Wanyonge waanza kumiliki barabara

Ni sehemu ya script ya mama katika movie yake ya Hollywood inayohusu utalii.
Hata 'wanyonge' ni kivutio cha utalii.

Ila hapo kwenye kuonyesha sura za watu umekosea mkuu. Kuna watu wameaga kwa wake zao wapo mkoa kikazi halafu unawaanika wanachanja mbuga kariakoo.
 
Kilichofanywa na Manispaa ya Morogoro kwenye Soko la Chief Kinga'allu ni chakushutumiwa na kina leta picha mbaya kwa kutumia majina ya viongozi wa nchi kuhalalisha matumizi mabovu ya soko tofauti na utaratibu uliowekwa katika 'design' ya soko hilo. Manispaa wamebadili matumizi ya soko na kuvuruga kabisa taswira nzuri ya Soko.

Viongozi wa manispaa waonywe. Nasubiri Institute Engineers Tanzania tawi la Morogoro watoe tamko.
 
Panakera sana pale,parking imekuwa shida sasa.
 
Serikali ya CCM haina long-term solution, unategemea nini? Wakiambiwa kilimo ni uti wa mgongo wa kumkomboa mnyonge hawataki. Wanyonge wamekimbilia umachinga maana kilimo hakijawa na tija Tz.
 
Hili ni bomu na itakuwa ngumu kulizuia lisilipuke.Kuwatoa itakuwa shida na kuwaacha ni shida vilivile.Tusubiri mtifuano.
 
Sasa tunaushi kiunafiki unafiki.Eti mtaa wa mama samia mtaa wenyewe wa vubanda vya mbao kweli?
Morogoro wajitafakari.
Parking zinalipa kuliko hata hao wanaotaka kuwaweka,watachafua na watasema hawapati faida na kugomea kodi ya pango tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…