Wapi naweza kupata kuku wa kienyeji kama wale wa KFC?

Wapi naweza kupata kuku wa kienyeji kama wale wa KFC?

Ndio maana huwa sipendi kuku wa kienyeji. Kuku mgumu utafikiri nini, siwezi kuumiza taya zangu kisa kuku wakati kuna option ya kuku laini.
Mkuu pole sana aseeh. Mnawezaje kula kuku unatafuna kila kitu hadi mfupa? Yan huyo kuku hana tofauti na biskuti. Hao kuku hawashuki kabisa
 
Kuki wa KFC Wana kuwa imported Toka South Africa na Kenya

Kulikuwa na Kampuni Tanzania ya waitaliano I aotwa Amadoli sijui kama Bado wapo walikuwa supplier wakubwa wa KFC
Upo sahihi.
 
Kuna statyle wanapikwa wanakuwa watamu, kuku anachemshwa anacharangwa then wanachanganya na viazi viliyopobdwa ba viungo, then ngano alafu anarostiwa
 
Siku moja nikasema nisipitwe na mie niende kfc kula kuku maweeeeee midude haina ladha mbali na kuungwa kwa viungo viiingi bei haiendani na uhalisia kiufupi hamna kitu sirudii tena
 
Wale kuku ni imported ndugu, wanakuja washachinjwa.ushasikia KFC wanauza filigisi?kingine ni utaalamu wa mapishi.
Hapo kuna ngano zimewekwa huko sijui viungo gani pia.
Kuku ni wa hapa hapa Tanzania.
 
Chemsha kidogo kuku huyo wa kienyeji... Mfanyie marinating.. Weka tangawizi.. Kitunguu saumu na limao, vinegar na majinamoto... Baada ya ku fanya hivyo... Weka nyama hiyo kwenye bakuli kubwa... Mimina soda ya coke then funika kwa foil paper au kama bakuli iko na mfuniko unafunika like 10min.

Pasua mayai kadhaa... Changanya na viungo kama chicken masala na pili pili manga... Kitunguu saumu cha unga.. Then weka na unga laini wa ngano... Tumbukiza vipande vya nyama kwenye mchanganyiko huo... Then Tumbukiza kwenye mafuta yaliyochemka vizuri... Wache iive vizuri ndani ya mafuta..

Hapo utapata crunch chicken mwenye ladha safi na mtam kabisa kuliko KFC.
 
Ngoja waje kukupa muongozo...
Kama wale wa KFC siyo wa kienyeji na habari zake na mbaya sana...


Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom