Even me nimempata mchumba wangu kipenzi kupitia hili jukwaa. Nashindwa kuelewa ni kwanini watu wengi hawaamini kama inawezekana kumpata mtu mwenye mapenzi ya dhati kupitia mitandaoni, na wakati hawo hawo tunaokutana nao kwenye mabasi, nyumba za ibada, michezoni au hata mitaani ndio hawo pia tunakutana nao mitandaoni.
Nadhani watu wengi wanapoona mtu umetoa thread yako humu ya kutafuta mchumba na baadhi ya members wanavyo respond kwa comments za kuvunja moyo na kukebehi wanadhani kwamba haiwezekani kumpata the right person. Ila wanatakiwa wafahamu kuwa unapotoa thread humu wengi wanaochangia ni JF registered members na ndio wengi wenye majibu ya kuvunja moyo, lakini pia kuna non-registered JF members ambao wapo serious na wana browse hizo thread na wanatafuta pia wachumba.
Ningependa nitoe ushauri kwa wanaotafuta wachumba humu, unapotoa thread yako basi ni vizuri ukaweka pia other private email addresses, ili hata wale ambao sio JF-registered members waweze kukutafuta. Natamka hivi kwakuwa hata msichana wangu niliebahatika kumpata hakuwa ni registered member humu bali aliona tu email yangu kwenye baadhi ya thread nilizotoa then akanitumia email.
Wakuu sio siri, naomba niseme mashaallah! Namshukuru Mungu sana kwakuwa niliempata nahisi ametimiza 99.99% ya sifa nilizokuwa nazihitaji kwa msichana awe nazo. Na mpaka sasa tupo kwenye relation inakaribia miezi kama sita sasa na tunakaribia kwenda kutambulishana kwa wazazi.
Alinipenda, akaniamini na kunipa moyo wake, pamoja na umasikini wangu na ukizingatia nilikuwa sina hata ajira ya maana kipindi wakati tulipokutana. Kiukweli nampenda sana na sitarajii kumuacha wala kumsaliti mke wangu mtarajiwa, nampenda sana.
Kwahiyo wazee ile dhana ya kudharau na kutoamini kuwa huwezi kumpata mke au Mume bora kupitia mitandaoni sometimes sio kweli, mimi naamini ukiwa makini na mkweli utampata tu atakaekufaa.