Wapi kuna mashamba ya sh 150,000/= mkoani Njombe

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Habarini watu wa Njombe, nchi iliyosheheni "asali" na "maziwa"!

Mwanzoni mwa mwaka huu nilifanya ziara mkoani Njombe, ziara ambayo ilinifungua macho kuhusu "utajiri" uliopo Njombe.

Katika hiyo ziara, nilibaini kuwa mashamba si ghali kwenye hiyo "nchi". Maeneo jirani na mijini ekari moja ni kama milioni moja na laki mbili, nje kidogo ya mji ni kama laki tano hivi, na vijijini mbali na mji (sikufika) nilimbiwa kuna "mashamba pori" yanayouzwa sh 150,000/= kwa ekari.

Wenyeji wangu walinionya nisiende kutafuta mashamba vijiji vya mbali kwa sababu barabara si nzuri ( lakini inapitika).

Mimi nimepalenga huko huko wanakodai hapafai. Patanifaa sana! Naamini ubovu wa barabara si wa kudumu.

Nimesahau majina ya hivyo vijiji, lakini nafikiri nauli ni kama shilingi elfu nne hadi nane kutokea Njombe mjini!

Mnaweza kunikumbisha majina ya hivyo vijiji?

Asanteni!!!
 
Ukishalima wanakuja kukuvunia bila ridhaa yako!

Ahsante
 
Ndugu ukifanikiwa nakuomba sana unijulishe na mimi tafadhali, huko mbali ndio kuzuri sasa.
 
Huwezi kupata kwa bei hiyo
 
Huwezi kupata kwa bei hiyo
Usiseme hivyo mkuu! Penye nia pana njia. Muhimu ni uvumilivu na kuwa na muda wa kutosha "kupeleleza"

Niliambiwa na zaidi ya watu wawili wa Njombe kuwa kuna "mapori" yanayouzwa shilingi laki moja na hamsini vijiji vya mbali. Walioniambia ni watu wa kuaminika, mmoja wao ni "bilionea" wa maparachichi.
 
Mashamba ya 150,000 ni uongo mashamba wastani ya huko ndani ndani sana ni laki 3-5 kuendelea hadi milioni tena maeneo ambayo wanamwagilia viazi mwaka mzima uko ata ugusi maana watu ni kiazi bandika bandua
Acha kukatisha watu tamaa
Mkoa wa pwani tu jirani kabisa na d as salaam hapa ukiwa na laki tano unapata shamba tena heka nzima
Huko unaposema inawezekana kuna maeneo unajifekea tu pori unaendelea na maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…