Wapambana Rushwa wanapopewa wanaochunguzwa kuwaongoza

Wapambana Rushwa wanapopewa wanaochunguzwa kuwaongoza

Wadau

Nimeona kwa kipindi kirefu Sasa Taasisi ya TAKUKURU inapewa watu kutoka nje kuiongoza. Nina maswali kadhaa,
1. Taasisi hii ina professional discipline? Au wanajiendea endea tu? Maake inaongozwaje na Kila mtu ?
2. Internally ina succession plans? Kama wanayo hao waliotakiwa kuwa katika nafasi husika huwa wanajisikiaje?

3. Hii Taasisi inawezaje kutunza organization culture? Kama Kila muda inapewa mtu mwenye culture tofauti kuiongoza?

Mwisho kwanini wanaoteuwa wanadhani hii Taasisi inaweza kuongozwa na yeyote?

Leo nimekuwa na maswali kuliko majibu
Mbona TRA kamishna mkuu anatoka nje na mashirika au taasisi nyingi viongozi wakuu wanatoka nje ya taasisi na hatujakusikia kuongea hayo yote au sababu ni TAKUKURU mkuu.
 
Ahaahaa Kalamu 1 hakuna nilipopinga kuwa takukuru siyo taasisi nyeti au taasisi hiyo eti wamenifanyia kitu kibaya la hasha naongelea uhalisia wanayo mazuri sana wamepanga kuyafanya au wameyafanya.

Sijaongelea objectivity hata kidogo nielewe mzee nimeongelea professionalism ambapo kiuhakika Polisi wako vizuri katika hili kuliko takukuru yako na ndiyo maana wenye kuona mbali wanamshauri Rais ateue kiongozi wa juu kutoka polisi kwa mara ya tatu kama sikosei i.e. mlowola,diwani na sasa aliyeteuliwa.

Rejea utendaji kazi wa anti corruption ya polisi kipindi hicho utapata jibu hakuna chuki hapa wala ushabiki bali mapenzi mema tu.
Naungana na wewe mkuu, katika suala la upelelezi nawakubali sana polisi
 
Wadau

Nimeona kwa kipindi kirefu Sasa Taasisi ya TAKUKURU inapewa watu kutoka nje kuiongoza. Nina maswali kadhaa,
1. Taasisi hii ina professional discipline? Au wanajiendea endea tu? Maake inaongozwaje na Kila mtu ?
2. Internally ina succession plans? Kama wanayo hao waliotakiwa kuwa katika nafasi husika huwa wanajisikiaje?

3. Hii Taasisi inawezaje kutunza organization culture? Kama Kila muda inapewa mtu mwenye culture tofauti kuiongoza?

Mwisho kwanini wanaoteuwa wanadhani hii Taasisi inaweza kuongozwa na yeyote?

Leo nimekuwa na maswali kuliko majibu
Mkuu una hoja ya Msingi. Tuliosoma management tunakuelewa sana. Nadhani hapana niavya dhati ya kujenga taasisi imara. Pamekuwa na malengo ya muda mfupi Tena ya kisiasa zaidi
 
Umeuliza maswali ya msingi sana ambayo sitegemei utapata jibu sahihi hapa JF.

Sisi tutabahatisha tu kwa majibu yetu.

Kwa mfano: huenda utendaji wenu huko huko ndani una matatizo.

Mnaweza kuwa ni sehemu ya tatizo mnalolitafutia ufumbuzi?

Kwa hiyo ni muhimu kwenu kujidadisi ndani kwa ndani kuhusu maswali hayo uliyouliza hapa; huko ndiko mtakapopata jibu sahihi.

