Wapendwa naona kama mwisho wangu umekaribia

Status
Not open for further replies.
Pole Sana .

Mimi naona tukuchangie mtaji hata million moja ukafanye Biashara hata Kwa kuanzia chini .

Pia usiache Kazi ya udalali hii huwa inalipa kiasili hii ndo Kazi namba moja duniani. Ya kuwaungaisha wat u.

Weka namba ya Account yako watu wakushike mkono
 
Mwanaume acha kudeka deka, acha kuwaza kirahisi rahisi hakuna kurudi nyuma wanaume ni simba kaka. Hakuna kutia huruma madogo wengi wako porini huku wanafanya kazi za hatari, wengine wanakufa wengine wanapata vilema na wanao toboa wanazikuta pesa wapo. Badilisha mazingira ya kazi hakuna kurudi nyuma mpaka pesa zipatikane.
 
Habari za wakati huu,

Sijui wapi pa kuanzia Ila tangia mwaka 2018 niliamua kuacha kazi na kuanza maisha ya kujiajiri.

Kazi niliacha baada ya kuona biashara zangu zingine ndogo ndogo zinalipa Ila changamoto ilikuwa ni kukosa usimamizi nzuri.

Pia sababu nyingine ilikuwa kutoelewana na supervisor wangu kutokana na roho ya kijicho kuona maendeleo niliyokuwa nayo hayaendani na mshahara ninaopata.ingawaje sikuwahi kuwa na loss yoyote au kujibizana naye Ila alichokuwa anafanya kunipiga Vita ya chinichini.kwanza mmiliki wa kampuni alikuwa ni mwenyeji wa Kanda ya ziwa hivyo kufanya asilimia kubwa ya wafanyakazi kuwa watu wa Kanda ya ziwa.

Pili kwenye vitengo vyote waliweka watu wa Kanda ya ziwa. Mimi peke yangu ndio nilikuwa mtu wa kaskazini.hii ilipelekea supervisor wangu kutengeneza na kueneza sumu ya chuki kwa urahisi kuwa watu wa kaskazini ni wezi .turudi kwenye mada

Baada ya kuacha kazi mambo yalinyooka kuliko mwanzoni.niliwaza muda wote nilikuwa wapi kwanini sikuingia mapema kwenye biashara.Ndani ya miaka mitatu nilifanikiwa kupata sehemu ya kujihifadhi na kausafiri kutokana na wakati mwingine Mishe zangu zilikuwa za udalali.

Mwishoni wa mwaka 2022 mambo yalianza kwenda mrama baada ya kuhamia kwenye kibanda changu.Mama yangu mzazi alikuwa akiumwa kifundo Cha mguu na pilingili mbili za mgongo zilikatika pia na sukari ilikuwa ikimsumbua.Hivyo ilibidi aje dar as salaam kwa ajili ya tiba

Tulipambana naye kwa wakorea pale mbezi kwa msuguri ikashindikana tukahamia mhimbili huko nako hakukuwa na nafuu ya kudumu.wakati huo nilikuwa na mtoto mdogo ambaye alikuwa Hali chakula Wala usiku halali.Lakini changamoto haikushia hapo kwenye maisha ya nyumbani.usiku kulikuwa hakuna kulala Mara watu wanagonga mlango wengine wanafagia nje .ukichungulia nje huoni mtu yoyote .hili nilimaliza kwa njia maombi

Changamoto hizi hazikuishia nyumbani tu Bali hata sehemu zangu za kutafuta ridhki.nilikuwa na ofisi mbili moja ya uwakala nyingine ya duka la vinywaji vya jumla na rejareja.Pesa nyingine nilikuwa nazungushia kwenye udalali.

Siku isiyokuwa na jina naenda kufunga hesabu kwenye ofisi ya uwakala mambo hayakuwa mazuri.Wakala hakuwa na cash yoyote wa float.pesa iliyokuwepo ilikuwa ni kamisheni jumla yake Kama laki tatu na machenchi.kuulizia pesa nyingine nikaambiwa iko kwa wakala mwenzake.basi pale tukagawana faida nikaondoka.kufupisha stori Yule wakala alikuja akasema pesa ametapeliwa hivyo atanilipa mdogo mdogo.

