Wapi bora kuwekeza: Fixed rate, BOT Bond, UTT?

Niliangaika humu na 100m kutaka ushauri niiwekeze wapi risk free
Nikaishia kuiweka Fixed deposit Ac 8% kwa mwaka
Hapo nakula 660k kila mwezi

Lakini naona kama nawafaidisha sana wao aisee
uliweka bank gani?
 
Kuna mtu anapigwa na kitu kizito muda si mrefu.... .......... .........😁😁😁😁😁😁😁 tulia wazee wa kazi washaona fursa
 
Niliangaika humu na 100m kutaka ushauri niiwekeze wapi risk free
Nikaishia kuiweka Fixed deposit Ac 8% kwa mwaka
Hapo nakula 660k kila mwezi

Lakini naona kama nawafaidisha sana wao aisee
Ina maana hukupata ushauri wa kuweka BoT ? Kwa hiyo 100m ungeweka kwa miaka 20 au 25 ungekuwa unapata 1.3 kwa mwezi ambayo ingelipwa semi annually. Ila hiyo ilikuwa ni kabla hawajashusha rate kutoka 15.49 % hadi 12% from last three weeks ago.
 
Kwenye Bonds sasa hivi wameshusha rates hivyo uwekezaji wake unaweza ukawa sawa na UTT AMIS kwenye Bond Fund. Kama UTT nao hawatashusha rates basi uwekazaji mzuri ni kupitia wao kwasababu kutakuwa na flexibilities. Unaweza kutoa hela yako muda wowote unlike BOT ambapo unaifungia kwa kipindi cha miaka 5, 10, 15, 20 na 25 na ulitaka kuuza kabla ya hapo ni through secondary market. Kwenye secondary market huuzi tu ni mpaka mteja apatikane.
 
Masharti yao ya kuweka miaka mingi yalinishinda mkuu
Huku unaweza kwenda nao hata miezi 6
Na pia wanakulipa kwa mwezi badala ya kusubiri kwa mwaka au miezi 6

Halafu nipo mkoani huku hata bank niliotumia ni hizi local bank zetu akina crdb rate zao mbovu
Lakini angalau hela ipo safe for now
 
Niliangaika humu na 100m kutaka ushauri niiwekeze wapi risk free
Nikaishia kuiweka Fixed deposit Ac 8% kwa mwaka
Hapo nakula 660k kila mwezi

Lakini naona kama nawafaidisha sana wao aisee
Mkuu si wanasema utt amis...bond fund au liquid fund ni nzuri kuliko hizo fixed account offered by commercial banks...? Fuatilia upande huu...! Kwa 100m...unapata about 10m kwa mwaka.
 
Sikushauri utumie hizi local bank kama nikiotumia mimi mkuu rate zao ndogo sana
Kama upo Dar tumia bank za kimataifa kama Barclays and the likes wana rate nzuri sana
Laki 6+ kwa mwezi kwa kuwekeza mil. 100 ni fedha kidogo hasa ukitilia maanani sh ya Bongo inavyoanguka na vitu kupanda bei kila kukicha. Hapo mwaka mmoja umepata kwenye mil 8 hivi kwa makadirio. Biashara kichaa hii ila ni njia nzuri ya kuhifadhi fedha zako wakati unatafuta cha kufanya. Angalau baada ya mwaka uwe umeshapata cha kufanya.
 
Sijakuelewa kabisa mkuu, tafadhali naomba uweke maelezo kidogo!
Unajua D 9? nilipoteza shilingi milioni 4 plus. Tuache hilo. Kuhusu BOT Kuna aina mbili za kuwekeza pesa Moja ni security bonds (bond ya muda mfupi) na Treasury bonds (bonds za muda mrefu). Hii Treasury bonds ukiwekeza mfano kwa miaka 15 unapata riba ya zaidi ya asilimia 12. Na wanalipa mara mbili kwa mwaka. Yaani mwezi wa sita na wa 12. Utalipwa hiyo pesa kwa kipindi chote cha miaka 15. Hiyo miaka ikiisha principal ipo pale pale. Ni stress free.
 
Mkuu,

kurekebisha kidogo tu hapo mwishoni, malipo sawa ni kila miezi sita, ila sio lazima iwe Juni na December. Iwapo kwa mfano umenunua bonds April, malipo ni kila April na October, na kadhalika.
 
Kwenye Bonds sasa hivi wameshusha rates hivyo uwekezaji wake unaweza ukawa sawa na UTT AMIS kwenye Bond Fund. Kama UTT nao hawatashusha rates basi uwekazaji mzuri ni kupitia wao kwasababu kutakuwa na flexibilities. Unaweza kutoa hela yako muda wowote unlike BOT ambapo unaifungia kwa kipindi cha miaka 5, 10, 15, 20 na 25 na ulitaka kuuza kabla ya hapo ni through secondary market. Kwenye secondary market huuzi tu ni mpaka mteja apatikane.
hao UTT AMIS wanakusanya ela za watu, wanaenda kununua bonds BOT.
 
Back
Top Bottom