Wapi naweza pima ngoma

Wapi naweza pima ngoma

Jamani hawachakachui majibu?

Mkuu, hakuna mtu anaeweza kukuchakachulia majibu... Labda zamani ukikutwa na ngoma dokta anaweza kuogopa kukuambia unaoa maana ilikua ni noma, bora siku hizi kuna madawa ya kupunguza makali.
 
zipo hom kit kwa ajili ya kupima HIV,nina boksi hom ambalo nilinunua S.A,,kila baada ya game kdhaa najipima mwenyewe hakuna kuchakachua na ni siri yangu mwenyewe
 
kama sio wa Iringa kapime tu, maana hao ndo naogopa kamba ikihusika.
 
Nenda NSSF Ubungo, njiani, fasta tena bure tu...

Lakini chukua tahadhari mazee, hivyo vizigo unavyobomoa kisha kuishi wa hofu inabidi uvipunguze kwenye list yako! Maana stigma katika jamii yetu ipo, hata kuelekea kupima tu watu hawachelewi kusema kuwa umeyakwaa mawaya. Na mbaya zaidi ni kuonekana ukitoka kwenye hivyo vi-mobile clinic kisha safari za pharmacy kuongezeka - hakiyanani tena huchelewi kupakaziwa na washenzi kuwa wewe ni 'mchafuzi wa hewa', na kwamba unatumia vidonge!!

Nyani Ngabu, home-test kits zinapatikana Bongo, lakini kuja nazo ni rahisi zaidi kama unasafiri.
Ila mimi kwa kweli hii kitu nahisi itaongeza kasi ya maambukizi kwa watu... NINA SWALI AMBALO HUJIULIZA NA LINAHITAJI MAJIBU YA HARAKA kuhusiana na hili, nalo ni kwamba: Ni muda gani inatumia baada ya mtu kukwaa mawaya kuweza kuonekana kwenye vipimo vya mate, hizo home-kit au vinginevyo vyovyote vile. Na baada ya mtu kukwaa mawaya ni muda gani yanatapakaa hata kuweza kuyanasisha kwa mwenzake?!
Akhsante.
 
Last edited by a moderator:

Nadhani swali lako linajibika kama tukijua kwa uhakika incubation period ya HIV ni muda gani ingawa nadhani inatofautiana baina ya mtu na mtu kulingana na mambo kama antibodies na mengineyo.
 
Sina uhakika kama kimeshaingia bongo ila kama vipi mi naweza kukuletea maana nashuka muda si mrefu.

Mpiganaji, tafazali usinisahau katika ufalme wako. Letea na mimi huu mzigo. Videmu vya bongo havikwepeki bana.
 
Mkuu King Kong III sifanyi kwa uzembe nafanya kwa nguvu kweli kweli mpaka mwenzangu anaridhika

Mpwa, Josephine wa Kingstar ulijilipua kavu? Jamaa yake tushafukia na dongo tani saba majuzi. Hata funza bado hawajaanza kula protini za mjeba.
 
Last edited by a moderator:
...upo tayari kupokea matokeo? Yataka moyo.
 
kuna siku nilikua hospitali moja hapa Dar ya private. Akaja baba mmoja na makelele yake, kama haya "nataka kupima ngoma maana nataka kuanza mazoezi, ili nikipungua watu wasidhani nina ngoma". Watu wote waliokua pale waliangua kicheko. Akaandikiwa aende Lab. Vile mimi ilikua zamu yangu, yule dada wa reception akaniambia, anayejitangaza hivi anapima na majibu wala hafuati. akanionyesha mafaili matatu yamejaa majibu ya waliopima lakini hawakuja kufuata majibu yao.
Fidel80 usije ukawa mmoja wao, makelele mengi halafu uache majibu hospitali. isitoshe hukua na sababu ya kuja hapa. Nadhani nusu ya hospitali sasa hivi wanapima na majibu ni chap chap. Kila la kheri kama kweli unamaanisha au umeamua kustrarehesha MMU.
 
mimi kwakweli kinachonipa tabu ni ule ushauri nasaha doh! Nnapataga presha natamani ingekuwa kama maralia unapimwa na kupewa majibu!
 
Back
Top Bottom