Wapalestina 36 wauawa katika mashambulio ya roketi ya Israel

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Mamlaka katika eneo la Gaza zimesema takriban Wapalestina 36, wakiwamo watoto 10 wamefariki kutokana na mashambulio ya maroketi kutoka Israel, huku wengine 250 wakijeruhiwa siku ya Jumatano.

Mashambulizi haya ni ya hivi karibuni zaidi yanayoongeza mvutano ulioanza baada ya Hamas kuvitaka vikosi vya Israel kuondoka katika eneo la msikiti wa Al-Aqsa, Mashariki mwa Jerusalem uliokuwa umevamiwa na vikosi vya Israel vilivyowashambulia waumini katika msikiti huo kwa kutumia risasi za mpira.

Mamlaka za Israel zimeripoti kuwa kombora lililorushwa kutoka upande wa Gaza limeanguka katika bomba la mafuta na kusababisha moto mkubwa. Kundi la Wapiganaji wa Kipalestina la Hamas limeapa kuendeleza mashambulizi yake dhidi ya Israel kulipiza kisasi cha vikosi vya Israel kushambulia msikiti wa Al Aqsa.

Wakazi wa maeneo ya Gaza wamelazimika kuondoka mapema asubuhi kukimbia athari za makombora hayo huku kukiwa na ripoti za Israel kusogeza vifaa vya kijeshi vikiwamo vifaru karibu na eneo la Gaza, ikiashiria kuwa mapigano zaidi yanatarajiwa kutokea katika siku za usoni.

1620802008666.png

Vikosi vya Israel vimejitapa kuwa makombora ya ndege zake za kivita yamefanikiwa kuwaua viongozi muhimu wa upelelezi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, akiwamo Hassan Kaogi, Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Hamas na naibu wake. Hamas haijatoa ripoti kuthibitisha madai ya Israel.

Wanaharakati wamemwomba Rais wa Marekani, Joe Biden kuingilia mzozo huo na kuiwajibisha Israel kwa kushambulia makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza kwa maroketi. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa Amani ya nchi za Mashariki ya Kati amechapisha, taarifa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akionya kuwa hali ya mambo inaweza kubadilika ghafla na kuwa vita kamili ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa. Hata hivyo, Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa Marekani inachelewesha kauli ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa mapigano hayo. Baraza hilo linatarajiwa kukutana baadaye hii leo.

Chanzo: Al Jazeera
 
Sam Gidori
Wapalestina wanatumiwa ili wengine wapate pesa, Kama wangekua na maamuzi Yao wenyewe wangemalizana na Israel wakae kwa Amani
 
Sidhani kama Israel huwa inapenda kufanya haya!

Lakini hawa Wapalestina a.k.a wavaa vipedo usipoongea kwa lugha ya kueleweka kama hiyo anayoitumia Israel, watakutia vidole.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Sidhani kama Israel huwa inapenda kufanya haya!

Lakini hawa Wapalestina a.k.a wavaa vipedo usipoongea kwa lugha ya kueleweka kama hiyo anayoitumia Israel, watakutia vidole.
Mkuu unajua ni sababu ipi iliyo sababisha haya mapigano ?au hisia za kidini zimekutawala?
 
Toa kibanzi cha upumbafu kichwani mwako, uione dunia.
 
Akir
Sidhani kama Israel huwa inapenda kufanya haya!

Lakini hawa Wapalestina a.k.a wavaa vipedo usipoongea kwa lugha ya kueleweka kama hiyo anayoitumia Israel, watakutia vidole.
Huna wew
 
Natanyahu yupo tayari kumaliza wapalestina wote ilimradi abaki madarakani. Hatari sana.
 
Stay in power at the expenses of human lives. Natanyahu,, go go go!
 
Sidhani kama Israel huwa inapenda kufanya haya!

Lakini hawa Wapalestina a.k.a wavaa vipedo usipoongea kwa lugha ya kueleweka kama hiyo anayoitumia Israel, watakutia vidole.
[emoji16][emoji16]
 
Mkuu unajua ni sababu ipi iliyo sababisha haya mapigano ?au hisia za kidini zimekutawala?
Itakuwa ni udini. Ukweli ni kwamba Netanyahu anajuwa njia pekee ya kuendelea kubaki ni kuzusha vita. So anataka abaki kwa gharama ya filistines!
 
Mamlaka katika eneo la Gaza zimesema takriban Wapalestina 36, wakiwamo watoto 10 wamefariki kutokana na mashambulio ya maroketi kutoka Israel, huku wengine 250 wakijeruhiwa siku ya Jumatano.

Mashambulizi haya ni ya hivi karibuni zaidi yanayoongeza mvutano ulioanza baada ya Hamas kuvitaka vikosi vya Israel kuondoka katika eneo la msikiti wa Al-Aqsa, Mashariki mwa Jerusalem uliokuwa umevamiwa na vikosi vya Israel vilivyowashambulia waumini katika msikiti huo kwa kutumia risasi za mpira.

Mamlaka za Israel zimeripoti kuwa kombora lililorushwa kutoka upande wa Gaza limeanguka katika bomba la mafuta na kusababisha moto mkubwa. Kundi la Wapiganaji wa Kipalestina la Hamas limeapa kuendeleza mashambulizi yake dhidi ya Israel kulipiza kisasi cha vikosi vya Israel kushambulia msikiti wa Al Aqsa.

Wakazi wa maeneo ya Gaza wamelazimika kuondoka mapema asubuhi kukimbia athari za makombora hayo huku kukiwa na ripoti za Israel kusogeza vifaa vya kijeshi vikiwamo vifaru karibu na eneo la Gaza, ikiashiria kuwa mapigano zaidi yanatarajiwa kutokea katika siku za usoni.

View attachment 1781703

Vikosi vya Israel vimejitapa kuwa makombora ya ndege zake za kivita yamefanikiwa kuwaua viongozi muhimu wa upelelezi wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, akiwamo Hassan Kaogi, Mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Hamas na naibu wake. Hamas haijatoa ripoti kuthibitisha madai ya Israel.

Wanaharakati wamemwomba Rais wa Marekani, Joe Biden kuingilia mzozo huo na kuiwajibisha Israel kwa kushambulia makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza kwa maroketi. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa Amani ya nchi za Mashariki ya Kati amechapisha, taarifa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akionya kuwa hali ya mambo inaweza kubadilika ghafla na kuwa vita kamili ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa. Hata hivyo, Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa Marekani inachelewesha kauli ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa mapigano hayo. Baraza hilo linatarajiwa kukutana baadaye hii leo.

Chanzo: Al Jazeera

If you are living in a glass house dont throw stones. Kuna watu wanauwawa kama wanyama huko jimbo la Tigray Ethiopia na Myanmar dunia imekaa kimya kama vile wao siyo binadamu.
 
Back
Top Bottom