Hizi ni nyakati za mwisho, tutafanya uovu lakini siku moja itaisha. Naomba uwe mtulivu, kama kweli hii shida unayo ebu mwambie Mungu akupe moyo wa uvumilivu. Sisi tukianza kusema hapa tuliyonayo nafiikiri utampenda mumeo sana na kuona yake ni nafuu. Sasa basi shika kilicho chako, komaa nae, mwambie nakupenda sana mume wangu hata kama wewe hunipendi unaenda kwa nyumba ndogo zako.
Nikwambie the way tunavyosurubika na hawa wanaume huku kitaa ungemshika wako vizuri usimwache mumeo (hakuna kama yeye). . Ebu angalia wapi unakosea maana tunaongea mengi lakini tukija kwenye ukweli unakuta sisi ni vyanzo. Hata wewe siyo mwema/mzuri sana. Omba kwa ajili yako, ujisamehe, msamehe mwenzio maana bila hivyo hutasamehewa.