Wakati huo nimeshauza gari la kutembelea ili ninunue guta.kumbe guta limeuzwa Mara mbili na Mimi ndiye mtu wa pili .kufupisha guta sikupata niliishia kulipwa mdogo mdogo.

Duka la vinywaji Mambo hayakuwa mazuri nilichezea vitasa Sana kwa TRA kutokana na mambo ya risiti .mbaya zaidi madeni yalikuwa mengi kwenye mabar na mapub .kuna meneja alifukuzwa kazi ,Kuna miliki alishindwa kulipa Kodi ya mwaka mzima Kama mwenye nyumba anavyotaka.

Kifupi ndani ya mwezi wa 11 mwaka 2022 maji yalifika shingoni ikabidi niende nyumbani Kilimanjaro kupumzisha akili.huku nikiwa siamini ni nini kilichonitokea.hatimaye Kodi ya duka iliisha duka nikarudisha kwa mwenye nalo.nikauza vitu vyote vya dukani pia asilimia kubwa niliuzia members wa if.

Tokea hapo maisha yakawa ni kuunga unga mjini kwa kutumia uzoefu .Naishi kwa kulipwa madeni na kuongeza madeni mapya .nikajaribu kutafuta kazi mtaani na humu jf Lakini sikufanikiwa mpaka Sasa bado mambo yamekuwa magumu.

Kusudi la kuandika haya yote wakuu kwa Sasa nimekosa rafiki au hata mtu wa karibu wa kuzungumza naye magumu ninayopitia.mke amerudi kwao amechoka kukaa na mtu anayeishi maisha ya kubahatisha .Nimeamini wakati wa magumu hata wapendwa wako wa karibu wanajitenga na wewe

Wakuu najiona kama nafika mwisho na siku zangu zinahesabika kwa sababu nimebaki na mama yangu na mtoto wangu mdogo.wote wananitazama Mimi Lakini kiukweli jaribu limekuwa kubwa kuliko uwezo wangu.madukani madeni yamefika mwisho.

Wakati mwingine huwa napiga saidia fundi ikipatikana maisha yanaenda japo nakuwa slow kutokana sio mzoefu na hizo Kazi.Pia Nina diploma ya mechanical engineering na leseni class d ,e na c1,c2 na c3 Ila leseni kwa Sasa leseni ni ya kurenew

Napatikana kibaha kwa Mathias wakuu .mwenye ajira yoyote ya halali naomba anishike mkono
Hongera kwa kupambana.

KAMWE USIKATE TAMAA
 
Mkuu ukiacha interest kwenye mambo ya Ujenzi, nimependa business skills zako na collapse experience...

Kama hutojal naomba sana nicheki PM tuyajenge...
 
Maombi kwa muumba wako ni muhimu kila siku.. jiombee,ombea familia yako,kazi/biashara yako.. mshirikishe Mungu kila hatua.. usichanganye imani.. (mchana nyumba za ibada,then usiku kwa kalumanzira..mbaya sana). Fanya review ya maisha yako ya imani.. mafanikio na kuanguka ni zao la roho,sio vita ya kimwili.. ninayo mengi
 
Mwanaume acha kudeka deka, acha kuwaza kirahisi rahisi hakuna kurudi nyuma wanaume ni simba kaka. Hakuna kutia huruma madogo wengi wako porini huku wanafanya kazi za hatari, wengine wanakufa wengine wanapata vilema na wanao toboa wanazikuta pesa wapo. Badilisha mazingira ya kazi hakuna kurudi nyuma mpaka pesa zipatikane.
Kila mtu Ana namna yake ya kubeba matatizo yanayomkabili kwa wakati huo kutokana na uzoefu wake na uwezo binafsi wa kufirkiri.Tokea niandike huu uzi kwa kiasi kikubwa nimepata mawazo mapya na connection za hapa na pale .

Ni tofauti Kama ningekaa kimya msongo wa mawazo nimeupunguza Kama sio kuumaliza.mwisho wa yote jamii forum imekuwa ni Kama sehemu ya maisha yangu kwa kipindi kirefu.
 
