Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja

Hitaji kubwa la Muungano tulishalivuka, nalo lilikua enzi zile tubapata uhuru kama Zenj ingeachwa peke yake ingetusumbua sana kiusalama kwa sasa dunia na milengo yake ishabadilika so wanaweza kuamua wakitaka

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Muungano huu kila upande unadai kuonewa na mwingine. Cha muhimu ni kuvumiliana tu.
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Hata hili la DPW, sasa linaleta kelele za Utanganyika na Uzanzibari, kelele hizi zinachosha!.

Mtu kama huyu, anawezaje kutoa kauli za kidedhuli kama hizi ? Nashauri kelele kama hizi za kihayawani, zisijibizwe kihayawani, zinyamazishwe kwa solid facts na sio denial.
P
 

Wosia Wa Baba Wa Taifa Kuhusu Muungano Na Utawala Bora.​



Wosia wa Baba wa Taifa​



USIA WA BABA WA TAIFA MWL. JK NYERERE KIONGOZI USILETE UDINI NA UKABILA UTAWAGAWA WA TANZANIA​



MWL. J.K. NYERERE: HOJA JUU YA TANZANIA NA MUUNGANO​


 
wazanzibari wana haki ya kulalamika na wana malalamiko ya halali kabisa
 
Hakuna mzanzibar anayetaka Muungano ila Mabazazi ya DANGANYIKA ndiyo wanaung'ang'ania kwa maslahi binafsi yao.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Naunga mkono hoja, kuhusu kuitishwa kwa kura ya maoni, watuwaulizwe, ila sii kweli muungano haukupata ridhaa ya wananchi, Tanganyika tuliridhia, Zanzibar ndio haikuridhia, ila mwanzo ilibiruzwa kisha ikaridhia!.

Muungano ni kama ndoa, Mwanamke kama hakutaki, mwache!. Usimbake!. Muungano wa bila upande mmoja kuridhia ni sawa na ubakaji. Ila aliyebakwa, ameendelea kuishi na mbakaji, akitoa huduma zote, hivyo anahesabika ni kuridhia by performance.

Japo Zanzibar haiku ratified muungano, lakini imetekeleza muungano, hivyo ni imeridhia impliedly. Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

Tanzania hatuna sheria ya kura ya maoni, Zanzibar mnayo, pigeni!. Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
P.
 
Kiukweli Wazanzibari ni shidaah!. Baada ya Mkutano Mkuu kupitisha jina la Mwinyi, bila CCM Zanzibar, Wazanzibari wamekiwasha hapa Dodoma kupangiwa rais wa Zanzibar Dodoma!. Vikao vya kuwapooza vimeanza!. Dawa ya kudumu ni serikali moja!, vinginevyo hawa Wazanzibari, watatusumbua sana!.
Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Duh...!. Kwa uamuzi huu, ina maana HII sauti nilioisikia sio sauti yake YEYE bali ni sauti ya yeye!.

Angalizo: Kama sauti HII
ni yake YEYE mwenyewe halisi na mhusika ameambiwa ila akatia pamba masikioni, kujifanya hajasikia, then kati ya 2025 na 2030, YEYE mwenyewe atasema nasi!.
Kazi iendelee!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…