Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

<br><br>mkuu hapo umenena na hii ndo gharama yake inajitokeza
 
mamii mungu atakupigania utaishinda hii mitihani. Jitahidi kujibu maswali ya huyo baba erick na bmp ingawa mengine nayaona ni CRAP ila huwezi jua labda wanataka kukushauri jambo la maana.

mmmh tunatafuta mzizi wa tatizo
 
hebu niambie akikwambia ndoa ilidumu miaka 6 au 20 itasaidia nini katika kumfanya huyu mama aweze kumake decision?

katika hicho kipindi ambacho kwako unaona hakina maana cha miaka 6 au 20 unavyodai lazima kuna tabia au migogoro iliyokuwepo katika maisha ya kila siku na pia maisha gani baba aliishi na mwanaye .. maana kuna ndoa zingine baba au mama anaweza kutokujali watoto hivyo tukawa tunahuku watu baada ya kuachana kumbe tatizo lilikuwepo hata kabla ya kuachana
 
Husninyo mzizi wa tatizo nitaeleza siku nyingine sio leo, na hata nikieleza watasema wanataka upande wa pili, leo nimetoa hili kwanza mamii nahitaji msaada waq mawazo tu
 
Sishangai wewe ni wa 2. Sijui elimu yako na huyo supposed to be Perfect Man lakini exact case ilitokea kwa parents 2 na wote ni graduates.
Aaaaaahg hata kama sio mwanao ni wa jirani, is there any reason kumfanyia binadamu mwenzako such a smooth killing!
Kina dada huwa mnaonyesha mapenzi makubwa sana kiasi kwamba jamaaa akikumbuka na anaona umemdhibiti ndio anafanya hayo.
Pole sana dada.
 
mkuu mbona naona hizo information kwa sasa ni irrelevant. Huyo mzee hata kama huyo mtoto asingekuwa amemzaa yeye kiungwana sio vizuri kabisa alichokifanya.

Mkuu hizo information ni relevant tena sana kwa sababu nafikiri suala kwa sasa sio alichofanya bali kwa nini alifanya alichofanya. Kuna umuhimu wa kujua kwa nini alifanya vile. Ili kujua ni lazima kuwa na information kama hizo. Kama wewe ungekuwa mshauri na huyu akaja kutaka ushauri, ungejump kwenye conclusion basing on alichokisema na kufanya assumptions kwenye ushauri wako? Vipi upande wa pili ukija kesho yake na completely opposite story. I am sure unakumbuka stories za Theone na mke wake. Bado hatujajifunza kutokana na zile thread zao?
 

Mkuu hapo kwenye red uko 100% right. Na ndio maana wengi tunashindwa kukupa ushauri wa maana kwa sababu tusilolijua ni sawa na usiku wa giza. Lakini kadri tunavyokubana ndivyozidi kutoa more info. Kama alishakutangaza kama wewe ni marehemu kwa nini bado unatumia namba zake tena kwenye masuala yanayohusu wanao? Mkuu unapoamua kutafuta ushauri ni lazima ukubali kudiclose all the relevant information, otherwise hutapata ushauri unaohitaji. Inaonekena kuna zaidi ya tuyajuayo.
 
nasubiri kwa hamu aje akanushe Kaka sio kitu unaweza kukitungia uongokama unavyofikiri ili nipate faida gani, au sifa gani kuna vit vinaumiza kwenye mahusiano
 
Husninyo mzizi wa tatizo nitaeleza siku nyingine sio leo, na hata nikieleza watasema wanataka upande wa pili, leo nimetoa hili kwanza mamii nahitaji msaada waq mawazo tu

ina maana ulikuwa una-beep ??? kuwa muwazi watu wakushauri sahihi sasa hapo unaweza kuamini umepata ushauri wa kutosha??? au ulikuwa unataka watu washauri kama wewe unavyodhania???
 
Reactions: EMT
Muda uliopo si wa ku-deal na huyo x husband, wewe nenda Bagamoyo, Father ambaye ni Manager mara nyingi yuko Marian Girls, kamuone, ongea naye atakuelewa vizuri sana, hao waliokujibu katika simu huwa wanakuwa na majibu hayo kupunguza maswali. Ninavyofahamu nafasi ya mtu haiwezi kutolewa kwa mwingine kwa kutumia majibu ya simu tu na hasa majibu yenyewe yakiwa kama ya huyo x husband wako. Kamuone Father.
 
Reactions: EMT

hahahaha dada naona unaanza kusogea taratibu hapo kwenye nyekundu ndo kuna tatizo utazunguka kote lakini tatizo huwezi kulikwepa kwani inaonekana malezi ya watoto kwenu ni kama kukomoana au kuonyeshana nani zaidi &nbsp;kitu ambacho naamini hakiwajengi watoto
 
nasubiri kwa hamu aje akanushe Kaka sio kitu unaweza kukitungia uongo kama unavyofikiri ili nipate faida gani, au sifa gani kuna vit vinaumiza kwenye mahusiano

majibizano au mashindano hata kudhalilishana hakusaidii na inaonyesha unapenda mashindano na majibizano, kumbuka hayajengi na wala hayatasaidia watoto ..

kawaida tatizo si tatizo bali jinsi ya kumaliza tatizo ndo tatizo
 
Reactions: EMT
majibizano au mashindano hata kudhalilishana hakusaidii na inaonyesha unapenda mashindano na majibizano, kumbuka hayajengi na wala hayatasaidia watoto ..

kawaida tatizo si tatizo bali jinsi ya kumaliza tatizo ndo tatizo
Kweli kabisa mkuu
 

