Wapenzi waliokutana jf na kubahatika kufunga ndoa /walioanza michakato ya ndoa

Siande

Senior Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
194
Reaction score
58
Kila nikisoma jukwaa hili najiuliza hivi kuna watu waliowahi kukutana tu jf wakafahamiana na baadae wakajuana na hata kufunga ndoa? sometimes naamini hii inawezekana lakini nataka watu waliopitia hapa waje watoe shuhuda zao na jinsi walivyokutana sina maana mbaya ila tu hii itasaidia wanajf wengine kuliamini jukwaa hili na pia kwa wale wanaobeza waweze kujua kuwa haya mambo yanawezekana. hata walioshuhudia ndoa hizo pia waje watoe ushuhuda

karibuni wadau kuchangia kama huna cha kuchangia pita tu kimya kwani wastaarabu wataleta busara zao hapa.
 
Hapa kuna wavuta bangi tu na wavuta sigara na waomba vocha. Na wala unga. Wengine wameoa na wengine kuolewa wakitaka kusaliti ndoa zao wanajifanya wanatafuta wachumba jf. Sijui lakini labda wapo walio bahatika humu ndani.
 
Kuna ukweli kabisa hapo nilipo bold..!
 
Mm nilim PM mmoja eti anataka nimtumie hela kwanza wakati wala hatujawahi kuonana ,je huo si wizi wakuu?
 
wapo sema wao wanataka ndoa fasta fasta wakati ujajua vizuri familia yake na yeye tabia yke
 
Hapa kuna wavuta bangi tu na wavuta sigara na waomba vocha. Na wala unga. Wengine wameoa na wengine kuolewa wakitaka kusaliti ndoa zao wanajifanya wanatafuta wachumba jf. Sijui lakini labda wapo walio bahatika humu ndani.

Umegonga mule mule kabisa.
Humu usipokuwa makini unaula wa chuya!!!
 
Kila nikisoma jukwaa hili najiuliza hivi kuna watu waliowahi kukutana tu jf wakafahamiana na baadae wakajuana na hata kufunga ndoa? sometimes naamini hii inawezekana lakini nataka watu waliopitia hapa waje watoe shuhuda zao na jinsi walivyokutana sina maana mbaya ila tu hii itasaidia wanajf wengine kuliamini jukwaa hili na pia kwa wale wanaobeza waweze kujua kuwa haya mambo yanawezekana. hata walioshuhudia ndoa hizo pia waje watoe ushuhuda

karibuni wadau kuchangia kama huna cha kuchangia pita tu kimya kwani wastaarabu wataleta busara zao hapa.

Toa mkwanja mtu aje afunguke,elfu 60,000 tu anasema story yake ni hati miliki sio ya kushare bure
 
Duh... Una ushahidi au ndo zenu waswahili ooh.. yule demu malaya ukiulizwa umemmega.? unaanza oooh c una mcheki mambo yake... Longolongo tupe ushahidi kiongozi..
Weewe!
Hapa kuna member wameoana!
Wengine wameibiana!
Wengine wanabanduana then wanakuja kupakaziana hapa hapa jamvini!!!
.....
CHEZEA JF WEYEEE!
 
Yaani hadi uje kusaka mchumba humu,wewe maeneo unayoishi na kutembelea hakuna watu????
 
si ndo hapo wengine wana mapungufu mazingira wanayoish watu hawawataki au walishawachoka ndio wanakuja kutafuta huku
 
Mi hata nikipata demu humu siwezi kubali kumtangazia ndoa kirahisi rahisi tuuuuu. Maana kama anakuja humu basi ujanja wa mjini keshaujua na huenda huko anakoishi watu wanamjua tabia zake mbovu ndio maana kaja kuangalia hukua asikojulikana.
Kuwezekana inawezekana maaana kuna wanaume wengine wana roho ngumu when it comes to maswala ya ndoa.
 
SIANDE, tupo tuliofanikiwa. Mwaka jana niliandika uzi wa kutafuta mume na nimepata. Nimefunga ndoa tayari na tupo na furaha sana ni kama tulijuana siku nyingi. Nilijiuliza sana wakati naandika lakini Mungu ni mwema nipo na mume wangu na tunaelewana kuliko wale ambao nilishakuwa nao kwenye relation kwa muda mwingi bila mafanikio. Nakwambia kama unafanya jambo kwa nia njema, Mungu atakuongoza na utafanikiwa. Ila majaribu ni mengi sana yakupasa kuwa na hekima kubwa kutafuta mwenza kwenye social networks. Kwa yeyote mwenye nia njema na asikate tamaa.
 
Back
Top Bottom