Kwa nini hamuaminiwi kwamba mnaweza kujiongoza?
Kwa maoni yangu Ni kinyume. Hii taasisi haijapewa Uhuru wa kukua yenyewe au kutambulika kuwa imekuwa. Kwa kuwa ilianzishwa mainly kutoka polisi basi imefanywa mtoto mchanga siku zote
 
Mbona TRA kamishna mkuu anatoka nje na mashirika au taasisi nyingi viongozi wakuu wanatoka nje ya taasisi na hatujakusikia kuongea hayo yote au sababu ni TAKUKURU mkuu.
Ndo Yale yale tu
 
In

Labda tuhoji sasa mfumo wao wa mafunzo hawa TAKUKURU
Mfumo wa mafunzo ubadilishwe na uwe wa kiujuzi na kinkakati katika kutokomeza rushwa na kuwe na uhuru kama ilivyo ktk nchi nyingine siyo ubabe ndani na nje ya taasisi.

Niwazi bado mafunzo yao siyo yabkimkakati kwani ni semina tu ya miezi 3 kwa mtu mwenye shahada yoyote ile iwe kilimo,uchumi,maktaba,sayansi ya jamii,n.k ambapo hujifunza partial marshal art kwaajili ya self defence na baadhi ya sheria na walimu wakiwa maboss wao au watangulizi wao na baadhi ya wakufunzi waalikwa kutoka polisi,mahakama,nk na ndito maana wanatoka nje ya majukumu yao.

Ndani ya hito course wanajifunza za pcca,cpa,tea,eoca na pc juu tu siyo kwa undani kwa hiyo miezi mitatu pasipo kujifunza masomo mengine yahusuyo RUSHWA na UCHUNGUZI.

Baada ya hapo eti watu wanakuwa wamehitimu tayari kupambana rushwa,kweli?

Haya baada ya miaka kama kumi kazini wanaenda semina ya senior ambao sasa hawa ndiyo wanachaguliwa kuwa dbcs,agrbcs,rbcs,directors,nk kwa fadhira za DG siyo kwa sababu ya elimu ya rushwa na ubobezi ktk maswala ya uchunguzi.

Haya hao watu unawaingiza mtaani na shahada zao na hiyo BIC wakachunguze na kupambana na rushwa kwa kupokea taarifa tu na siyo ujuzi.

Je huyo mtu atatenda miujiza ndani ya taasisi au nje ya taasisi katika kupambana na rushwa au utamlinganisha na polisi aliyepitia mafunzo na hatua mbalimbali ya uingozi?

Tukubali kubadilika takukuru hamna weredi na fairness zaidi ya ubabe na kuogopwa kwa fikira tu humo ndani kuna viongozi viraza kweli ambao wapo kulinda maslahi yao kwa kumpotosha kila DG ajae kwa kumlisha matango pori na kuwachongea subornates wenye vipaji pamoja na mwenda zake kuwaondoa baadhi yao na kuwapeleka taasisi nyinginezo mmoja wao akiwa aliyekuwa AgDPP.

Polisi wakisimamiwa wanaweza kabisa kutokomeza rushwa siyo kwa hii takukuru kupambana na rushwa siyo degree/master/phd, majengo,idadi kubwa ya watumishi,upendeleo na magari bali WEREDI

Viongozi wa takukuru wengi wanalipiana fedha za serikali kusomea elimu za juu vyuoni i.e pgraduate,masters,degree,phd badala ya kuwaandaa watu wa kada ya chini kwa kuwapa elimu nzuri zenye msingi ktk maswala ya kupambana na rushwa kwa kuanzia chini hadi juu.

Hivi kweli mtu mwenye shahada ya maktaba na hizo semina za bic na uandamizi anapewa mkoa au wilaya eti atokomeze rushwa bila nyongeza yoyote ya ujuzi wa uchunguzi wa maswala ya rushwa kunaweza kuleta tija?

TUTAFAKARI!!!!
 
Aanze na Kange alimla kichwa nae ale kichwa file lake la rushwa alijafungwa.
Huu utumishi uacheni hivi hivi Mdogo anaweza akawa Mkubwa and vice versa
 

Attachments

  • 2776001-93fc003c37ed19ac99cc71a6c7972313.mp4
    3 MB
Hivi ukitaja rushwa nchi hii katika vyombo vya ulinzi akili yako inkutuma JWTZ au POLICE?

