Wapalestina ni wavamizi kwa mujibu wa Quran

Wapi kwenye biblia imeandikwa hiyo ardhi ya tanganyika ukae wewe
 
Fungua Quran sura ya 17 kuanzia aya ya 4-8 usome habari za mayahudi na nini kilichowatokea na maisha wanayopitia sasa na nini kitakwenda kuwakumba mwishoni.
 
Upuuzi mtupu. Hata hiyo biblia manyang'au kama Netanyahu na Tramp wanayotumia iliwakuta pale. Acheni kujiridhisha na kujifurahisha. Hawaendi popote.
 
Qur’an Inakiri kuwa Wana wa Israel Waliandikiwa Ardhi

Katika Surat Al-Ma'idah (5:21), Nabii Musa anawaambia Wana wa Israel:

يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ

"Enyi watu wangu! Ingieni katika ardhi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni..."

Neno "كَتَبَ اللَّهُ لَكُمْ" (ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni) linaweza kufasiriwa kama haki ya milele ya Wana wa Israel juu ya ardhi hiyo, kwani Qur’an haitaji kuwa haki hiyo iliondolewa.
 
Katika Uislam hao wapalestina wanatambulika kuwa ni Waislam. Waislam wote regardless ni wa kutokea ardhi gani tuna haki ya ardhi ya Palestine kwasababu ni ardhi iliyokuwa chini ya dola ya Kiislam toka wakati wa Khalifa Umar ibn khattab.

Waislam wameishi katika ardhi ya palestine kwa zaidi ya miaka 1300 mpk pale Muingereza na mmarekani walipokuja kupandikiza mayahudi katika ardhi hiyo
 
endelea aya iliyofuata...baada ya mussa kuwaambia waingie katika ardhi hiyo mayahudi walimjibu nini Musa? Usikopi aya nusu nusu
 
Qur’an Haijasema Waisraeli Waliondolewa Milele

Katika Surat Al-Isra (17:4-7), Qur’an inasema kuwa Wana wa Israel walifanya ufisadi na wakashindwa:

بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ

"Tuliwaelekezea waja wetu wenye nguvu kali..."

Aya hii haijasema kuwa walinyang’anywa ardhi milele, bali walipata adhabu ya muda kwa sababu ya uovu wao.
 
Kwahiyo wale WAPALESTINA ndio nyie?

Manabii wote ni wayahudi na wamezaliwa maeneo hayo na kukulia na kuzikwa hapo

Unalijua hilo?
 
Fungua Quran sura ya 17 kuanzia aya ya 4-8 usome habari za mayahudi na nini kilichowatokea na maisha wanayopitia sasa na nini kitakwenda kuwakumba mwishoni.
Ukitaka historia ya wayahudi na utabiri wao Hadi ulivyotokea na utakavyotokea kasome biblia ,Hadi jinsi unabii wa kurudishwa kwao 1948 ulivyotimia
 
Quran 21:105

Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.
Surat Al-Baqarah (2:47)

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذكرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ

"Enyi Wana wa Israel! Kumbukeni neema yangu ambayo niliwajalia ninyi, na kuwa mimi niliwafadhilisha juu ya walimwengu."

Hapa, Qur’an inatambua kwamba Wana wa Israel walikuwa na neema maalum kutoka kwa Mungu, na kwa hivyo wana haki ya kudai nafasi maalum katika dunia.
 
endelea aya iliyofuata...baada ya mussa kuwaambia waingie katika ardhi hiyo mayahudi walimjibu nini Musa? Usikopi aya nusu nusu
Surat Al-Isra (17:104)

وَقُلْنَا مِن بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا
"Na tukawaambia baada yake Wana wa Israel: Kaeni katika ardhi... Hata wakati wa ahadi ya mwisho, tutawafikisha nyinyi."

Aya hii inaonyesha kwamba Wana wa Israel walikumbushwa na Mungu kuishi katika ardhi hiyo, na inatoa ahadi ya kuwa wataweza kurudi baada ya kipindi cha uhamisho. Hii inadhihirisha kuwa ardhi hii inachukuliwa kama urithi wao.
 
Aya zinathibitisha kuwa Waisrael ni wavamizi , walikuta watu na maisha yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…