Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

Wapendwa nimfanyaje huyu X husband

Mkuu hapo kwenye red uko 100% right. Na ndio maana wengi tunashindwa kukupa ushauri wa maana kwa sababu tusilolijua ni sawa na usiku wa giza. Lakini kadri tunavyokubana ndivyozidi kutoa more info. Kama alishakutangaza kama wewe ni marehemu kwa nini bado unatumia namba zake tena kwenye masuala yanayohusu wanao? Mkuu unapoamua kutafuta ushauri ni lazima ukubali kudiclose all the relevant information, otherwise hutapata ushauri unaohitaji. Inaonekena kuna zaidi ya tuyajuayo.

unajua kaka mi siamini kama kweli huyu mama ndiye mwenye watoto wakubwa hivi alafu anajicontradict kama mtoto. Sasa ukawachukua kwa kujitia unaweza kuwa somesha alafu ukaandika namba za baba ili nini? Wewe huna simu? Au bado unajigonga kwake ile hali umeshabwagwa? Nonsense
 
ukiomba ushauri kuna mambo mengi sana lazima uyaweke wazi lakini naona watu wengi huficha na kutaka wapate ushauru kulingana na wao wanachotaka kiwe kwa kuamini makosa yabaki upande wanaoutuhumu
 
Mara nyingine huwa sielewi tunakuwaje sie akina mama.... unajua kabisa ribwana rako harina akiri, mnashindana kuonyeshana ubabe, halafu, bado unatoa mwanya kwa hayo mauza uza kuwafikia watoto.... hapo ndipo sikuelewi. Kwani wewe huwezi kulea mwenyewe ukae kimya hadi awe tayari mwenyewe kuwafuatilia? Sikukuelewa kabisa, kabisa kwa nini uliweka namba zake za simu shuleni. Unajidai unamwaga mboga, yeye anavuta sahani ya ugali anamwaga anakojolea hata kuwapa mbwa haiwezekani. Nani anakuwa amekomeshwa hapo? Please weka watoto mbali na hizo game zenu... I hate it! Nimepita huko na sikutoa hiyo ruhusa.
 
Ndiyo haya haya tunayosema kila siku kuwa kuna watu wengine wanawaza kwa kutumia makalio! Sasa huyo X mumeo sijui alikuwa na maana gani kuyatenda hayo, pole sana!

Kwa sasa achana na kuwazia yaliyopita. Fanya hima rudi shule nenda kajaribu kumombea hiyo nafasi, na kama utakosa mtafutie shule nyingine. This time ukumbuke kutoa namba yako ya simu na details zako na siyo huyo X mumeo.

Pole na kila la kheri ktk kuanza upya.
 
inawezekana mimi nimelichukulia jambo kirahisi au sijaelewa topic. Huyu mama kilichomuuma na kumkera ni baba kuharibiwa mpango wa shule wa mtoto, inawezekana kabisa walikuwa na ugomvi mingi kabla ya hili lakini hajataka kutushirikisha. Issue iliyopo mezani ni hiyo ya shule, anauliza huyo baba amfanye nini? Watu mmekazana kuuliza ooh ndoa ina miaka mingapi, hapo nyuma alikuwa ana upendo? Umuhimu wake ni nini kwa sasa? Ndoa kama ilikuwa na miezi 3 au miaka miwili itataleta tofauti ya ushauri utakaompa? Kama ndio, kivipi?
Halafu kama hutajali naomba uniwekee link ya threads ya theone na huyo mkewe. Nahisi zilinipita.

nami ningependa kupata hiyo link ya theone na mkewe
 
Mara nyingine huwa sielewi tunakuwaje sie akina mama.... unajua kabisa ribwana rako harina akiri, mnashindana kuonyeshana ubabe, halafu, bado unatoa mwanya kwa hayo mauza uza kuwafikia watoto.... hapo ndipo sikuelewi. Kwani wewe huwezi kulea mwenyewe ukae kimya hadi awe tayari mwenyewe kuwafuatilia? Sikukuelewa kabisa, kabisa kwa nini uliweka namba zake za simu shuleni. Unajidai unamwaga mboga, yeye anavuta sahani ya ugali anamwaga anakojolea hata kuwapa mbwa haiwezekani. Nani anakuwa amekomeshwa hapo? Please weka watoto mbali na hizo game zenu... I hate it! Nimepita huko na sikutoa hiyo ruhusa.

tatizo wakina mama wengi hupenda sana waonewe huruma lakini hawajui madhara ya hiyo huruma ni nini .. kuna muda unatkiwa mtu kujitoa mhanga au kujishusha kwa ajili ya watoto lakini wengi wanadhani kufanya hivyo atakuwa kamyenyekea mwanaume
 
aisee...pole sana!!japo na wewe unakosa kwa kutomtaarifu ila baba nae ana kosa zaidi
 
