Wape neno dereva na utingo wake

Wape neno dereva na utingo wake

Wacha watwaliwe tu na ziraili maisha chini ya awamu ya sita hayana dhamani kabisa
 
View attachment 1895253

Hawa jamaa siujui ni ujinga, ujasiri au kutegemea bahati kwa kuweka maisha yao rehani.

Wape neno!
Mkasi juu mkasi chini acha kabisa kule longijave arusha kama unaenda namanga nililitupa baada ya kuona linataka kunipeleka kwa muumba nimeshona nguzo nimetoa forest (nyuma ya mlima meru) mbona nilikula hapo mtu 3[emoji24][emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1895253

Hawa jamaa siujui ni ujinga, ujasiri au kutegemea bahati kwa kuweka maisha yao rehani.

Wape neno!
Hapo ukiwaambia wanakuona mjuaji au unajifanya wa kishua.

Watu kama hawa huwezi jua pengine waliumbwa ili watumike kama mifano kwenye jamii. So unamuacha tu yamkute.

Nakumbuka kuna jamaa alimpandisha mke wake na katoto kichanga usiku saa sita kutoka boko kuja tabata. Kisa ni lift ya bure. Nikamuuliza why unapandisha familia yako kwenye pikipiki tena anaendesha ndio hawa machakalamu. Ananijibu mimi sio wa kishua kama wewe, sasa kama hela ya tax sina nifanyeje....... ?!

Nikamuitia Uber ila nikamwambia kuilinda familia yako sio swala la kipato ni swala la kujali. Ungewajali ungewaandalia mazingira mapema sana ya kuondoka kwa usalama.
 
Back
Top Bottom