Wapi ilipo ndege ya Malaysia MH 370?

Wapi ilipo ndege ya Malaysia MH 370?

Mimi binafsi nililitilia shaka suala zima la ndege ya Malaysia kutoweka angani na isipatikane kokote kwenye uso wa dunia mpaka hivi leo, bado nalitia mashaka suala hilo kwamba halina ukweli wowote ndani yake, bali ni moja kati ya filamu zao nyingi wanazo ziigiza ilikuendelea kuulaghai umma, lakini zaidi mimi naona ni hayo ni

MAANDALIZI YA KUMTAFUTA ADUI MPYA ATAKAYE CHUKUA NAFASI YA ‘VITA DHIDI YA UGAIDI’.

Kwa kuanzia tu, tuitazame moja ya nambari kuu zinazo pendelewa kutumiwa kishetani na Illuminati, nambari 11.

Wakati ndege hiyo ya Malaysia ikipotea ndani yake kuliwa na abiria 227, nambari hiyo ni sawa na 2+2+7=11, ndege yenyewe ni Boeing 777 nambari inayogawika kwa 11.

Ndege hiyo ya Malaysia ilipatwa na ‘ugonjwa’ kama ule uliozipata ndege za 9/11 ambayo tunajua kuwa tukio lile lilifanywa na utawala wa Bush mwenyewe.

1. Ndege hiyo ya Malaysia ilipoteza mawasiliano kama zilivyokuwa ndege za 9/11. Masaa mawili baada ya ndege hiyo kuondoka ilipoteza mawasiliano kabisa na kitengo cha anga ambacho ndicho kilicho kuwa na dhamana ya kuiongoza ndege hiyo.

2. Ndege hiyo iliacha njia yake ya safari kama ilivyokuwa kwenye 9/11. Ndege hiyo ya Malaysia ikaendelea kusafiri maelfu ya maili nje ya njia yake iliyopaswa kupita bila hata ya kutuma taarifa za tahadhari na msaada kwenye kituo chochote cha kuongezea ndege na kisha ‘ikatoweka’ kama mazingaombwe vile.

3. Ndege hiyo ikapotea kabisa na isionekane kama zilivyo potea ndege iliyo gonga Pentagon na ile ya Pennsylvania kwenye tukio hilo la 9/11.

4. Kama ilivyokuwa kwenye 9/11, kwenye ndege ya Malaysia nako abiria simu zao zilikuwa hewani!!!!!

Kila mtu anajiuliza ni nini hicho? Ndugu na jamaa wa abiria kwenye ndege iliyo potea wamethibitisha kusikia milio ya simu walipojaribu kuwapigia wapendwa wao. Na pia baadhi ya kurasa za fecebook za abiria hao zimeonesha kuwa wapo ‘online'.

Shirika hilo la ndege la Malaysia limethibitisha pia simu ya mhudumu aliyekuwepo kwenye ndege hiyo nayo iliita tu bila kupokelewa na mtu yeyote mpaka ikakata kama zilivyo fanya simu 19 za abiria walio kuwepo kwenye ndege hiyo baada ya kupigia na ndugu na jamaa. Hayo yalisemwa na msemaji wa shirika hilo bwana Hugh Dunleavy.

Lakini pia hadithi ya simu za abiria na ile ya muhudumu kuita inatupatia mwanga wa jambo moja, kwamba ndege hiyo haipo ndani wala chini ya bahari! Simu haiwezi kuita kama ipo ndani ya maji, lakini zaidi simu hiyo lazima iwepo karibu na mnara wa simu, ambao tunajua hauwezi ukawepo chini ya bahari isipokuwa aridhini.

5. Kama ilivyokuwa kwenye 9/11 hapa napo kwenye ndege ya Malaysia mapema kabisa Illuminanti walianza kutoa dondoo za tukio zima takribani miaka minne kabla. Tizama picha hii inayofuata na linganisha na tukio lenyewe kisha kuna kichwa na kujiuliza ikiwa tangazo kwenye picha hiyo limetokea kwa bahati mbaya?

Tunapoendelea kulitolea macho suala hili, tunayo maswali ya msingi ya kujiuliza, kumbukua hapa tunazungumzia ndege kubwa aina ya Boeng, ndege ya kisasa kabisa, ndege hii haijalipuka, haijaanguka mahala kokote, si nchi kavu si baharini, imetoweka ghafla, narudia tena IMETOWEKA GHAFLA ikiwa angani, na haijapatikana mpaka hivi leo.

Vipi kama vile MUVI linajirudia ...?

Vipi wanataka kututengenezea Septemba 11 nyingine au?

Swali # 1

Ndege zote aina ya Boeing 777 zimetengenezwa pamoja na ‘Black Box’ ambayo inaweza kuhimili mlipuko wa aina yeyote ule utakaoipata ndege hizo. Kisanduku hicho kinabeba taarifa zote muhimu yakiwemo mawasiliano ya hatua kwa hatua tangi ndege inapotokea mpaka inapo elekea.

Swali linakuja NI VIPI KIBOKSI HICHO KIMESHINDWA KUTUELEKEZA WAPI NDEGE ILIPO?

Swali # 2

Black Box zote zinayo uwezo wa kuendelea kusafirisha mawasiliano na kutambua wapo kilipo hata kwa muda wa siku 30 hata kama ndege ikiwa imezama baharini.

Swali linakuja ni kitu gani hicho kilicho zima ‘signal’ ya kisanduku hicho kiasi kwamba shughuli za kuipata ndege hiyo zimekuwa ni ndoto. Tunajua ndege hiyo haijawaka moto wala kuzama baharini, sababu simu za abiria na wafanyakazi wa ndege zilikuwa zikiita kila zinapo pigwa. Sasa inakuwaje simu zinaweza kuendelea kuleta mawasiliano lakini kisanduku cheusi kipoteze mawasiliano kabisa?

Swali # 3

Ndege inapokuwa imepotelea baharini, mara zote kuna sehemu na mapande ya ndege hizo yataonekana yakielea baharini.

Kama ndege ya Malaysia ingekuwa imetungulia na kushushwa chini basi vipande lazima vingeonekana vikielea baharini, lakini viko wapi vipande hivyo? Ndege ya Boeing 777, imetoweka ghafla kwenye uso wa dunia, IMETOWEKA, ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.

Swali # 4

Mahala ambapo ndege hiyo ‘imepotelea’ panafahamika. Waongozaji wa ndege wanakuwa taarifa zote za ndege husika, kumbuka wao ndiyo waongozaji, hivyo nukta ambayo ndege inakata mawasiliano na wao wanakuwa wanafahamu ilikuwa eneo gani, ilikuwa kwenye mwendo kasi wa aina gani, vyote hivyo vinaweza kutumika kuelekeza ni wapi mapande ya ndege hiyo yanaweza kuwa yameangukia. Lakini ni vipi ndege hii ya Malaysia imeshindwa kupatikana chochote pamoja na kwamba inafahamika ni wapi nukta ya mwisho ilionekana kwenye rada?

Swali #5

Tuseme Ndege 370 ya Malaysia imetekwa, lakini ndege haipotei kwenye rada hata kama ikitekwa. Sasa inakuwaje ipotee hata kwenye rada isionekane?

Ndege nambari 370 ya Malaysia aina ya Boing 777 HAIJALIPUKA, HAIJANGUKA KOKOTE, ILA IMETOWEKA? KIVIPI??

Itaendelea....

View attachment 468866
Binafsi natamani chama cha ccm na wanachama wake wote wafutike kama hii ndege....
 
