Wapendwa naona kama mwisho wangu umekaribia

Status
Not open for further replies.
Pole Sana .

Mimi naona tukuchangie mtaji hata million moja ukafanye Biashara hata Kwa kuanzia chini .

Pia usiache Kazi ya udalali hii huwa inalipa kiasili hii ndo Kazi namba moja duniani. Ya kuwaungaisha wat u.


Weka namba ya Account yako watu wakushike mkono
 
Mwanaume acha kudeka deka, acha kuwaza kirahisi rahisi hakuna kurudi nyuma wanaume ni simba kaka. Hakuna kutia huruma madogo wengi wako porini huku wanafanya kazi za hatari, wengine wanakufa wengine wanapata vilema na wanao toboa wanazikuta pesa wapo. Badilisha mazingira ya kazi hakuna kurudi nyuma mpaka pesa zipatikane.
 
Hongera kwa kupambana.

KAMWE USIKATE TAMAA
 
Mkuu ukiacha interest kwenye mambo ya Ujenzi, nimependa business skills zako na collapse experience...

Kama hutojal naomba sana nicheki PM tuyajenge...
 
Maombi kwa muumba wako ni muhimu kila siku.. jiombee,ombea familia yako,kazi/biashara yako.. mshirikishe Mungu kila hatua.. usichanganye imani.. (mchana nyumba za ibada,then usiku kwa kalumanzira..mbaya sana). Fanya review ya maisha yako ya imani.. mafanikio na kuanguka ni zao la roho,sio vita ya kimwili.. ninayo mengi
 
Kila mtu Ana namna yake ya kubeba matatizo yanayomkabili kwa wakati huo kutokana na uzoefu wake na uwezo binafsi wa kufirkiri.Tokea niandike huu uzi kwa kiasi kikubwa nimepata mawazo mapya na connection za hapa na pale .

Ni tofauti Kama ningekaa kimya msongo wa mawazo nimeupunguza Kama sio kuumaliza.mwisho wa yote jamii forum imekuwa ni Kama sehemu ya maisha yangu kwa kipindi kirefu.
 
Ubarikiwe Sana mkuu kwa moyo wa utoaji nazidi kujiona sehemu sahihi..nam
Shukrani mkuu kwa moyo wa utoaji.
21210021343 NMB..Kelvin emanuel
 
Shukrani mkuu Hapo keds kwa wachina napafahamu vizuri .kazi ya kulipwa kwa wiki kwa upande wangu inakuwa ngumu kwa sababu nauli ya kwenda na kurudi Kila siku ukijumlisha na chakula inakuwa kipengele kwa upande wangu

Niko natafuta backup ili niweze kukomaa na kazi za kulipwa kwa wiki au hata kwa mwezi
 
Imani hizi napingana nazo Sana mkuu ndo maana inakuwa kwangu kupata backup kwa ndugu zangu .Wananiambia mpaka niende kwa mtaalam nisafishwe ndo nirudi kwenye ramani

Pia wakati nayumba walinishika mkono kiasi Fulani. dakika ya mwisho wakasema bila kusafishwa siwezi kutoboa.isivyokuwa bahati wameambiana wote Mimi nimefungwa Sana mpaka siamini mambo ya ushirikina.Hivyo wakinishika mkono ni kupoteza hela zao.ugumu zaidi unakuja pamoja na Mimi kutembelea rimu kwa muda mrefu wengi wa ndugu zangu hawajafikia hatua niliyokuwepo..hivyo inawapa mashaka kumshika mtu mkono aliyekuzidi kiasi Fulani kimaisha
 
kuna yule jamaa anaitwa kiboko ya wachawi ushamuona? mwamposa je? au nenda kwa mwakasege ukishindwa kabisa muone hata godilavu mzee wa jicho la tatu...... mizimu ya kwenu umeitembelea lini....


usije ukafuata ushauri wangu utapotea
 
Ni kweli ungekuwa na mtaji ungefungua hata genge ikawa unapambna km Kuna mtu nyumbni ukamuacha ukaenda kupmbna huko japo kule ni mateso mapumziko ukafanya shughuli nyingine ni changamoto
 
Huna ulinzi meku, umepigwa rohoni unachokiona ni matokeo ya pigo tu. Rekebisha mifumo yako ya ulinzi kiroho...kama unaegemea upande wa nuru komaa na damu ya Yesu...kama unaegemea upande wa giza...toa kafara ya damu. Ukikamilisha hayo, rudi kwenyw game
 
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…