Mkuu labda nikuulize swali. Kwenye post yako ya mwanzo umesema kuwa hujawahi kuumia kama ulivyoumia baada kutapata maelezo toka shuleni kuwa baba alisema mtoto yupo kwa mama yake na yeye baba hayamhusu so hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine. Kwenye hii post umesema kuwa alishawaambia watoto kuwa hawana mama kwa ville alishakufa. Kati ya haya mawili lipi la kuumiza zaidi. Watoto kuambiwa hawana mama kwa vile alishakufa wakati mama yuko hai au shule kuambiwa mtoto yupo kwa mama yake na yeye baba hayamhusu kwa hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine?
 

inawezekana mimi nimelichukulia jambo kirahisi au sijaelewa topic. Huyu mama kilichomuuma na kumkera ni baba kuharibiwa mpango wa shule wa mtoto, inawezekana kabisa walikuwa na ugomvi mingi kabla ya hili lakini hajataka kutushirikisha. Issue iliyopo mezani ni hiyo ya shule, anauliza huyo baba amfanye nini? Watu mmekazana kuuliza ooh ndoa ina miaka mingapi, hapo nyuma alikuwa ana upendo? Umuhimu wake ni nini kwa sasa? Ndoa kama ilikuwa na miezi 3 au miaka miwili itataleta tofauti ya ushauri utakaompa? Kama ndio, kivipi?
Halafu kama hutajali naomba uniwekee link ya threads ya theone na huyo mkewe. Nahisi zilinipita.
 
Reactions: EMT

husn , hakuna kitu kisichokuwa na historia au chanzo na wengi hupenda kuanzia kwenye tatizo pasipo kutaka kujua chanzo cha tatizo ni nini... kumbuka mpaka inafikia mtu kuwaficha watoto kwa miaka miwili au kukataa kusupport mtoto shule lazima kuna jambo au kitu kilichojificha .. na ushauri bora ni kupata kilicho sahihi lakini ukiwa unatoa kitu nusu hutafaidika na ushauri japo unaweza kudhani wanachosema wachangiaji ni sahihi kumbe unaweza ukapotoka zaidi
 

Yale yale.............. HOPELESS!! No matter what the facts could have been, hizi tabia za kuhamishia ugomvi kwa watoto zinatakiwa zife! Think twice, kama baba anamsusa mtoto leo siku ikitokea huyu mama amekuwa disabled unadhani hayo maisha ya mtoto yatakuwaje?? Eti kisa mama kasababisha! Wewe unadhani kususa kwa baba yenu kungekuwa na faida kwenu kama mama yenu angekuwa hana uwezo wa kuwatunza hata kama ni ye ndo mwenye makosa?? Si mngekuwa mnaranda tu mitaani huku mkisikia kauli za 'mama yao ndo aliyataka' wakati maisha yanaendelea kuwachapa!! Au we utafurahi kumuona mwanao anapoteza muelekeo kwa kosa lililofanywa na mama yake, tena ambalo lipo ndani ya uwezo wako?
 
Reactions: BAK

Issues iliyo mezani sio ya elimu ya mtoto tuu bali pia anataka ushauri amfanye nini huyo baba. Sasa kama baba alishawahi kuwaambia hata watoto kuwa mama yao ni marehemu and got away with it unafikiri kwa hili mama atafamfanya nini? Issue ya elimu ya mtoto ameshauriwa na wachangiaji wengi tuu hapo juu lakini inaelekea pia anataka ushauri amfanye nini huyo baba. Ndio maana maelezo zaidi yanahitajika.

Na katika kumbana ndio katupa info kuwa baba alishawahi kuwaambia watoto kuwa mama ni marehemu which make the issue even more complicated and serious than previously thought. Mtu akutangaze kwa watoto wako uliowazaa kuwa ni marehemu and you still not only keep his telephone number but also unaitumia officially? Kama huyu mama anataka baba awe fully responsible kwa ada ya mtoto ni bora awe direct.

Ndoa iliyodumu kwa siku mbili ni tofauti na iliyodumu kwa miaka miwili. Kwa mfano, huwezi kuoa na kudivorce within two days halafu utake mgawane mali ulizonikuta equally. And who knows labda wapo ambao wanapenda kushauri warudiane for the best interest ya watoto? Duration na nature ya ndoa vinaweza pia kusaidia kujua connection ya watoto na baba.

By the way kwenye form alijaza nani atalipa ada n.k? Baba, mama or both? Paying secondary school tuition is often a contractual obligation in a divorce decree. Kwenye divorce decree walikubaliana nini kuhusu kumsomesha huyu mtoto hasa kwenye elimu ya sekondari?
 
Baba Erick hata kama mama wa mtoto alimkosea vipi huyo baba, still hakuna justification yoyote ya kuhamishia kisirani kwa mtoto-tofauti zenu wazazi zibaki kwenu wenyewe hazihusiani kwa namna yoyote na mustakabali wa mtoto

wakati mwingi wanawake hufunza watoto kuwadharau wazazi wao wa kiume pale ambapo wazazi hao wametengana. Baba yako hakujali, si unaona mimi peke yangu ndio ninahangaika na wewe, nijue ule nini, uvae nini, baba yako hana habari na wewee...mwishowe mtoto/watoto wanajingea tabia ya kuwa baba hatujali na wala hatupendi. Mtoto na mama alienda kumwambia baba yake kuwa anaenda kuomba shule gani? Kama hawakumshirikisha baba tangu mwanzo. Baba huyo ana kila sababu ya kufanya ivo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…