Wapambana Rushwa wanapopewa wanaochunguzwa kuwaongoza

Nyundo2017

Kwa kweli umeliweka kwa kina jambo hili. TAKUKURU inakosa mashiko na misingi ya kitaaluma ya mapambano ya Rushwa.

Wako pia wafagia ofisi na wahudumu. Wakipata degree wanakuwa wachunguzi automatically bila taalumu nyingine.

Nakumbuka Kuna wakati walikuwa na mkakati wa kujenga chuo chao cha mafunzo. Sijui likiishia wapi wazo hili
 
bado unaishi gizani sana.

nanyinyi kwa mitazamo hii ndio mnavunja mionyo wachache walioamua kuzifanya kazi hizo kwa haki,mko negative masaa 24.
unadhani polisi hakuna walokole na swala tano wanaomuogopa Mungu??

jikiteni katika kujadili namna ya kuwaboreshea maslahi ili tuwahukumu kwa haki,huko bandarini,takukuru,tra kuna mishahara na watu wanapiga mikunjo sio kizembe,hao polisi mnawalilia kisa buku mbili mbili zà barabarani mnazowapa huku mnawasimanga!!!!
 
anajua nini huyo anahemka tu.
 
Mbunifu kwenye medani zakivita anapelekwa kwenye kupambana na rushwa ilihali kule hutumii bunduki na amri ,mtoaji ,mpokeaji wote hawa wanaakili sana,ndimana tunakuta rushwa inaendelea na ukuaji badala to decline

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Kwa rushwa zote hizo ambazo polisi wanajihusisha nazo, leo hii ndo mmoja wao anapewa mamlaka ya kusimamia taasisi ya kupambana na rushwa? ama kweli...
kama rushwa ni taasis zote zina rushwa.
ni different levels tu.
however si wote .. wapo wale wenye clean records.
 
Kwa JWTZ was ok,ila Kwa police a big no
Kwa Taarifa yako, CP Salum.Hamduni anakuwa Polisi wa Tatu kuiongoza PCCB ,alianza DCP Valentino Mlowola, Akaja CP Diwani Athumani, na Sasa CP Salum Nassor Hamduni.
Yule Brigadier wa Jeshi hakuwa anatosha kabisa pale, No wonder Most of the time akawa anavaa Sare za Jeshi, Combat kutaka ku hide Weaknesses zake
 
Kwa JWTZ was ok,ila Kwa police a big no
Sikiliza wewe police ndio wataalam unaongea ujinga tupu,police ni law enforcement agence ambayo anasimamia sheria zote za nchi kwa taarifa yako hiyo PCCB ilikuwa ndani ya police wakatenganisha ni ma nguli wa criminal investigation kwenye nyanja zote na wana power kubwa katika kuzuia na kupambana na uhalifu ikiwemo kutoa nakupokea rushwa huyo afande atafanya kazi za PCCB na inapobidi nguvu ya police anatoa maelekezo kwa maofisa wa chini sababu yeye ni COMMISIONER OF POLICE.
 
Ujinga Tu,Kwa akili zako fupi unajua Kwa nn ilitenganishwa na police?
 
Hivi police unamtemganishaje na Rushwa?
Akili zenu fupi Sana,ndo mana watu wenye IQ kubwa hawaezi weka police Kua wapambana na Rushwa zaidi ya wao wenyewe kuhitaji kupigwa msasa na kupitia mara Kwa mara na Pccb.

Rudisheni akili zenu Sawa Sawa, police Kua Pccb ni Sawa na kesi ya ngedere hakimu nyani.
Hata Huyo Diwani Athumani watu waliongea ndo akang'ofolewa .

Discipline ya jeshi dunia nzima si ya kutiliwa Shaka,hebu geukia upande wa pili wa hao police ndo utajua ufinyu WA akili yako ya kimhemuko
 
No wonder police 90% ni ngao ya watawala kujifichia maovu Yao na kuwatumia katika kuwaziba midomo wote wanaopingana na unyonyaji na wizi WA viongozi.
Suala la msingi ni police ana legacy gani ya kuchunguza rushwa Hali ya Kua wao ndo wananuka rushwa kila idara?
 
sasa rushwa ni paka,nani atamfunga kengere??

kama taasisi hamuiamini,watumishi hamuwaamini.
 
Huna akili. Hivyo tu ndivyo ninavyoweza kusema.
 
Huwezi kupambana na rushwa duniani usiwe askari au kupata mafunzo ya kijeshi na ukafanyakazi kwa tija.

Kama wanyama pori tu wanalindwa na askari sembuse binadamu mla rushwa?

Leo hii mnasema polisi wanakula rushwa ambao wamepitia mafunzo ya kijeshi halafu unawategemea takukuru ambao ni raia tu wakapambane na polisi ambao ni askari kweli?

Kupambana na rushwa ni vita na vita inataka weredi,ujasiri,mbinu,ukakamavu,nk.

Mimi napendekeza takukuru iundwe upya kwa kuchanganya askari kutoka majeshi mbalimbali na vyombo vya ulinzi na usalama wapikwe waive waganye kazi kama task force iliyo na lengo kuu siyo kurukaruka.
 
Kwanini hawasomeshi watu sasa?
 
Nilizani unataka kuuliza "Kwanini hawa wala rushwa wanaaminiwa na kupewa kazi ya kupambana na rushwa?"
 
Nilizani unataka kuuliza "Kwanini hawa wala rushwa wanaaminiwa na kupewa kazi ya kupambana na rushwa?"
Assuming iko hivo Hilo Swali. Tolea maoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…