Sultan MackJoe Khalifa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2022
- 6,782
- 14,148
hatimae limesanuka😂😅🙏Vp, BADO umekomaza shingo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hatimae limesanuka😂😅🙏Vp, BADO umekomaza shingo?
Njaa inaanza mwezi huu, Bei za vyakula zitapanda maradufu zaidi ya 2022.Kila mara wananchi tulipohoji kuruhusiwa Kwa wafanyabiashara Kutoka nje ya nchi kuingia nchini kununua mazao ya vyakula mashambani kwa pesa za kitanzania, tulijibiwa kuwa " Tusimpangie MKULIMA wapi auze mazao yake".
Pesa za Umma zimetumika kuagiza mbolea na pembejeo za KILIMO nje ya nchi Kwa Dollars, iweje wafanyabiashara Kutoka nje ya nchi waruhusiwe kununua nafaka mashambani kwa pesa za madafu?
Pesa ya wananchi imetumika kuweka RUZUKU kwenye Bei ya mbolea Ili MKULIMA anunue Kwa Bei himilivu, iweje wafanyabiashara Kutoka nje waruhusiwe kwenda mashambani kununua mazao Badala ya kununua masokoni?
Tukilea mtindo huo kuzoeleka, KARIAKOO itakosa wanunuzi Kutoka nje ya nchi maana watakimbilia mashambani kumpiga MKULIMA.
Makampuni Kutoka nje yataingia mashambani kununua maembe, machungwa, parachichi nk nk, masoko yetu yatafanya KAZI Gani kama mnyororo huo utafupishwa kiasi hicho?
Kwanini Serikali itumie tena hazina ya pesa za kigeni kuagiza Mchele na vyakula nje ya nchi wakati ingeweza kuyanunua mazao hayo muda huu na yakatunzwa katika maghala yaliyoko katika mikoa mbalimbali nchini?
Jukumu mojawapo muhimu la wizara unayosimamia ni kuhakikisha MKULIMA ananufaika na JASHO lake, lakini pia wizara inawajibika kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa Bei holela.
USHAURI.
1. Wanunuzi wa mazao ya vyakula Kutoka nje waelekezwe kununua mazao kwenye maghala ya Serikali au kwenye masoko makubwa ya mikoa na wilaya na waje na Dollars, maana hivi sasa Nchi yetu Ina uhaba wa pesa za kigeni.
2. Vikundi vya wakulima viwezeshwe mikopo Ili vifanye package ya bidhaa zao Ili wauze nje ya nchi Kwa pesa za kigeni.
3. Maghala ya Serikali yafunguliwe katika miezi ya September Hadi February Ili kusaidia wakulima na wananchi kununua vyakula Kwa Bei nafuu kipindi ambacho wanasubiri kukomaa Kwa mazao Yao.
Kwa kufanya hivyo, Serikali itaweza kudhibiti mfumuko wa Bei maana itajua Kwa HAKIKA demand ya soko la ndani ni kiasi Gani hivyo kuuza ziada nje bila kuathiri Bei katika masoko ndani ya nchi.
ANGALIZO;Lipo TISHIO la njaa litakaloikabiri Dunia miaka michache ijayo hivyo, Nchi inatakiwa kuhakikisha inaweka akiba ya CHAKULA itakayodumu angalau Kwa miaka mitatu Ili kuhakikisha utulivu unakuwapo nchini endapo tutapitia kipindi hicho kigumu.
Mungu ibariki TANZANIA.
Amen.
Bashiru si aliwaambia njaa siku zote ,hudhalilisha taifa ..rais akakaza fuvu kiko wapiWaziri BASHE ungejiuzulu Ili kumpisha mwingine aje na Utaratibu mzuri wa kusimamia WANUNUZI Kutoka nje maana mwanzo uliruhusu waingie Hadi mashambani kuvuruga demand and supply chain.
Inakuja njaa Kali sana kuanzia mwezi huu na kuendelea,Bashiru si aliwaambia njaa siku zote ,hudhalilisha taifa ..rais akakaza fuvu kiko wapi
Wazo zuri. Kama tunaexport chakula basi kinunuliwe kwa dola.
Kwani ni lazima tuexport raw materials?Ndugu ili pesa Yako iwe na dhamani usiruhusu nchini kwako matumizi ya pesa za kigeni wageni waje na pesa zao lakini wakitaka kufanya malipo wanunuwe kwanza pesa zetu au walipe Kodi kwa pesa zetu na sisi TU export raw materials nje hapo ndipo pesa yako na uchumi wako unakuwa na kikubwa zaidi kinachokuza ni kupunguza Kodi wawekezaji wataweka mitaji mikubwa kwetu
Ndiyo, wanatakiwa kuja na dola. Hapa wapewe madafu ndiyo wayatumie kununulia bidhaa. Hatutaki Ksh. Wakishindwa waje na EuroNdugu ili pesa Yako iwe na dhamani usiruhusu nchini kwako matumizi ya pesa za kigeni wageni waje na pesa zao lakini wakitaka kufanya malipo wanunuwe kwanza pesa zetu au walipe Kodi kwa pesa zetu na sisi TU export raw materials nje hapo ndipo pesa yako na uchumi wako unakuwa na kikubwa zaidi kinachokuza ni kupunguza Kodi wawekezaji wataweka mitaji mikubwa kwetu
Kwani ni lazima tuexport raw materials?
Huko masokoni tunao uwezo wa kukoboa Mahindi ,Mchele nk nk na kupack mazao ya wakulima na kuexport nje ya nchi kupata pesa za kigeni kupitia viwanda vidogo vidogo.
Si sawa wageni kuingia mashambani kuwapiga wakulima.
Wakulima wetu wajengewe uwez
Stuka,Yaani mnafikiri eti ni nyie tu Mnao mazao / nafaka ya biashara ulimwengu huu wooote eeh?
😆😆,Haiya chungeni msije kuwatafuta wanunuzi wa nafaka na mazao yenyu Kwa kutumia kirunzi mvunguni.
Kama tu Russia anavyohaha kutoa nafaka na mafuta Kwa bei ya Chee pamoja na kugharamikia usafirishwaji juu yake .
Punguaniz detected!😆
Mie siyo mtz bana ,pole 😆naitetea nchi yangu.S
Stuka,
Main aim ni Nchi inunue chakula Kutoka wakulima Kwa Bei nzuri,
Chakula kitunzwe ghalani , Nchi ijitosheleze Kwa chakula maana njaa Kali Iko mlangoni inabisha HODI!!!
.
- Je hao wafanyabiashara wanakuja na Tsh toka watokako?
- Kama hujui mambo uliza jombaa
Sasa kama mnapanga maandamano muda wa kwenda shambani mnategemea nini?M
Mie siyo mtz bana ,pole 😆naitetea nchi yangu.
Muambaa ngoma huivutia kwake.
Kelb wahed.