Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) kimeingia kwenye mgogoro mkubwa na wapangaji wake zaidi ya 450 baada ya kuwapatia notisi ya kutakiwa kuhama katika nyumba zao ndani ya siku 60 hadi 90.
Wapangaji hao walioishi ndani ya nyumba hizo zilizoko eneo la Kijenge jijini Arusha kwa zaidi ya miaka 40, wamedai kuwa hawatahama katika nyumba hizo kwa sababu ya muda waliopatiwa ni mdogo huku wakidai AICC haijawatendea haki.
Mwananchi imezungumza na Assah Mwambene ambaye ni Ofisa Uhusiano wa AICC na amethibitisha kuwa taarifa za wapangaji hao kutakiwa kuhama ni za kweli.
Mwambene amesema AICC imeshawakabidhi barua za notisi wapangaji wote ikiwataka kuhama ndani ya siku 60 mpaka 90 kupisha eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji mpya.
MWANANCHI