Mwanamfalme mwengine leo ametoa kauli kali zaidi kuipasha Israel na haijawahi kutokea.Wale wanaosema Saudia ni wanafiki leo inabidi wajiulize upya.
Huyu ni yule mwanadiplomasia na muwakilishi wa Saudi Arabia kwa miaka mingi .
Ni Turk Al Faisal kwenye kongamano lililofanyika Manama mji mkuu wa Bahrain.Waziri wa mambo ya nje wa Israel hakutarajia mashambulizi kama hayo akabaki kuduwaa na alipojaribu kujibu Turk akambamiza tena.
Alianza kwa kusema Israel inajigamba kama ni mpenda haki mkubwa kinyume na ukweli kwamba wamewafanya wapalestina waishi kama koloni lao. Wamewalazimisha wapalestina waishi kwenye maisha ya kambi za mateso kwa kisingizio cha kipuuzi kuhusu kitisho cha usalama.Wazee kwa vijana,wake kwa waume wanaozeana humo bila kujua kosa lao.Israel wanavunja majumba yao kama wapendavyo na kumuua yeyote wanayemtaka.
Mwanamfalme Turk akaendeleza mashambulizi kwa kusema Israel ina zana za nyukia ambazo haitaki kuzitangaza na huku ikitumia wanasiasa walio chini yake na mitandao yake ya kueneza habari ikiishutumu Saudia na baadhi ya misimamo yake.
Baada ya hapo akasema Saudi bado imeshikamana na maazimio ya siku za nyuma yanayotaka kuwepo kwa taifa la Palestina na Israel irudi kwenye mipaka yake kabla ya mwaka 1967.Akasema huwezi kutibu donda linalochirizika damu kwa kutumia dawa za kuuwa maumivu.
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gabi Ashkenazi alipofuatia kuzungumza akasikitishwa na matamshi ya Turk Alfaisal na kusema mashambulizi yake hayaendani na mabadiliko yanayotokea sasa hivi katika mashariki ya kati na akaendeleza lawama kwa wapalestina kwamba ndio kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya amani.Akajigamba kwamba katika hali hiyo kuna uchaguzi jee yapatikane makubaliano au tuendeleze mchezo wa kulaumiana.Naye Dore Gold mwakilishi mwengine wa Benjamin Netanyahu katika mkutano huo akasema shutuma za mwanamfalme Turk ni za kizamani na nyingi si za kweli.Kauli hiyo ikazidi kumpandisha hasira Turk na kwa kukumbushiia mahojiano ya televisheni ya zamani akasema Dore Gold anaatkiwa awe mtu wa mwisho kuzungumzia misimamo ya zamani.
Mwanamfalme Turk ameshikilia nafasi ya mkuu wa usalama wa Saudia kwa miaka mingi na kuwa balozi wa nchi hiyo Marekani na Uiengereza kwa nyakati tofauti ambaye kwa sasa hana cheo maalum.Mawazo yake yanasemekana ndiyo msimamo wa mfalme wa nchi hiyo yaliyodhidi ya mrithi wa mfalme Mohammed bin Suleiman ambaye ni mtoto wake.
”