Wankyo Nyigesa, RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Wankyo Nyigesa, RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi

Leo imefanyika hafla ya kumuaga aliyekuwa RPC mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa na kumkaribisha RPC Mpya wa Pwani Pius Lutumo. Wankyo Nyigesa sasa ni RPC wa mkoa wa Kagera ambae amesema anajiandaa kuwa IGP na anaamini maombi yake Amiri Jeshi mkuu ameyasikia. Amedai alijiandaa kuwa DCI na kamishna Zanzibar nafasi ambazo zimeshachukuliwa

Kuhusu IGP aliyepo sasa amesema anaamini anafanya kazi vizuri ila yeye atafanya kazi nzuri zaidi. Wankyo amemuomba Mungu akamuonyeshe Rais Samia na atakuwa amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

Binafsi naliona picha la kutisha Jeshi la Polisi, subordinate huwezi kutoka hadharani na kudai cheo cha bosi wako tena katika sehemu inayohitaji nidhamu kwenye chain of command kama polisi kisha unabaki na matarajio mtendelea kufanya kazi vizuri, otherwise awe ameshapangwa na bosi wa bosi wake.

======

RPC Wankyo Nyigesa: Nilikuwa najiandaa kuwa DCI lakini nafasi ya DCI ikachukuliwa, nikajiandaa kuwa Kamishna wa Zanzibar wakachukua, sasa hivi najiandaa kuwa IGP, na ninaamini Rais Samia maombi yangu anayasikia, siku moja tafadhali niteua kuwa IGP, Mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama Mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo?,"

"Binadamu lazima uangalie mbele, natamani kuwa IGP, najua IGP aliyopo (Sirro) hajafanya makosa anafanya mazuri lakini Mimi nitafanya mazuri zaidi, matarajio yangu ni hayo, unajua Binadamu lazima uwe na malengo target ya mbele, uwe na ndoto kubwa, huwezi tu kuwa una malengo ya kwamba nitaendeela tu kuwa RPC Mimi nataka kuwa nafasi za Juu, IGP ili nifanye makubwa kwa faida ya Watanzania wengi kuliko Watanzania wa Mkoa mmoja"

"Mimi naamini siku Rais akiniota vizuri anaweza kunipa U-IGP na matamanio yangu ni kuwa IGP, na naendelea kumuomba tu Rais Samia akiona nafaa na akaomba kwa Mungu akamuonesha Mimi sio kwamba atakuwa amekosea yupo sahihi tu, amepata Mtu sahihi kwa wakati sahihi.

View attachment 2166233
 

Attachments

  • insta_23_20211203_005533.mp4
    537.3 KB
Wewe unaamini hizo porojo za miaka mitatu au kua na vision.Ata hivyo Uzoefu wakiafrika unaonyesha watu wanaojipigia debe mara nyingi wakipata hiyo nafasi wanakuaga wabovu kupindukia.Mimi naamini kwenye uwezo wa mtu.ukiwa na uwezo au mawazo makubwa utaonekana tu.maana unatakiwa uanze kuonyesha uwezo na mawazo yako kuanzia pale ulipo.Kisha uwezo wako ndio ukupandishe sio kujipigia debe.
Muache mzee akaoneshe uwezo wake anajiamini.
 
Anayo kadi ya chama? Amelipia ada zote? Yule kama marehemu kada mtiifu wa CCM afande Jonathan Shana nae aliutaka sana uIGP ila ndo hivyo tena mwendo aliumaliza
 
Sio kosa kusema ndoto zake, kama ingekuwa ni kosa asingesema katumia haki yake ya kikatiba kutangaza malengo yake, kila la kheri kamanda
 
Mama alidhani Jeshi la Magereza ndio wanahujumiana kumbe na Polisi nao wamo!
 
Wameamua kumchanganya hangaya ili asimshughulikie boss wao anayeonekana kupwaya. Janja janja za kitoto.
 
Salam tosha kwa Siro,maana yake amekumbushwa tena kua ajiuzulu na ile nafasi alipewa na marehemu pasi kustahili!!!

Siro haoni tu maneno ya hadi mkulu,"geshi lijitafakari,geshi tendeni haki"
 
Mama siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama Mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo?,"

Huyu kazua jambo
 
No matter alikuwa anatania au alikuwa siriazi ,huyu bwana maadili!!
 
Kasema vizuri.

Kuna ubaya gani kuwa na ndoto kubwa?

Akwa mfano mimi nikisema siku moja nataka kuwa mkurugenzi wa taasisi nayofanya kazi kuna ubaya gani?

Watu mnataka kumfitinisha Wankyo na Sirro.

Nampongeza Wankyo kuwa na mawazo makubwa na ndoto kubwa ila nimhakikishie hapo alipofika panamtosha.
Kijeshi si kiraia
 
Inaelekea kwenye hilo jeshi kuna wengi wasiompenda. Huyu aliyetamka hadharani naamini amefanya hivyo kuwaonyesha wananchi kwamba sio wananchi tu wanaomlalamikia Sirro bali hata askari ndani ya jeshi lake lenyewe. Kulingana na mwongozo wa jeshi mwanajeshi yeyote anatakiwa atii amri ya mkuu wake. Kwa hiyo, kusema yeye anaweza kazi kuliko Sirro ni kama kusema akimpa amri hataitii.

Kwa hiyo, huyu lazima atastaafishwa au "kurudishwa makao makuu akapangiwe kazi nyingine" (Na hiyo ni ya kusoma magazeti)
 
Back
Top Bottom