Kuna watu mnapenda ubishi hadi basi (mimi nipo Nyave), kwa mwenye hela nimesema aende Nyave akalipie apige kazi. Kuamini sio lazima. Karibu tulime.
Watu waache kukariri! Shamba siyo sukari, halina bei elekezi. Kwa vile Hamisi kauziwa ekari 1 shilingi milioni moja hainilazimu na mimi kuuziwa kwa bei hiyo. Huyo aliyemwuzia Hamisi kwa bei hiyo anaweza akaniuzia mimi kwa shilingi laki moja. Inategemeana na uwezo wangu wa "kubargain".
Nina uzoefu kidogo katika hilo. Nimefikia hitimisho la kutokulipokea jibu la "haiwezekani" kama sijajiridhisha mwenyewe kwa "first hand experience".
Mwaka Juzi niliwaomba watu fulani wanitafutie mashamba ya bei rahisi mkoani Kigoma, hasa ambayo hayajawahi kulimwa(mapori) ili bei isizidi shili laki moja kwa ekari, lakini wengi wa wenyeji wangu waliniambia hakuna mashamba ya bei hiyo wilayani kwao. Waliniambia bei ya shamba huko ni kuanzia shilingi laki tatu mpaka sita kwa ekari.
Lakini miezi michache baadaye, mtu mmoja ninayemfahamu aliuziwa ardhi (pori) ekari 20 kwa shilingi milioni moja na laki sita, kwamba kila ekairi shilingi elfu themanini. Nilimwomba huyo aliyemwuzia anitafutie na mimi, tena safari hii, nilimwambia bei isizidi elfu hamsini kwa ekari.
Mwaka Jana alinipigia na kuniambia ana uhitaji wa milioni moja kama nipo tayari aniuzie ekari 20, kwamba kila eka shilingi elfu hamsini, lakini gharama za kuandikishana ziwe juu yangu. Nilimkubalia, na kwa shilingi milioni moja, nilipata shamba pori la ekari ishirini ingawa kwa vipimo vya GPS ni zaidi ya ekari 20.
Kama hiyo haitoshi, mwaka huu huyo mtu aliniambia aniongezee ekari 10 kwa bei ile ile ya sh 50,000/= kwa ekari. Sikutilia maanani hivyo muda ulipita bila kumpa jibu.
Kuelekea mwishoni mwa mwaka, alinipigia tena na kuniambia kuwa ameamua kunipunguzia bei hadi laki 4 kwa eka zote 10, ila gharama za kuandikishana nizibebe mimi. Maana yake kila eka shilingi elfu arobaini. Nilimkubalia, hivyo ndani ya wiki moja hilo eneo likawa langu. Kwa hiyo nikajikuta nimenunua zaidi ya ekari 30 kwa shilingi milioni moja na laki nne, nje ya gharama za uandikishaji ambazo hazizidi jumla ya shilingi laki mbili kwa eka zote thelethini.
Mwaka huu, kwenye mwezi wa nne hivi,nilisikia kuwa kule Kakonko katika kata ya Kasanda kuna maeneo yanauzwa na Serikali ya kijiji kwa bei rahisi. Nilienda huko hivi karibuni, na nilijutia kwa kutokuchukua hatua haraka.
Niliambiwa kuwa ni kweli kulikuwa na hilo zoezi lakini eneo lililokuwa lilmetengwa kwa ajili ya kuuzwa limeshaisha. Watu waliopata taarifa wameyawahi. Ekari moja ilikuwa ikiuzwa shilingi elfu ishirini. Kwa kila aliyenunua alipewa hati ya kimila. Japo yalikuwa ni mapori, ardhi yake ni nzuri sana. Udongo wake na hali ya hewa ilitaka kufanana na ya Njombe, japo si kama ya Njombe, lakini ina rutuba sana.
Mimi ninaamini hata Njombe naweza kupata "mashamba pori" kwa bei isyozidi shilingi laki moja kwa ekari, kwamba kwa shilingi million tano naweza kupata ekari zisizopungua hamsini.
Siyo kila mtu anaweza kuipata hiyo "bahati" lakini mimi naweza, ingawa siyo Sheria!