Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
"Serikali kupitia Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ilifanya utafiti na kubaini kuwa sababu za wanafunzi kuandika lugha zisizo na staha kwenye karatasi za mitihani ni mmonyoko wa maadili, msongo wa mawazo, na kukata tamaa kitaaluma."
"Matahiniwa anayeandika matusi kwenye karatasi ya jibu hupewa adhabu ya kufutiwa matokeo ya mtihani husika. Baraza limekuwa likiziandikia shule ambazo zimebainika kuwa na watahiniwa wa namna hii ili kuwasa wanafunzi wao."
"Utafiti huo ulibaini kuwa vitendo hivi havihusiani na jinsia moja tu; jinsia zote mbili (wavulana na wasichana) huwa wanaandika lugha zisizo na staha katika mitihani yao."
"Serikali inatambua kuwa kuna maeneo ambayo baadhi ya wazazi huwashawishi wanafunzi (hasa wa kike) kufanya vibaya au kuandika lugha isiyofaa ili wafeli, kwa lengo la kuwatoa kwenye mfumo wa elimu na kuwaozesha."
"Serikali imeunda kikosi kazi maalum cha kitaifa kinachopita kila mkoa kuangalia chanzo cha tatizo hili. Pia inaendelea kuimarisha utoaji wa ushauri na nasaha (guidance and counseling) shuleni ili kupunguza msongo wa mawazo kwa wanafunzi."