Wewe ndiye unamakosa mumy kwani umetoa personal contacts bila idhini ya muhusika pia hukumshirikisha muhusika. Pia we umemweleza mwanao ya nini sasa. Inaonyesha una-depression

ashilikishwe kwa nini mbona mnamtetea sana huyu baba mkwepa majukumu,wakati anazaa alitegemea zitakuwa zinaandikwa information za nani kuhusu watoto wake, mtoto ni wake ndo maana mama akaandika number za baba na mama wa mtoto, RIP baba ningekuchunia mpaka ukajinyonga
alikwepa majukumu kama huyu,bahati yako sikuwi kukujua
 
Pole dada,chamsingi nikuachana na huyo mtu asie kua na fadhila wala hisani hata kwa mtoto wake na sijui kama anajua umuhimu wa mtoto kusoma,
Usife moyo wala hukufanya kosa kuandika number yake ya cm kwani ulikua na nia safi na mzazi mwenzio,na wala huna haja yakumtia mtoto sumu kumueleza chochote usimchanganye na masomo yake,jitahidi kusahau huo upupu wake na shughulika na maisha ya mtoto yeye iko siku atajutia alichofanya...
 
ashilikishwe kwa nini mbona mnamtetea sana huyu baba mkwepa majukumu,wakati anazaa alitegemea zitakuwa zinaandikwa information za nani kuhusu watoto wake, mtoto ni wake ndo maana mama akaandika number za baba na mama wa mtoto, RIP baba ningekuchunia mpaka ukajinyonga
alikwepa majukumu kama huyu,bahati yako sikuwi kukujua
Kate sweetie pole mydia ulivyoimalizia post yako imenigusa sana.
Hata hivyo ninaamini kuwa kuna issues hapa baina ya kyelli na mumewe! Miaka sita mko apart afu bado kuna chuki za kukomoana kijinga namna hii!?
 
Utakuta wewe unahangaika nae hivyo baadae mtoto atasoma kwa shida na atafanikiwa.usishangae wakati huo mtoto akaanza kumtunza baba yake na kukusahau wewe!!!Hii duni sijui ikoje???wewe fanya lililo sahihi kwa mwanao wala usimfikirie baba wa mtoto.Kama unajiweza songa mbele( na kweli wajiweza).Hii ifanye kama stori tu wala usiishikie kidedea.shule ziko nyingi atasoma na kufaulu si lazima asome hapo.ukubali pia kuwa ulifanya kosa kujipendekeza kuweka namba yake
 
huyo mr usimshirikishe tena kwenye swala lolote lianalohusu wewe na mwanao
 
Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.

Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.

Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.

Asanteni nakaribisha ushauri wenu
pole dada.
ebu jipe moyo sissta, kama mlisha achaa miaka saba ukaumia kwa kuachana nae na ukaweza kuhandle ilo utashindwaje kuhandle hili dogo.
hata hiivy ni kama ulifanya kumtmbua na kumheshim kama baba wa mtot ila kama hataki hata hiyo heshima mwache.
tafuta suluhu ya suala la mwanao kwenda shule, mpe moyo mwanao, nawe binafsi sahau kuhusu huyo babae.
 
Pole sana kwa matatizo dada yangu..
Nyote naona mmechangia kwenye hili tatizo.
kwanza ulitakuwa kumjulisha ex mumeo kuwa umejaza namba zake kwenye form za shule ya mtoto.kwa kufanya hivyo msingefikia hapo.
Pia hata kama mmeachana mlitakiwa kukaa chini na kujipanga namna ya kulea watoto...ina kwa kuendekeza ugomvi wenu mmemuumiza mtoto na kakosa fursa ya kwenda shule...nyie mna akili gani...nadhani utakuwa umemweleza mwanao ukweli ndio maana umesema amejua ana amekosa amani...sio yote twawaeleza watoto..
Fanyeni yote ila watoto wasiwe wahanga na 'utoto' wenu.
Tafakari chukua hatua...

Namuhunga mkono mwnzangu ametumia busara sana na hakuhuma huma maneno, yaani inaonyesha kwa uwazi kabisa kwamba Mama na Baba wanafanya mambo ya kitoto sana: Wewe hata kama umehachana na mumeo kwa nini usiwe na heshima kidogo ya kutoa taharifa kwa mwenzako kuhusu uhandikishaji wa mtoto wako - inavyo onyesha nadhani labda huyo baba hatohi matunzo kwa mtoto wake huyo, kwa hiyo na wewe hukahamuwa kwamba hakuna haja ya kumfahamisha - hilo ni kosa, hiyo mimba haikuingia ndani ya tumbo lako kutokana na kasi ya upepo! ulishirikiana na mwenzio ndiyo kapatika huyo mtoto, sasa magomvi yenu yasi-tricle down mpaka yaka-involve watoto wenu - we mpe taharifa mwenzio hata kama atapuuzia lakini wajibu utakuwa umeutimiza msiwe munawachukulia watu mlio zaa nao for a RIDE they matter a lot BEWARE.

Tukija kwa mtaraka wako, naye anaonekana kufanya kitendo cha kitoto sana, yeye kama mwanaume angemezea na kumuacha mtoto wake aendelee na shule, kitu ambacho angefanya ni kukufuta wewe hili umweleze ni kwa nini unamuandikisha mtoto shule bila ya kumpa taharifa, lakini siyo hii cowboy tactic aliyo tumia kuwezesha mtoto wake aliye mzaa kutimuliwa shule! huo ni ukatili husiyo kifani na ni wanaume wachache wenye hulka kama hizo za kishetani. yaani kwa mawazo yake finyu anaona kufanya hivyo ni njia ya kuku-teach a lesson mzazi mwenzake in other words getting even - ni matatizo ya kisaikolojia. Kaeni chini muyamalize kwa manufaa ya watoto wenu, siyo lazima kurudiana, na wewe mama huwe unahakikisha watoto wanakwenda kumtembelea mara kwa mara baba yao, na husiwajengee watoto wako imani mbaya kwamba baba yao hawapendi au hawajali hata kama anafanya hivyo wewe hayo husiwaeleze.
 
Vin D, Baba alikuwa anaelewa kila kitu, hata mtoto alipofaulu nilimweleza, ila nadhani yeye ndio anaamua kumwumiza mwanae kupitia mimi akijua ananikomoa mimi, suala la mtoto kujua alifatilia mwenyewe pale msimbazi na kuambiwa hivyo baada ya kuona mimi namchenga kumwambia ukweli, tatizo hapo sio utoto tunatofautiana uelewa
Huwezi kupata ushauri wa tija hadi hapo X wako atakapotoa maelezo yake kuhusu kadhia hiyo na mazingira ya kutengana kwenu na mapatano ya kuishi na kuhudumia watoto baada ya kutengana....inawezekana ulishamkandia kuwa hata huyo mtoto hakuwa wake (biological father) bali alisaidiwa na mwingine..or similar provocations
 
Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.

Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.

Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.

Asanteni nakaribisha ushauri wenu
Pole lakini wewe ndio uliemnyima amani huyo mtoto, kilichokufanya ujipendekeze kwahuyo baba nini mpaka uweke namba yake ya simu kwenye hiyo fumu? Kwanini usingeweka namba yako'hayo ndio madhara yakufatafata wanaume ambao mlishaachana nao
 
pole sana. Tumia hilo kama fundisho, wakati mwingine usiandike namba ya huyo baba mtoto. andika details zako mwenyewe

Andika single parent, baba yake kafa! Or andika ya uncle wake kama yupo i.e ndugu yako wa kiume by the way ndo ndugu zake halisi baba can be anyone.
 
Mara nyingine huwa sielewi tunakuwaje sie akina mama.... unajua kabisa ribwana rako harina akiri, mnashindana kuonyeshana ubabe, halafu, bado unatoa mwanya kwa hayo mauza uza kuwafikia watoto.... hapo ndipo sikuelewi. Kwani wewe huwezi kulea mwenyewe ukae kimya hadi awe tayari mwenyewe kuwafuatilia? Sikukuelewa kabisa, kabisa kwa nini uliweka namba zake za simu shuleni. Unajidai unamwaga mboga, yeye anavuta sahani ya ugali anamwaga anakojolea hata kuwapa mbwa haiwezekani. Nani anakuwa amekomeshwa hapo? Please weka watoto mbali na hizo game zenu... I hate it! Nimepita huko na sikutoa hiyo ruhusa.

Nimechekajeeeeeee! Dah! ndo maana nisipopita JF a day nahisi kuumwa,
 
Huwezi kupata ushauri wa tija hadi hapo X wako atakapotoa maelezo yake kuhusu kadhia hiyo na mazingira ya kutengana kwenu na mapatano ya kuishi na kuhudumia watoto baada ya kutengana....inawezekana ulishamkandia kuwa hata huyo mtoto hakuwa wake (biological father) bali alisaidiwa na mwingine..or similar provocations

yaani hata mimi nimejaribu kujiuliza huyu mwanaume kwanini afanye hivi sikupata jibu, lakini kwa hiyo bolded in RED, inawezekana kabisa, lakini hata hivyo jamaa amefanya mbaya sana kwa kijana, na mama alitakiwa kwa hali yoyote ile ajitahidi huyu mtoto asijue kilichotokea. Sasa kwa kuwa imeshatokea, ajitahidi kumwelewesha na amtafutie shule nyingine, na kama inawezekana ajaribu kufuatilia ile shule inawezekana kabisa wamweke kwenye reserve kwakuwa alifaulu, akiwaeleza issue nzima wanaweza mpa nafasi ya wale watakaoshindwa kuja au kulipa!
 
unajua kaka mi siamini kama kweli huyu mama ndiye mwenye watoto wakubwa hivi alafu anajicontradict kama mtoto. Sasa ukawachukua kwa kujitia unaweza kuwa somesha alafu ukaandika namba za baba ili nini? Wewe huna simu? Au bado unajigonga kwake ile hali umeshabwagwa? Nonsense

Acha bange wewe manake naona unakurupuka tu!! Hayo unayoyauliza yameshaelezewa! Uwe unasoma kwanza comments kabla hujaja kututimulia vumbi hapa sio lazima ujiforce kudadisi, huwezi waachie wanaojua!! Una undugu na huyo baba wa mtoto, au we ndo baba mwenyewe?? Manake umeng'ang'ania kubwagwa tu!!
 
Back
Top Bottom