Wapi Misanya Bingi & Dena Amsi?

Wapi Misanya Bingi & Dena Amsi?

Pasco mwenye haki ya post zote za jf ni nani ? Kama mtu ameamua kuweka post mara moja moj akule na nyingine huko kuna tatizo gani si zake , ina maana wewe unajua members wote kwenye forum hii na kujua nani ni nani ? Mpaka kuingilia mambo ya watu ?
 
Ikimita, kama aliyehudhuria lectures asilimia 100% na kutoka ametoka na PASS na aliyehudhuria lectures 40% na katoka na 2nd, yupi kati ya atakuwa proud of himself/herself, hivi ningehudhuria kwa 100% si ningetoka na 1st?.

Wewe usiingie darasani halafu ukapasua, unayo sababu ya kusikitika, sasa sana utajijutia tuu kwa nini sikuingi darasani, kumbe ningeingia ningefanya even better!.

Kwa kujijutia hapo ndipo huzuni hufuata na kuishi kwa masoneko ninge jua, dawa ni kuridhika na ulicho kipata, wengine ni watu wa wastani tuu, nami ni mmoja wao, sio book worms, hata usome vipi, ukeshe, kama ni mtu wa wastani, ni mtu wa wastani tuu, hivyo its true I'm very proud kuwa mtu wa wastani kama nilivyokuwa proud kukaaa back bench tangu primary mpaka chuo!.

Elimu yetu wa-TZ hiyo!!! Unatamba kwa kuingia lecture hall kwa machale! Pole sana, ndo maana hata tukipambanishwa na wakenya tunatoka kapa tunabaki kulalama tu ooh kampuni hii inaupendeleo sijui kitu gani!! Ni maarifa gani uliyo nayo ya kupambanua mambo kama siyo unalingishia cheti cha daraja la juu wakati maarifa hola?

Kwa kweli utabaki na hicho cheti lakini mara nyingi kazini utakuwa unachemsha maana huna maarifa na ujuzi unaohitajika kazini wewe ulibaki kukazania kufaulu mitihani na siyo kupata maarifa! Pole sana na endelea kutamba na hiyo shahada yako!!
 
Mpeni sifa zake jamani pale anapostahili mie nimewahi kumchukua kuwa facilitator/mwezeshaji kwenye semina yangu alifanya vizuri sana.
 
Shy, asante kwa hili, kwa kweli niite mdogo wako, au hata mtoto wako kwenye forum kwa vile wewe humu ni miongoni mwa members waanzishili, ili hali mimi ni wakuja tuu.

Ila pia ni kweli, ninatia huruma, na nahitaji sana huruma yako, hivyo nakuomba sana, unihurumie mimi, na hao unaowachukulia mabandiko yao na kubandika kule kwako huku ukujifanya umeandika wewe.

Sina problem kabisa na freedom of information kwa information kuenea zaidi kwa kuonekana forums mbalimbali, lakini kuna element ya intalectual property ya originality, hii sio favour ni right, unawajibika siku zote, unapochukua kazi ya mtu, no matter how small or insignificant it is, lazima una attribute source, kwa kuandika tuu source:jf, basi, is is asking for too much brother/baba?.

Pasco:

Hapo bold umenena! Kila siku huwa najuliza kwa nini Shy anapenda sana "copy and paste" bila ku-acknowledge author(s)?

Nakumbuka kwenye 2005 ukisoma kwenye EthinkTank mojawapo ya email za Shy utabaki mdomo wazi! Lakini leo "he is the master of all trades" Shame!
 
Mpeni sifa zake jamani pale anapostahili mie nimewahi kumchukua kuwa facilitator/mwezeshaji kwenye semina yangu alifanya vizuri sana.

Hongera sana Misanya Bingi! Siku hizi mbona sikuoni mitaa ya "Kwa Mae"? Au Phd inabana sana?
 
Ni Lecturer sasa, Yupo School of Arts and Social Science, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

UDSM hakuna school of Arts & Social Science ni College of Arts and Social Science mkuu
 
Misanya Hongera sana kwa kutoka chini kwenda juu. Usijali na maneno ya watu.
 
Yuko UD. Radio one walimbania akaamua kwenda shule. Hakwenda kwa kupenda. So wakati mwingine mtu akikubania kwenye sehemu moja sometimes anakuwa anakupa fursa nyingine na Bam! ukiitumia unatoka. Big up Bingizz.
 