We unafikiri huyo police aliyeteuliwa mpaka SASA hajawahi pokea rushwa? Au hajawahi ona rushwa ikitembea waziwazi Huku akijua na kuinyamazia Kimya!

Nilitegemea Huku kujaa thread za watu wakipinga hiyo Taasisi ya TAKUKURU kukabiziwi police ili wajitathmni zaid na said,

Binafsi ktk Maisha yangu Kwa kusikia,kuona,kushiriki Jambo lolote linalowahusisha askari iwe Kwa kukamatwa ndugu,mtaani,Barabarani matrafik n.k sijawahi sikia askari akipinga rushwa zaidi ya kutoa maelekezo rushwa zao watazipataje ama zipelekwe Kwa Nani ili isiwe direct.
Kwa Hyo sikubaliani nao hao watu kitengo hicho
 
TAKUKURU inakuwa undermined sana na kwa style hii inasababisha loyal Senior officers wapoteze guts za kufanya kazi kwa bidii
 
Hivi ukitaja rushwa nchi hii katika vyombo vya ulinzi akili yako inkutuma JWTZ au POLICE?

We unafikiri huyo police aliyeteuliwa mpaka SASA hajawahi pokea rushwa? Au hajawahi ona rushwa ikitembea waziwazi Huku akijua na kuinyamazia Kimya!

Nilitegemea Huku kujaa thread za watu wakipinga hiyo Taasisi ya TAKUKURU kukabiziwi police ili wajitathmni zaid na said,

Binafsi ktk Maisha yangu Kwa kusikia,kuona,kushiriki Jambo lolote linalowahusisha askari iwe Kwa kukamatwa ndugu,mtaani,Barabarani matrafik n.k sijawahi sikia askari akipinga rushwa zaidi ya kutoa maelekezo rushwa zao watazipataje ama zipelekwe Kwa Nani ili isiwe direct.
Kwa Hyo sikubaliani nao hao watu kitengo hicho
Nakumbuka nepotism ya takukuru ya mjeda ? Ati ikanywea kushughurikia walarushwa wanasiasa eti wakashugurikiwe na CCM kuanzia hapo nikaidharau takukuru
 
Kwa JWTZ was ok,ila Kwa police a big no
Kwa Polisi ni OK. Polisi kisheria ndio wenye dhamana ya kushughulikia (kupeleleza) jinai zote na rushwa ikiwemo. Refer kesi ya R Vs Jerry Murro ambapo upande wa utetezi uliibua hoja kuwa, kama Jerry Murro aliomba rushwa kwa nini aliyeombwa rushwa hakwenda PCCB na akaenda Polisi? Hapa utetezi ulitaka kujenga hoja kuwa, inawezekana kuna mchezo ulikuwa umechezwa na Polisi na mtoa taarifa dhidi ya Jerry. Lakini mahakama ikaeleza kuwa, Polisi haizuiwi kwa vyovyote vile kudili na jinai yoyote ile, iwe jinai hiyo ina mamlaka yake tofauti kama ilivyo rushwa au lah.

Kwa hiyo, kwa kuwa PCCB ni chombo cha kupeleleza jinai, basi Polisi ni sahihi kabisa kupewa kukiongoza chombo hicho. Kwa JWTZ haikuwa poa sana, maana wao kitaaluma sio wapelelezi kabisa.
 
Kwa maoni yangu Ni kinyume. Hii taasisi haijapewa Uhuru wa kukua yenyewe au kutambulika kuwa imekuwa. Kwa kuwa ilianzishwa mainly kutoka polisi basi imefanywa mtoto mchanga siku zote
Nadhani upo sahihi mkuu.

Rushwa na ufisadi ni tatizo kubwa mahali popote duniani, na nchi ambapo hali hii inapoachwa na kushamiri nchi hiyo haina amani hata kidogo.

Ni vyema basi, taasisi muhimu kama hii ingepewa umuhimu unaostahili ili iweze kufanya kazi yake kikamilifu kabisa.
 
Back
Top Bottom