sababu ya ufeki wa itakayopita. Wakati huo yeye ndiye atakuwa shujaa kwa kusimama upande sahihi sasa. Hizo 300,000/- hazilingani na heshima waliyopewa hawa wajumbe japo sawa na njaa ipo.
 
Back
Top Bottom