GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Habarini watu wa Njombe, nchi iliyosheheni "asali" na "maziwa"!
Mwanzoni mwa mwaka huu nilifanya ziara mkoani Njombe, ziara ambayo ilinifungua macho kuhusu "utajiri" uliopo Njombe.
Katika hiyo ziara, nilibaini kuwa mashamba si ghali kwenye hiyo "nchi". Maeneo jirani na mijini ekari moja ni kama milioni moja na laki mbili, nje kidogo ya mji ni kama laki tano hivi, na vijijini mbali na mji (sikufika) nilimbiwa kuna "mashamba pori" yanayouzwa sh 150,000/= kwa ekari.
Wenyeji wangu walinionya nisiende kutafuta mashamba vijiji vya mbali kwa sababu barabara si nzuri ( lakini inapitika).
Mimi nimepalenga huko huko wanakodai hapafai. Patanifaa sana! Naamini ubovu wa barabara si wa kudumu.
Nimesahau majina ya hivyo vijiji, lakini nafikiri nauli ni kama shilingi elfu nne hadi nane kutokea Njombe mjini!
Mnaweza kunikumbisha majina ya hivyo vijiji?
Asanteni!!!