Wapenzi wa push-ups & squats

Mwili wangu umejaa uvivu kila siku nasema nianze mazoezi lakn naishia kusema tu bas
 
Hongereni sana wadau wote hapo juu kwa michango yenu mimi nikiri kwenu ni veteran wa mazoezi ,nilianza mazoezi hapo kwa wajeda ukonga nikiwa nimekuja kumwona shangazi yangu ,wajeda muda mwingi kwa michezo wa football,netball,na volleyball wanaanza na mazoezi ya viungo hivyo nami ikifika jioni nakwenda kujumuikanao mwanzoni ilikuwa ngumu kutokana na ushamba baada ya miezi miwili nilianza kuzoea mazoezi mengi baada ya mwaka nikawa naweza kuongoza mazoezi ndipo tunaanza kucheza ,jamani niwasihi tu mazoezi ni matamu sana ,ukiweza kupiga hizo push up kwa usahihi unaweza kukimbia mbio ndefu au fupi kuanzia pale morogoro,yaani msamvu mpaka mikese bila kuhema asanteni
 
Bwanawee mie nilianzaga hizo tizi, kuna mdau huku ali pigia debe sana tizi si nikaunga asee, matokeo yalikua mazuri sana sana changamoto kufika Novemba mwaka jana nikaumwa ugonjwa kama uchovu fulani hivi...nikasema ngoja nipone niendelee ikawa kimoja.
Kitambi kimerudi kwa mbaali.
 
Napenda mazoezi Ila push ups ilishanishinda siku nyingi Bora squats kidogo nafanyaga Ila sio sana
 
Napenda mazoezi Ila push ups ilishanishinda siku nyingi Bora squats kidogo nafanyaga Ila sio sana
Asee tuwe tunafanya wote, utanishawishi nirudi kwenye ubora.
 
Mimi sijui push up zilishanishinda kabisa naweza kufanya mazoezi yote Ila push ups Sasa chineke ooooh
Ahahahaha wewe utapiga ukishindwa kunyanyuka nakunyanyua...teh!!
 
Baada ya kuona The Rock anapiga pushups 150 kwa siku nilianza...heheh nilipiga mia kwa siku kwa wiki nzima mpaka sasa katikati ya kifua nikiinama panalia kacha kama mfupa unajinyoosha ila hamna maumivu.
Kuna dawa au msaada wowote au ni kawaida kwenye mazoezi
 
Au ulizidisha kiwango mkuu? ila utakua poa usiwaze.
 
Mbona squatting nasikia ni za kujenga hips na viuno kwa kina dada, wanaume zinasaidia nini
 
Madhara ya push ups kwa wanawake ni zipi? Hasa anaepiga nyingi, je tumbo utengeneza six pack nk
 
Nina mwezi sasa sijapiga zoezi lolote..si cardio squart Wala push up zangu za ukutani

Mwili na akili havirelax hata kidogo..mazoea bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…