Pole Sana .

Mimi naona tukuchangie mtaji hata million moja ukafanye Biashara hata Kwa kuanzia chini .

Pia usiache Kazi ya udalali hii huwa inalipa kiasili hii ndo Kazi namba moja duniani. Ya kuwaungaisha wat u.

Weka namba ya Account yako watu wakushike mkono
Ubarikiwe Sana mkuu kwa moyo wa utoaji nazidi kujiona sehemu sahihi..nam
Pole Sana .

Mimi naona tukuchangie mtaji hata million moja ukafanye Biashara hata Kwa kuanzia chini .

Pia usiache Kazi ya udalali hii huwa inalipa kiasili hii ndo Kazi namba moja duniani. Ya kuwaungaisha wat u.

Weka namba ya Account yako watu wakushike mkono
Shukrani mkuu kwa moyo wa utoaji.
21210021343 NMB..Kelvin emanuel
 
Shukrani mkuu Hapo keds kwa wachina napafahamu vizuri .kazi ya kulipwa kwa wiki kwa upande wangu inakuwa ngumu kwa sababu nauli ya kwenda na kurudi Kila siku ukijumlisha na chakula inakuwa kipengele kwa upande wangu

Niko natafuta backup ili niweze kukomaa na kazi za kulipwa kwa wiki au hata kwa mwezi
 
Pole sana Ndg yangu kwa changamoto.Nimepitia huko na Bado naendelea kupambana mambo yamekuwa nafuu kuliko jana.USHAURI wangu ...
Mtangulize sana Mwenyezi Mungu,piga magoti ukiwa mwenyewe Lia na usali,akupe faraja na Amani maishani(mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote na wala usitegemee akili zako mwenyewe ,katika shida zako umkiri yeye naye atayanyoosha maisha yako.Kama ni Mkatoliki tafuta Novena ya MTAKATIFU RITA ..
ONYO;kipindi hiki Cha majaribu usithubutu hata kidogo USHAURI wa kwenda kwa waganga
Imani hizi napingana nazo Sana mkuu ndo maana inakuwa kwangu kupata backup kwa ndugu zangu .Wananiambia mpaka niende kwa mtaalam nisafishwe ndo nirudi kwenye ramani

Pia wakati nayumba walinishika mkono kiasi Fulani. dakika ya mwisho wakasema bila kusafishwa siwezi kutoboa.isivyokuwa bahati wameambiana wote Mimi nimefungwa Sana mpaka siamini mambo ya ushirikina.Hivyo wakinishika mkono ni kupoteza hela zao.ugumu zaidi unakuja pamoja na Mimi kutembelea rimu kwa muda mrefu wengi wa ndugu zangu hawajafikia hatua niliyokuwepo..hivyo inawapa mashaka kumshika mtu mkono aliyekuzidi kiasi Fulani kimaisha
 
kuna yule jamaa anaitwa kiboko ya wachawi ushamuona? mwamposa je? au nenda kwa mwakasege ukishindwa kabisa muone hata godilavu mzee wa jicho la tatu...... mizimu ya kwenu umeitembelea lini....

usije ukafuata ushauri wangu utapotea
 
Shukrani mkuu Hapo keds kwa wachina napafahamu vizuri .kazi ya kulipwa kwa wiki kwa upande wangu inakuwa ngumu kwa sababu nauli ya kwenda na kurudi Kila siku ukijumlisha na chakula inakuwa kipengele kwa upande wangu

Niko natafuta backup ili niweze kukomaa na kazi za kulipwa kwa wiki au hata kwa mwezi
Ni kweli ungekuwa na mtaji ungefungua hata genge ikawa unapambna km Kuna mtu nyumbni ukamuacha ukaenda kupmbna huko japo kule ni mateso mapumziko ukafanya shughuli nyingine ni changamoto
 
Huna ulinzi meku, umepigwa rohoni unachokiona ni matokeo ya pigo tu. Rekebisha mifumo yako ya ulinzi kiroho...kama unaegemea upande wa nuru komaa na damu ya Yesu...kama unaegemea upande wa giza...toa kafara ya damu. Ukikamilisha hayo, rudi kwenyw game
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom