Wapi Hidaya wa Pepe Kalle?

Wapi Hidaya wa Pepe Kalle?

IMG_4906.JPG
hidaya last post iyo apo 4 days ago kweny page yake ya insta
 
Kwenye Instagram ya Mange J Kimambi leo amepost kuwa mtoto wa kike wa Hidaya ameuwawa leo huko Uingereza
 
hidaya yupo hai,aliefaliki ni bint yake,kuhusu picha yake pitia instagram page ya yule bint aneitwa mange kimambi ameweka picha ya hidaya na ameeleza kwa ufasaha habari ya kifo cha bint yake na picha ya hidaya pia ipo,nimeshindwa kuweka picha...ushamba mzigo

Hidaya bint mohamedi bado yu hai anazeeka ila uzuri wa muonekano upo palepale..

kuna wanaosema kuwa hidaya alimpa pesa Pepe kale(empire bakuba) ili amtungie nyimbo kama alivofanya Abbas Guramali wa yanga aliempa pesa Pepe ili atunge kile kibao cha young african,hapana huyu hakumpa pesa ila alikuwa ni mpenzi/mchepuko wake huyu mama alikuwa tajili kias kwamba pepe alipokuwa bongo ghalama zote alisimamia huyu mama wakat ule akiwa ndiye mwanamama tajili aliefahamika pale arusha/mwenge akimiliki bonge la toyota pajelo

Pepe kale kwa mapenzi yake akaamua kumtungia wimbo huu wa hidaya alipofika kwao Zaire(Congo DRC),na kabla ya kufa alitimiza ahadi yake ya kusema ataludi maana nakumbuka alikuja kupiga show mwanza na hidaya alihudhulia na alimtuza zawadi flan nimeisahau ila haikuwa pesa,alipotoka mwanza alikuja moro na wakat huo na mimi nilikuwa morogoro hivyo nilifanikiwa kuhudhulia ile show na ndio ikawa mala ya mwisho kumuona The Grand Pepe kale live maana haikupita muda umauti ukamfika.......
Toyota pajelo!!! Haya bana!
 
Nasikia katika usachana/ujana wake alikuwa Moto was kuotea mbali with pure stunning, undisputed and eye catching beauty. Hadi uzeeni bado alitisha kwa uzuri.

Dhahabu zilikuwa zimetanda mwilin mwake. Alipanda hewani, figure ilikuwa ya hatari Na Sura ya kuvutia. Si mwengine Ni Hidaya ambaye Pepe Kale alimuimba katika kibao chake matata akiwashirisha Akina nyboma.

Jamii Forums hapashindiki Jambo. Yeyote mwenye picha za the Cleopatra was Bongo atutupie humu. Nifurahi Sana kuziona.

Yupo hai bado
 
Yupo hai nineona kwenye acc yake ya instagram

Ndio ambae mwanae kauawa huko ulaya
 
Watu waongo jmn
Wakazusha amefariki kumbe mzima wa afya
 
Hidaya kwa sasa anaishi Dar, wala hana watoto wengine wa kiume, yupo na bint mmoja tu aliemzaa kabla ya kuwa na pepe kale, huyu binti ana mtoto wa kiume, Hidaya ana mjukuu wa kiume.
Na kwa bahati mbaya huyo mwanae Hidaya anaeitwa Leila, juzi amchomwa kisu na mumewe na kufariki dunia, huko nchini Uingereza walipo kuwa wanaishi na mwanaume pia ni Mtanzania.
 
Kwa wanaJF wakongwe hasa wale walioishi Arusha wanaweza kumkumbuka mwanamama HIDAYA (mwanamke wa kwanza kumiliki Toyota pajero ndani ya jiji la Arusha) aliyeimbwa na jitu la miraba minne PEPE KALE.

Naomba kwa wale wanaojua yuko wapi watujuze. I miss her so much!
Hidaya naskia yupo Dar kwa sasa, na kwa bahati mbaya umemkumbuka na yeye amepata msiba mkubwa sana kwani mwanae kipenzi anaeitwa Leila, juzi amchomwa kisu na mumewe na kufariki dunia, huko nchini Uingereza walipo kuwa wanaishi. Na huyo mume pia ni Mtanzania. Picha ya Marehemu Leila mtoto wa Idaya Pepe kale, na huyo jamaa ndio mume wake ambae amemchoma kisu.
IMG-20180330-WA0035.jpg
 
Hidaya naskia yupo Dar kwa sasa, na kwa bahati mbaya umemkumbuka na yeye amepata msiba mkubwa sana kwani mwanae kipenzi anaeitwa Leila, juzi amchomwa kisu na mumewe na kufariki dunia, huko nchini Uingereza walipo kuwa wanaishi. Na huyo mume pia ni Mtanzania. Picha ya Marehemu Leila mtoto wa Idaya Pepe kale, na huyo jamaa ndio mume wake ambae amemchoma kisu.View attachment 731371
Duh, huko kwa wenzetu huyo jamaa ni straight anaenda kunyea debe.

Angekua bongo walau angejificha kwenye kivuli cha Wasiojulikana.
 
Hidaya naskia yupo Dar kwa sasa, na kwa bahati mbaya umemkumbuka na yeye amepata msiba mkubwa sana kwani mwanae kipenzi anaeitwa Leila, juzi amchomwa kisu na mumewe na kufariki dunia, huko nchini Uingereza walipo kuwa wanaishi. Na huyo mume pia ni Mtanzania. Picha ya Marehemu Leila mtoto wa Idaya Pepe kale, na huyo jamaa ndio mume wake ambae amemchoma kisu.View attachment 731371
HUYO JAMAA MBWIGA SANA,UNAUA M/KE KWA AJILI YA KWENDA CLUB? YEYE AKIENDA CLUB NA WEWE SI UNATOKA UNAENDA CLUB TU KAMA MBWAI MBWAI,ONA SASA UNAENDA LUPANGO.
 
Back
Top Bottom