Wapanga mipango ya ushindi, fitina, na propaganda wa CCM na upinzani ni wafanyakazi hewa

Wapanga mipango ya ushindi, fitina, na propaganda wa CCM na upinzani ni wafanyakazi hewa

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
17,119
Reaction score
32,195
Salam wakuu,
Naomba niseme CCM, CHADEMA, na ACT mnalipa wafanyakazi hewa kwenye vitengo vyenu vya ubunifu wa mikakati ya ushindi, propaganda, fitina, figisu figisu na uenezi.

Mnatabirika mno, yaani kama kuna madudu au propaganda au bao la mkono linajulikana hata na mtoto mdogo.

KUNDI LA UPINZANI:
Kuna watu wamewashauri mtumie teknolojia(mitandao ya kijamii) kueneza propaganda au mikakati yenu, lakini tatizo mna watumia watu walewale, fake ID zile zile, namna ya kukosoa au kusifia ni ile ile kwa miaka zaidi ya 4.
Kwa kawaida binadamu anachoka mazingira yale yale kwa muda mrefu, au kuzisoma na kuzisikia kauli zile zile kwa muda mrefu.
Na ndio maana watu huchepuka kutafuta mazingira, sura, tabia, kauli, na ladha mpya.
Watu hufurahia simu, mavazi, nyumba, au gari mpya.

Yaani pattern au tuite 'modus of operand' ya kufanya mikakati yenu ni ile ile, kwa vile mliambiwa mkitumia mitandao ya kijamii mnaweza kuwang'oa madarakani watawala kama ilivyotokea ktk Arab Spring au Arab Uprising basi mnafanya kienyeji sana bila ubunifu.

Kwanini kusiwe na kitengo chenye watu waliofuzu toka fani mbali mbali ukatengenezwa mfumo (ICT System kama unaotumia AI, bots kama Skype bots, chat bots. etc.) wa kutengeneza rondom message zinazo onekana kuwa very authentic za binadamu sio za bots ambazo huchambua kero mnazolalamikia na kusambaza ujumbe.

Zitumike Account(ID) tofauti sana bila kujirudia mara kwa mara kusambaza jumbe nilizotaja juu kiasi kwamba wananchi wasijue hawa ni watu walewale wachache, pungufu ya milioni moja.
Sasa ukienda JF unakuta wale wale, jumbe zile zile, ukienda twitter, Instagram, au Facebook unakuta Makada wa chama makao Makuu, wabunge, madiwani, au magavana wa kanda za kichama. Jumbe hazionekani kuanzishwa na wananchi wa chini wa kawaida ambao hawapo ktk kundi la wanufaika wa ruzuku au malipo ya nafasi za kisiasa.

Kuaminisha umma walalamikaji ni tofauti na wengi toka chini kabisa, kero zilizo lalamikiwa zitaonekana ni za wananchi wengi na kuna tatizo kubwa ktk utendaji wa walalamikiwa.

Mnajua kwanini mgomo wa uchaguzi za serikali za mitaa umekuwa na 'impac't kubwa?
Sababu washindani wenu wamegusa wananchi wengi hadi ngazi za chini kabisa huko vijijini.
Sasa mmepata uungwaji mkono mkubwa hadi toka kwa watu wasio na chama au wa CCM.
Imeonekana ni tatizo la wote, la wengi, la wananchi na sio la waliotumbuliwa au waliobanwa upigaji.
Hii imekuwa ajenda au kero mpya masikioni mwa wengi hasa watu wa kawaida.

UPANDE WA CCM NA MLINZI(PATRON) WAO:
Naona kuondoka kwa wazee wa tusker, goal la kisigino, na mwezi wa njaa(njanuari) na wengine wengi kumeondoa kundi la watu wenye kutumia mbinu za subira.
Utamkamata vipi kuku wako kama unatumia mbinu za mabavu zisizo za kificho?
Unatakiwa umuache kuku ajidai kidogo, avuruge nafaka au pumba huku unamvutia taratibu bandani umkamate.

Kwani miaka yote uchaguzi wa serikali za mitaa kulikuwa hakuna figisu na mabao ya misigino?
Kwanini safari hii uwanja mzima watazamaji wa timu zote na wachezaji wa timu iliyo ugenini wanampigia kelele muamuzi na kususia kuendelea kucheza mechi?

Tatizo kuna watu wametumia dakika 5 kuandaa mpango wa ushindi uliostahili kuandaliwa zaidi ya mwaka mzima tena na jopo la watu wenye busara au hekima za Mfalme Sulemani. Tatizo asafari hii imetumika njia ya mabavu na primitive, ingekuwa kwenye taaluma yetu ile tungeita BRUTE FORCE method.

Leo tuishie hapo, nitaendelea kwa CCM wakati mwingine ...
 
Labda kwa faida yako na wengine wenye mawazo kama yako ( ambao ni upungufu ) , wote uliowataja hapo hawajawahi kutumwa na chadema kuandika mitandaoni , ni watu wenye mawazo huru wanaoandika ukweli unaofahamika , na uliowataja wala hata hawajuani kabisa .

Msemaji wa Chadema anaitwa Tumaini Makene na labda viongozi wake .
 
Labda kwa faida yako na wengine wenye mawazo kama yako ( ambao ni upungufu ) , wote uliowataja hapo hawajawahi kutumwa na chadema kuandika mitandaoni , ni watu wenye mawazo huru wanaoandika ukweli unaofahamika , na uliowataja wala hata hawajuani kabisa .

Msemaji wa Chadema anaitwa Tumaini Makene na labda viongozi wake .
Mkuu mimi nimetoa mawazo au maoni tu, yanaweza kuwa sio sahihi au sahihi.
Kwa kuweka rekodi sawa hapa hausiki msemaji wa chama tu.
 
Ufala.com
tapatalk_1573980728131.jpeg
 
Unashauri nini kifanyike ili kujikwamua na hilo
Soma tena mkuu, kwa upinzani nimeshauri kidogo lakini kuna mengi sana ambayo nikiyaweka hapa naweza kujikuta adui wa upande wa pili.
Kwa CCM bado makala inaendelea, subiri sehemu ya pili .
 
Back
Top Bottom