Huyu jamaa nasikia alipata ajira kwa ukaribu aliokuwa nao na Marehemu Chachage ambapo waliokuwa na sifa kuliko yeye waliachwa. Naskia hii ilileta mtafaruku kidogo na utawala wa chuo siku zilizofatia. Utiaji shaka wa mienendo ya kutoa ajira katika Idara ya Sociologia na baadhi ya Idara hapo Mlimani ulipelekea kuanzisha utaratibu wa Centralized Recruitment ambapo maombi yote lazima yatumwe kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma yaangaliwe alafu ndo yashuswe idara huska kwa mchako zaidi. NB sifa ambazo ni GPA 3.8 undergraduate anazo ila inasemekana alisaidiwa sana kuandika Dissertation

Pia zilikuwepo taarifa kuwa Misanya Bingi hupata shida sana katika kufundisha. Sikumoja alisikika mwanafunzi mmoja akisema "Misanya anachukua notice toka wikipedia hivyo hataka ukikosa kipindi chake huna cha kupoteza" !!!!!!!!!!!!!!

hapo kwenye red kama wameanzisha utaratibu huo pale UDSM basi itasaidia kuifanya UDSM kuwa Equal Opportunity Employer!!!!!, maneke zamani bila kumjua MUKANDALA basi hata ujifue vipi ama upasue vipi hupati teaching positions. Kwa mademu ilikuwa hadi jamaa ale mzigo ndio utapewa chance ya kuwa Tutorial Assistant. Kuna wadada tulipokuwa freshers walikuwa walokole lakini huyo profesa hapo juu akawatia majaribuni....wengine hadi leo hii wamekuwa wakifundisha pale Pol. Science:coffee:
 
Elimu yetu wa-TZ hiyo!!! Unatamba kwa kuingia lecture hall kwa machale! Pole sana, ndo maana hata tukipambanishwa na wakenya tunatoka kapa tunabaki kulalama tu ooh kampuni hii inaupendeleo sijui kitu gani!! Ni maarifa gani uliyo nayo ya kupambanua mambo kama siyo unalingishia cheti cha daraja la juu wakati maarifa hola?

Kwa kweli utabaki na hicho cheti lakini mara nyingi kazini utakuwa unachemsha maana huna maarifa na ujuzi unaohitajika kazini wewe ulibaki kukazania kufaulu mitihani na siyo kupata maarifa! Pole sana na endelea kutamba na hiyo shahada yako!!
Job K
kusema kweli sitambii cheti, ningetaka kutambia ningeshasema nimesoma nini, wala sitambii gredi wala GPA, ningeshasema nimepata nini.

Mlimani nilikwenda kusoma kwa raha zangu, sio ili nipate ajira, nilichosomea nimekisoma just for the love of it na sio kusakia ajira, ninachofanya hakihusiani kabisa na nilichosoma, sikuwahi kuomba kazi popote kwa hicho cheti cha UD na kubwa kuliko hata cheti chenyewe sinacho!. Nilisoma na nilihitimu ila sikuwahi kukifuata au kukichukia hicho cheti unachodhani ninatambia, ila kwa vile ni changu sikumoja nitakifuata japo nikiweke tuu kabatini kwa maana kwenye mambo yangu, bado sija kihitaji na sijakitumia na heunda nisikitumie kabisa maana shughuli ninazofanya hazihitaji cheti chochote, ujuzi wowote, wala maarifa yoyote!.

Back to the Topic, Misanya Bingi is good kwa anachokifanya, kutoka mtangazaji mpaka mhadhiri wa Ph.D is a great leap na anastahili pongezi zetu.

Kuna baadhi yetu huwa ni hatters, kila kwenye mafanikio ya wenzetu, tunaweka hates zetu ili tu minimize mafanikio hayo, hizi pia ni siasa za 'maji taka'!.
 
Jamani naomba kuuliza, kuna yule jamaa aliyekua ni mtangazaji wa Redio 1 kipindi cha nyuma kwa jina Misanya Bingi hivi kaendaga wapi? kuna mtu anataarifa zake nikazipata? Asanteni.

Sio misanya bingi pekee!!, na yule dj rankim ramdhan na yule mtangazaji taji liundi, a.k.a master t, nao wako wapi? Nakumbuka kama walikuwa wote na misanya
 
Alikuwa anawika sana miaka michache ya nyuma akiwa RadioOne Sterio lakini siku hizi simsikii kabisa hata kwenye vituo vya radio zingine, amefuria kabisa?
 
Ni mwanazuoni. Baada ya kuhitimu BA akabakizwa chuoni hapo UDSM sehemu ya mlimani kufundisha sosholojia.
 
Back
Top Bottom