Wanu Hafidh Ameir achangia Milioni 10 Ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Rufiji

Hongera sana kwake.Mwenye mawasiliano yake please naomba,nami nina shida pengine anaweza nisaidia
Nina namba za wabunge wote wa majimbo na viti maalumu walioingia Bungeni baada ya uchaguzi wa 2015 na baada ya uchaguzi wa 2020 yaani walioingia madarakani magufuli akiwa Rais. Walioingia Bungeni baada ya kifo Cha magufuli sina. Kama upo siriasi ni pm nikupe namba . VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.
 
Wachangie vyumba vya madarasa kwa watoto huko kusini kwetu madarasa kama Jehanamu fulani vile...ingawaje huwezi kumpangia mzala matumizi..
 
Hao ndio wanakula mema ya nchi na sio mpuuzi Lucas mwashambya ambae saivi katega boda yake uyole huku anasikitika jinsi alivyokosa nafasi ya uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura
Na baridi ya Mbeya/Songwe saa hizi atakuwa anachoma viazi vitamu kwenye majivu ale apate joto mwilini. Akitoka hapo,uso umepauka kama msukule kwa kurukiwa na majivu ya mafiga.
 
MHE. WANU HAFIDH AMEIR ACHANGIA MILIONI 10 YA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU UWT WILAYA YA RUFIJI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Unguja Kusini tarehe 30 Julai, 2024 alifungua Baraza la UWT Wilaya ya Rufiji na kuchangia Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kutatua changamoto zao ikiwemo kumalizia ujenzi wa nyumba ya Mtumishi UWT, kuendeleza miradi yao pamoja na kununua simu za kusajilia wanachama kielektroniki.

Mbunge Wanu Hafidh Ameir amewaomba Wazazi hasa Wanawake kulinda Watoto dhidi ya vitendo vya kikatili kwa watoto lakini pia Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura; Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi bora; Kugombea nafasi mbalimbali.

Aidha, UWT Wilaya ya Rufiji wamemvisha rasmi Mbunge Wanu Hafidh Ameir vazi la asili ya Rufiji maarufu kama vazi la Bibi Titi wakati alipofika akiwa ni Mgeni rasmi kwenye Baraza la UWT Wilaya ya Rufiji katika ukumbi wa FDC Rufiji.

Zoezi la kumvisha vazi rasmi la Biti Titi limefanyika kwa Uongozi wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Rufiji, Rehema Mlawa na Katibu wa UWT Wilaya ya Rufiji Mariam Mugasha kwa niaba ya akinamama wa wilaya hiyo.

Mshahara wake kwa mwezi ni bei gani[emoji15][emoji15]
Enzi zile hawakuwahi kuchangia hata daftari moja.
 
Nina namba za wabunge wote wa majimbo na viti maalumu walioingia Bungeni baada ya uchaguzi wa 2015 na baada ya uchaguzi wa 2020 yaani walioingia madarakani magufuli akiwa Rais. Walioingia Bungeni baada ya kifo Cha magufuli sina. Kama upo siriasi ni pm nikupe namba . VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.
Asante sn mkuu kwa maelekezo yako na kujali kwako. Suala ni yupi atanisaidia?
Nina namba za wabunge wote wa majimbo na viti maalumu walioingia Bungeni baada ya uchaguzi wa 2015 na baada ya uchaguzi wa 2020 yaani walioingia madarakani magufuli akiwa Rais. Walioingia Bungeni baada ya kifo Cha magufuli sina. Kama upo siriasi ni pm nikupe namba . VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.
 
Hapana, anauza vitenge kariakoo namuonaga pale mtaa wa Congo ana meza yake, hana makuu binti wa watu,na wala watu wengi hawamjui pale,mimi na mke tu ndiyo tunamjua!!
Nyie ni wale wale, huyu ni mbunge viti maalum kutoka Zanzibar lakini kaolewa na Mchengerwa Pwani, upo hapo?
 
MHE. WANU HAFIDH AMEIR ACHANGIA MILIONI 10 YA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU UWT WILAYA YA RUFIJI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Unguja Kusini tarehe 30 Julai, 2024 alifungua Baraza la UWT Wilaya ya Rufiji na kuchangia Shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kutatua changamoto zao ikiwemo kumalizia ujenzi wa nyumba ya Mtumishi UWT, kuendeleza miradi yao pamoja na kununua simu za kusajilia wanachama kielektroniki.

Mbunge Wanu Hafidh Ameir amewaomba Wazazi hasa Wanawake kulinda Watoto dhidi ya vitendo vya kikatili kwa watoto lakini pia Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura; Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi bora; Kugombea nafasi mbalimbali.

Aidha, UWT Wilaya ya Rufiji wamemvisha rasmi Mbunge Wanu Hafidh Ameir vazi la asili ya Rufiji maarufu kama vazi la Bibi Titi wakati alipofika akiwa ni Mgeni rasmi kwenye Baraza la UWT Wilaya ya Rufiji katika ukumbi wa FDC Rufiji.

Zoezi la kumvisha vazi rasmi la Biti Titi limefanyika kwa Uongozi wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Rufiji, Rehema Mlawa na Katibu wa UWT Wilaya ya Rufiji Mariam Mugasha kwa niaba ya akinamama wa wilaya hiyo.
Dada ameolea na mbunge WA Jimbo la rufiji.
 
Back
Top Bottom