Wapi Hidaya wa Pepe Kalle?

Nasikia katika usachana/ujana wake alikuwa Moto was kuotea mbali with pure stunning, undisputed and eye catching beauty. Hadi uzeeni bado alitisha kwa uzuri.

Dhahabu zilikuwa zimetanda mwilin mwake. Alipanda hewani, figure ilikuwa ya hatari Na Sura ya kuvutia. Si mwengine Ni Hidaya ambaye Pepe Kale alimuimba katika kibao chake matata akiwashirisha Akina nyboma.

Jamii Forums hapashindiki Jambo. Yeyote mwenye picha za the Cleopatra was Bongo atutupie humu. Nifurahi Sana kuziona.
 
Miaka ya mwanzoni mwa 2000 alikuwa mjasiriamali Kungwi!
 
Hahahah mhenga upo?
 
hidaya yupo hai,aliefaliki ni bint yake,kuhusu picha yake pitia instagram page ya yule bint aneitwa mange kimambi ameweka picha ya hidaya na ameeleza kwa ufasaha habari ya kifo cha bint yake na picha ya hidaya pia ipo,nimeshindwa kuweka picha...ushamba mzigo

Hidaya bint mohamedi bado yu hai anazeeka ila uzuri wa muonekano upo palepale..

kuna wanaosema kuwa hidaya alimpa pesa Pepe kale(empire bakuba) ili amtungie nyimbo kama alivofanya Abbas Guramali wa yanga aliempa pesa Pepe ili atunge kile kibao cha young african,hapana huyu hakumpa pesa ila alikuwa ni mpenzi/mchepuko wake huyu mama alikuwa tajili kias kwamba pepe alipokuwa bongo ghalama zote alisimamia huyu mama wakat ule akiwa ndiye mwanamama tajili aliefahamika pale arusha/mwenge akimiliki bonge la toyota pajelo

Pepe kale kwa mapenzi yake akaamua kumtungia wimbo huu wa hidaya alipofika kwao Zaire(Congo DRC),na kabla ya kufa alitimiza ahadi yake ya kusema ataludi maana nakumbuka alikuja kupiga show mwanza na hidaya alihudhulia na alimtuza zawadi flan nimeisahau ila haikuwa pesa,alipotoka mwanza alikuja moro na wakat huo na mimi nilikuwa morogoro hivyo nilifanikiwa kuhudhulia ile show na ndio ikawa mala ya mwisho kumuona The Grand Pepe kale live maana haikupita muda umauti ukamfika.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…