HII NI MARA YA PILI SASA UNAKOPI POSTI KUTOKA KWENYE BLOGI YANGU, "salim msangi" na kuviweka huku kwenye JAMII FORUM KAMA VILE WEWE NDIYE ORIGINATOR WA THEMES/TOPIC/POST.
TAFADHALIA ZINGATIA SHERIA YA MITANDAO NA SHERIA YA HABARI. TAFADHALI KABLA YA KUFANYA TENA HIVYO AU KUEDNELEA KUKOPI NA KUPOSTI KUTOKA KWENYE BLOGI NILIYOITAJA HAPO JUU, WASILIANA NA MIMI KWA NJIA YEYOTE ILE INAYOWEZEKANA, VINGINEVYO SHERIA ITAFUATA MKONDO WAKE.
KENGO LA KUFANYA HIVI NI KUILINDA KAZI YANGU. WADAU WAMEULIZA MASWALI NA WAMECRITISIZE ULICHOKIPOSTI HAPA LAKINI SI DHANI KAMA UTAWEZA KUYAJIBU AU KUWAELEWESHA, SABABU WEWE SIYO ORIGINATOR WA MADA HUSIKA, TAFADHALI, WASILIANA NA MIMI KABLA YA KUENDELEA NA UTARATIBU HUU.
akha! kumbe we ndo salim msangi.?!!
 
hiyo hesabu kama ingekuwa inatumika kuhesabu pesa.sizani kama hata bando ya internet ungekuwa nayo.na mambo hayo
 
cia wanajua kila kitu..kuhusu hiyo ndege....tusubiri baada ya miaka 50 watakapo chapisha top secret operation zao walizozifanya kwa kipindi cha miaka 50 nyuma.....kama ilivyo taratibu zao....nadhani na hiyo itaelezwa kwa kina...
in sha allah tuombe uhai mrefu na afya njema.....
 
it landed in antarctica and is located in a deep underground nazi base
 
Anaye weka habari hapa anabeba dhamana ya habari hiyo, endapo habari hiyo itasababisha lolote baya au zuri kwa mtu, taasisi, au kikundi cha watu au nchi kwa ujumla wake, aliweka habari hapa anakuwa ndiyo wa kwanza kuwajibika na habari hiyo. Hivyo unaposema inaweka habari zote, hii siyo mtu mwenye utashi bali ni chombo, muwekaji wa habari ni wewe na mimi, ndiyo maana kuna sheria ya habari, sheria ya hati miliki ya habari, ambazo zina lengo la kumlinda na kuuongaza mtoa habari kulingana na taratibu za jambo hilo. Unavyo weka habari ambayo si yako lazima utanabaishe wazi kuanzia mwanzo kuwa habari hii ni kwa mujibu wa "-----" ili likitokea la kutokea inajulikana chanzo cha habari hiyo ni ipi, lakini si kujifanya ni yakwako halafu ukibanwa ndiyo unaanza oooh! mimi niliikuta tu, sijui mimi .... acha hizo. kama umeikubali kazi yangu just simple niandikie kwenye email kuwa naomba niwe na post kazi zako mahala fulani, na mimi nitakupa utaratibu wa kufanya hivyo.
Mkuu

Mara nyingi habari huwekwa vyanzo chake, jamii Forum inajitegemea, tuna okota okota tu
 
Mtoa post usiwe mjinga

Wabongo tumezidi kuamini uchawi na mambo ya freemason ndio maana hatuendelei

Hiyo ndege ni kuwa inawezekana ilivyopoteza mawasisiano iliendelea kuwa hewani hadi pale marubani walipoona mafuta yameisha wakaamua kutua kama ile ndege ya american airline

ilivyotua kwenye maji na watu wote wakapona

So Inawezekana marubani akili yao ilikuwa ni kutua ikiwezekana ielee kwenye maji hadi hapo msaada utakapopatikana

Hivyo inawezekana walifanikiwa kutua juu ya maji bila ndege kulipuka au kugawanyika hivyo ikaanza kuzama mdogo mgogo hadi chini ya bahari


