Wapenzi wa Muziki Mzuri: Home Theatre ya Sony vs Soundbar ya Hisense

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu Mambo.

Nataka kununua kati ya Home Theater ya Sony DAV TZ 140 5.1 au Sound Bar ya Hisense HS 281 2.1

Zote mbili bei zinafanana approximately Tsh 450,000/= kila moja.



Sony Home Theatre hiyo hapo, Wat 320. Nimeona haina Bluetooth connectivity sijui itafaa?

Na Hapa chini ni Hisense Soundbar ina sub yake, ni Wat 200 jumla.



Matumizi makubwa ni kwaajili ya Movie, na Game, Music kidogo sana.

Shukrani.
 
kwa specification naona iyo sony home theatre iko njema kuliko sound bar ya hisense, kwa iyo sony kwa apo iko bora, watts 320 vs watt200, lakin pia sony ni channel 5. 1 vs channel 2.1, ila kwa matumizi uliyosema zote zinafaa, na kama hupend minyaya minyaya sebulen na unataka kua stylish, chukua hisense sound bar
 
Asante mkuu. Ngoja nifanye ivyo. Nilikua naogopa maana iyo Sony naona ni ya zamani kidogo lakini Hisense nadhani ni ya 2020 kuja juu.
 
Asante mkuu. Ngoja nifanye ivyo. Nilikua naogopa maana iyo Sony naona ni ya zamani kidogo lakini Hisense nadhani ni ya 2020 kuja juu.
kwa hiyo bajeti yako ya 450k nakusogezea pendekezo zuri zaidi toa hiyo hisense weka hii, Hiyo nimeitoa Kwenye app ya kariakoo Mall, Najua ukiingia town mwenyew utapata bei chini ya hapo, sikushauri kuhusu Hiyo Sony Ishapitwa na wakati vya kutosha bluetooth kitu muhimu sana kwenye hizi mambo.
 
Shukrani boss. Hiyo 2.1 itakua na surround effect nzuri kwa movies na game?
 
Unaweza kufanya maamuzi kwa kuzingatia haya yafuatayo :
Hiyo Sony ni ya kizamani ingawa ina real surround featues kwa kuwa ina 5.1 speaker configuration. Hiyo Hisense sound bar ingawa ni 2.1 channel ikimaanisha inategemea virtual surround na hivyo kuwa nyuma ya Sony upande wa movie lakini ina HDMI na optical na pia Bluetooth connretivity kwa hiyo kwa tv za kisasa utaenjoy zaidi .
Mimi ningechagua Soundbar
 
Utapata effects kupitia virtual surround. Hii ina maana kuna sauti utazisikia kutokea upande ambao hakuna spika. Soundbars zimetengenezwa zikiwa na uwezo wa kurusha sauti ukutani au darini (forward/upward firing)halafu inakufikia wewe ikitokea ukutani/darini . Kwa hiyo effects utazipata tatizo liko kwenye ubora wa sauti. Hakuna mbadala wa spika halisi unaoweza kukupa ubora wa juu wa sauti. Kwa hivyo 2.1 haiwezi kuwa sawa kabisa na 5.1. Lakini pia huwezi kufananisha movie experience unayopata kwenye 2..1 system na stereo. 2.1 ni bora sana.

Namimi nilikua na wasiwasi huo. Ninavyoelewa mimi huwezi kupata sorround sound effect kwa system ya 2.1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…