nyie kuna kitu hamjakifahamu ndugu zangu! Fuatilia simulizi hii inayonihusu mimi mwenyewe!
Nilizaliwa miaka zaidi ya ishrn ilyopita na wkt ninakua nikajikuta ninaish na mama yangu pekee,alitupenda sana wanae na kutusomesha hadi sasa ndo yeye anahusika na nipo chuo sasa,
ilipofika wkt wa kuhoji baba yetu alipo tulielezwa na mama yetu mambo mengi sana akimtuhumu mzee kwamba hafai na kiufupi alitujengea concept ya kumchukia baba yetu,na alifanikiwa sana.
Kumbe walikuwa na ugomvi wao kwa muda mrefu na mama alitutumia kama ngao kuficha ukorofi wake,na kwa vile waliishi separate,sisi tulikuwa kwa mama,
nilipomaliza form6 nilikaa na mzee na kupata maelezo yake kuhusu ugomvi wake na mama! Japokua mama kanisomesha had chuo kikuu leo,najuta sana kwa kutokufaham ukwel mapema na kujikuta namchukia baba yangu bure,nilipougundua ukwel nilimtafuta mzee mwenye age kama ya baba yangu nikaomba anisaidie kuomba msamaha kwa baba na baba akanisamehe na ndo mwanzo wangu ku balance kwa wazazi wangu wote na sasa naishi kwa amani moyoni.
Kwahyo,naamin kwa aliyefuatilia kisa hiki,atakuwa ameelewa kwanin huyo baba anawaona kama mama na wanae lao moja!
Kumbuka hakuna baba anayependa mtoto wake aegemee upande mmoja tu wa wazazi wkt yeye yupo hai.