Wapendwa, nifanyeje niache POMBE?

Wapendwa, nifanyeje niache POMBE?

Kuna jamaa yetu ananafasi kubwa tu kwenye taasisi fluni ya serekali alikuwa mlevi sana pamamoja na maombi na ushauri nasaa lakini ilishindikana kabisa kuacha pombe.

Ilifikia mahali tuna mkwepa kunywa naye maana tunajua atasumbua kupelekwa home.

Ilifikia mahali mke wake alitaka kuomba talaka waachane maana jamaa alikuwa akipiga vyombo mpaka anazima na kojo juu analetwa nyumbani hajitambui.

Siku moja nilikutana mzee mmoja anauza dawa ya kuacha pombe hivyo nikamuunganisha na mke wake ingawa bei ilikuwa imechangamka 800,000 lakini mke wa jamaa alitoa cash.

Kwa hiyo alipewa dawa mbili moja ya kuacha pombe na ya pili ni yakupunguza ukali wa wa dawa ya kwanza ambayo hii dawa ya kuacha pombe aliambiwa achanganye kwenye chakula au pombe na iwe siku ambayo kesho yake hataenda kazini, huyo mzee alimuhakikishia kama hataitafanyakazi na jamaa kuacha pombe basi arudi apewe dozi ya pili.

Basi mke wa jamaa akamsubiri mume wake amerudi toka kazini akamwandalia chakula ambacho kimechanganywa na dawa basi jamaa akagonga msosi fresh na baadaye akatoka zake kama kawaida yake akapate moja moto moja baridi.

Baada pombe kukolea jamaa kavua nguo zote akaanza kukimbia kuzunguka mtaani huku akiimba huku nyuma watoto kibao wanakimbia wakiimba wakimtaja jina lake.... majita majita majita....(si jina lake) naye ndiyo mzuka unapanda kwelibkweli anapiga na pushup..mara kuruka ruka...yaani hivyo.

Baadaye mke wake akapata taarifa kutoka kwa majirani kuwa baba....fluni amevua nguo zote anazinguka mtaani ndiyo mke wake kukimbia pale na wanaume wakamshika wakamfunga kanga na kumpeleka mpaka home mkewe akawa analia sana basi ndiyo akasema alimpadawa ya kuacha pombe lakini alipewa na ya kupunguza makali ambayo walikorogea kwenye maji wakampa ndiyo akapata hauweni na usingizi juu.

Usiku kushituka mkewe akampa mkanda wote kilichotokea, jamaa alijisikia vibaya sana kesho yake alienda kazini kuomba off ya ugonjwa akaunganisha na likizo akahama mtaa akahamia kwenye nyumba yake ingawa ilikuwa haijaisha hivi leo jamaa ni swala tano halafu kawa mstaarabu kweli kama siyo yule cha pombe.

Chaajabu zaidi jamaa na mke wake toka siku hiyo hatunamawasiliano mazuri tena, badala ya kunishukuru, ule ukaribu wa awali hatuna tena.

Leo watu wanaomba niwaunganishe na huyo mzee kwakweli nimegoma na wala sitaki kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulivyokaa !! Ni mataptap kwa sababu ya ufukara . Pombe sio chai , kuacha ni dhamira tu (change your attitude) ukipata pesa nunua maziwa unywe na mengine peleka nyumbani , afya itabadilika na utaona taptap sio dili . Baadae utaona kipato kinaongezeka na maisha yatabadilika . Mimi napata siku moja moja kama mfuko unaruhusu na pombe hainitawali kwani sio hitaji muhimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom