Wapenzi wa Magari ya Audi: Kuanzia mwaka 2025 Audi A4 hatunazo tena, zimekua replaced na Audi A5!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Tumetoka mbali sana na Audi A4, kuanzia mwaka 1994 na hatimaye tumefika mwisho wake baada ya miaka 30.

Hadi sasa tumekua na jumla ya generations tano za A4, kuanzia B5 ya mwaka 1994 hadi B9 ya 2015.
1st Gen B5

2nd Gen B6

3rd Gen B7

4th Gen B8

5th Gen B9


Ni moja ya gari nilizowahi zielewa sana, na nilikua na kiutata kununua kati ya A4, BMW 3 series au C Class.

Sasa kuanzia generation ya 2025, Audi A4 zimekua terminated na kuungana na Audi A5 kuanzia model ya B10.

Audi A5 ya kuanzia 2026 (ambayo ndio new generation ya A4 ya zamani, usimix na A5 ya 2007-2024) itakuja na engine za kuanzia cc 2000 hadi 3000 za kawaida na hybrid.

Hybrids ndio ziko interesting, zina battery ya 25 kWh na zinauwezo wa kutembea 70+ km kwa umeme tu.

Audi wamephaseout magari mengi sana hiki kipindi, ata kipenzi cha wadada Audi TT nayo imetoka kwenye game tokea 2024.

Supercar yao Audi R8 my dream car nayo chali.

Pia Audi A1 na Q1 nazo pia zimetoka.


Mabadiriko makubwa haya yanatokana na sababu nyingi ila kubwa zaidi ikiwa ni kuamia kwenye EV, pia kupunguza models zenye mauzo madogo mfano A1 na Q1 na pia kupunguza production costs mfano kuunganisha A4 na A5 ili kua gari moja.

All in all kila lakheri Audi.
 
Audi sijazielewa bado. Labda sijazijaribu.

Nina jirani yangu anapenda sana Audi.

Ila nilivyochukua BMW X5 aliishobokea sana, sijakaa sawa nikachukua MB GLE 450 alizima fegi.
Kwa ujerumani naonaga BMW na Benz kwanza, Audi namuwekaga mbali sana.

Mfano GLE na CX5 ukizifananisha na Q5 za Audi unaona kabisa gepu kubwa.
 
Naiheshimu Q7 TDI saana.... naifahamu moja jamaa kakaa nayo karibu mwaka wa 15 huu ila gari bado kama imetengenezwa Jana.

Raha yake masafa marefu.

Sijui kwanini kila Audi 4 niliyokutana nayo inapiga kelele....hili lilinifanya nisizielewe Audi japo ni mpenzi mkubwa wa kampuni yake mama VW.
 
Mkuu mimi nimepiga deals mpaka Wall St. zinapochapishwa pesa za dunia usinichukukie poa kwa sababu tu tunakutana JF kila siku πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
πŸ˜…πŸ˜… Imebidi niulize maana hali ni tete, halafu zinazungumzwa fedha za maana..

BTW I respect you!
 
Nimeagiza BMW 750L ya 2016
 
Audi naona bado Sana dhidi ya BMW.
Kwangu Mimi naona Bora nitumie BMW kuliko Audi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…