Alafu usijidanganye kuwa kila mawasiliano yanategemea minara, Hapana, kuna baadhi ya makampuni yanatumia satellite kama signal yao kuu ya mawasiliano hivyo kama ndege ilikuwa ishazama na bado maji yalikuwa hajaingia ndani si kitu cha kushangaza kama sim bado zilikuwa zinaita

Kama curiosity iliyopo sayari ya marz ipo umbali wa mabilioni ya km kutoka duniani na bado inadetect mawasiliano pamoja na satelite iliyopo duniani basi sio kitu cha kushangaza sim iliyo chini ya bahari kudetect mawasiliano


Na ukitaka kujua hii ndege kweli ipo chini ya bahari ni yale baadhi ya masalia ya mbawa zake yaliopatikana kandokando ya bahari mwaka uliopita. Kampuni ya Boeing ilithibitisha kuwa yale mabaki ambayo ni vipande vidogo vilivyochomoka kwenye mbawa ni mabaki ya MH 370

Daaah
Hadi huku umo!!!

Umemjibu ki intellectual sana. Tukutane central kwa makonda nikutoe lunch nikitoka kuhojiwa
 
Kuna kitu kinaitwa Bermuda Triangle.

Ndege au meli ikijikoroga ikakatisha hapo itajikuta ipo sayari ya jua au kokote kule.
 
Mi naamini dunia ina mwisho wake na huko ikifika basi inaingia ktk sayari(galaxy)nyingine.Pia si ajabu abiria wapo katika sayari nyingine maisha yanaendelea
 
Mi naamini dunia ina mwisho wake na huko ikifika basi inaingia ktk sayari(galaxy)nyingine.Pia si ajabu abiria wapo katika sayari nyingine maisha yanaendelea
Hahaha
Ukute wako sayari.nyingine wana kula bata tu.
[emoji23]
 
Ila sio mbaya maana nisingeijua blog yako kama sio wewe kucomment katika hiyo post ya Hugo jamaa,samehe bure hiyo mutu
Haina shida yeye ku-copy na kupaste kama mwisho au mwanzo wa hiyo kazi ataknowldge mwenye kazi hiyo ni nani na ikibidi kuweka link ya kuwaelekeza wengine watakao taka mada kwa pana zaidi, kama unavyoona amekopi sehemu ndogo, kisha akandika itaendelea, ikiwa na maana kuwa yeye ndiye hasa mwenye usukani, kumbe kaiba kazi ya mtu. Hiyo blogi inaposti zaidi ya 100 zenye maudhui mbalimbali yeye kwa kukiri kuwa si kazi yake au kuweka link ya source itawafanya wengine wafaidike na mada zingine zilizopo kwenye hiyo blog, ila huo anao fanya ni wizi halafu tena ni mchoyo, kwamba chimbo lake likijulikana ujanja wake nao utakuwa kwishni.
 
Mkuu

Mara nyingi habari huwekwa vyanzo chake, jamii Forum inajitegemea, tuna okota okota tu
Ndugu sikatai kazi zangu kukopiwa na kusambazwa kwa wengine, nadhani hiyo ndiyo sababu ya mimi kuanzisha blogi, napingana na wewe pale unapokataa kukubali kazi si yako, pale unapobania hilo chimbo kwa wengine, we ukikopy weka link hapo chini kuwa huu mzigo nimeuvumbulia sehemu fulani, ndivyo tunavyo fanya hivyo, kwenye posti nyingi za hiyo blogi nimeonesha ni wapi nimetolea hizo data, sababu lengo ni kujenga maarifa kwa hoja mwingine yeyote anakuwa na nafasi nzuri ya kupinga au kuunga mkono hoja. Blohi yenyewe inayo posti zaidi ya 100 zenye maudhui tofauti tofauti, wewe umevutiwa na posti hii lakini ukiweka link mwenzako utakutana na nyingine inayomvutia, utanisaidia kufikisha ujumbe kwa wengi, na kunipa moyo wa kuendelea kuposti mada mpya.
Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom