Wapenzi waliokutana jf na kubahatika kufunga ndoa /walioanza michakato ya ndoa

Toa mkwanja mtu aje afunguke,elfu 60,000 tu anasema story yake ni hati miliki sio ya kushare bure

wengine hawa hapa

Mm nilim PM mmoja eti anataka nimtumie hela kwanza wakati wala hatujawahi kuonana ,je huo si wizi wakuu?

wanawake wengi wa jf wamkaaa kihela zaidi yani wewe mwanaume kazi yako kuw pm na kuwaalika dinnera lunch au mtoko wowte na kutuma hela ya vocha then kama kugongana siku moja mbili mmeshaachana
 
Kila nikisoma jukwaa hili najiuliza hivi kuna watu waliowahi kukutana tu jf wakafahamiana na baadae wakajuana na hata kufunga ndoa? sometimes naamini hii inawezekana lakini nataka watu waliopitia hapa waje watoe shuhuda zao na jinsi walivyokutana sina maana mbaya ila tu hii itasaidia wanajf wengine kuliamini jukwaa hili na pia kwa wale wanaobeza waweze kujua kuwa haya mambo yanawezekana. hata walioshuhudia ndoa hizo pia waje watoe ushuhuda

karibuni wadau kuchangia kama huna cha kuchangia pita tu kimya kwani wastaarabu wataleta busara zao hapa.

Even me nimempata mchumba wangu kipenzi kupitia hili jukwaa. Nashindwa kuelewa ni kwanini watu wengi hawaamini kama inawezekana kumpata mtu mwenye mapenzi ya dhati kupitia mitandaoni, na wakati hawo hawo tunaokutana nao kwenye mabasi, nyumba za ibada, michezoni au hata mitaani ndio hawo pia tunakutana nao mitandaoni.

Nadhani watu wengi wanapoona mtu umetoa thread yako humu ya kutafuta mchumba na baadhi ya members wanavyo respond kwa comments za kuvunja moyo na kukebehi wanadhani kwamba haiwezekani kumpata the right person. Ila wanatakiwa wafahamu kuwa unapotoa thread humu wengi wanaochangia ni JF registered members na ndio wengi wenye majibu ya kuvunja moyo, lakini pia kuna non-registered JF members ambao wapo serious na wana browse hizo thread na wanatafuta pia wachumba.

Ningependa nitoe ushauri kwa wanaotafuta wachumba humu, unapotoa thread yako basi ni vizuri ukaweka pia other private email addresses, ili hata wale ambao sio JF-registered members waweze kukutafuta. Natamka hivi kwakuwa hata msichana wangu niliebahatika kumpata hakuwa ni registered member humu bali aliona tu email yangu kwenye baadhi ya thread nilizotoa then akanitumia email.

Wakuu sio siri, naomba niseme mashaallah! Namshukuru Mungu sana kwakuwa niliempata nahisi ametimiza 99.99% ya sifa nilizokuwa nazihitaji kwa msichana awe nazo. Na mpaka sasa tupo kwenye relation inakaribia miezi kama sita sasa na tunakaribia kwenda kutambulishana kwa wazazi.

Alinipenda, akaniamini na kunipa moyo wake, pamoja na umasikini wangu na ukizingatia nilikuwa sina hata ajira ya maana kipindi wakati tulipokutana. Kiukweli nampenda sana na sitarajii kumuacha wala kumsaliti mke wangu mtarajiwa, nampenda sana.

Kwahiyo wazee ile dhana ya kudharau na kutoamini kuwa huwezi kumpata mke au Mume bora kupitia mitandaoni sometimes sio kweli, mimi naamini ukiwa makini na mkweli utampata tu atakaekufaa.
 
Mi kila nikitongoza napigwa chini
 
Baadhi ya Wanaume hapa love connect wapenzi wao wapo mikoani anaanzisha thread akimpata wa karibu yake anaanzisha mahusiano ili amalize hamu tu na si kingine.
 
Umegonga mule mule kabisa.
Humu usipokuwa makini unaula wa chuya!!!
Namshukuru Mungu mm nililenga sehemu ya ukweli kwa mdada mwenye uelewo na sasa nasubiri tu jibu nitangaze mchakato!Naomba dua zenu posa ikubaliwe.
DEMBA Mungu azidi kukujaza hekima zaidi na zaidi na insha allah uzidi barikiwa Maam!
 
Last edited by a moderator:
Even me nimempata mchumba wangu kipenzi kupitia hili jukwaa. Nashindwa kuelewa ni kwanini watu wengi hawaamini kama inawezekana kumpata mtu mwenye mapenzi ya dhati kupitia mitandaoni, na wakati hawo hawo tunaokutana nao kwenye mabasi, nyumba za ibada, michezoni au hata mitaani ndio hawo pia tunakutana nao mitandaoni.

Nadhani watu wengi wanapoona mtu umetoa thread yako humu ya kutafuta mchumba na baadhi ya members wanavyo respond kwa comments za kuvunja moyo na kukebehi wanadhani kwamba haiwezekani kumpata the right person. Ila wanatakiwa wafahamu kuwa unapotoa thread humu wengi wanaochangia ni JF registered members na ndio wengi wenye majibu ya kuvunja moyo, lakini pia kuna non-registered JF members ambao wapo serious na wana browse hizo thread na wanatafuta pia wachumba.

Ningependa nitoe ushauri kwa wanaotafuta wachumba humu, unapotoa thread yako basi ni vizuri ukaweka pia other private email addresses, ili hata wale ambao sio JF-registered members waweze kukutafuta. Natamka hivi kwakuwa hata msichana wangu niliebahatika kumpata hakuwa ni registered member humu bali aliona tu email yangu kwenye baadhi ya thread nilizotoa then akanitumia email.

Wakuu sio siri, naomba niseme mashaallah! Namshukuru Mungu sana kwakuwa niliempata nahisi ametimiza 99.99% ya sifa nilizokuwa nazihitaji kwa msichana awe nazo. Na mpaka sasa tupo kwenye relation inakaribia miezi kama sita sasa na tunakaribia kwenda kutambulishana kwa wazazi.

Alinipenda, akaniamini na kunipa moyo wake, pamoja na umasikini wangu na ukizingatia nilikuwa sina hata ajira ya maana kipindi wakati tulipokutana. Kiukweli nampenda sana na sitarajii kumuacha wala kumsaliti mke wangu mtarajiwa, nampenda sana.

Kwahiyo wazee ile dhana ya kudharau na kutoamini kuwa huwezi kumpata mke au Mume bora kupitia mitandaoni sometimes sio kweli, mimi naamini ukiwa makini na mkweli utampata tu atakaekufaa.

Mkuu ubarikiwe sana. Ngoja nikai-update thread yangu kwa kuweka email.
 
....Sina uhakika sana...lakini bado aina ya maisha tunayoishi....utamaduni wetu......imani zetu....ni vigumu sana kupata mke/mume kupitia mitandao ya kijamii.....wengi wetu tunaotafuta humu ni wale waliokosa sehemu fulani katika mahusiano yao na hivyo hujaribu kujazia kupitia mitandao hii ya kijamii.........
 
Back
Top Bottom